-PIA AMZUNGUMZIA JINSI ALIVYOONDOKA RADIO ONE NA UHUSIANO
WAKE NA MKURUGENZI WA ITV/RADIO ONE.
SEHEMU YA KWANZA.
Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii
wa mtandao wa MO BLOG unaotisha kwa sasa, Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy
Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji
maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo.
MO BLOG: Kitu kingine ambacho MO BLOG ingependa
kufahamu ni kuondoka kwako ITV,
fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?
MILLARD AYO: Ningependa
watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.
Kwanza kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona
na alipanga ndio maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine
nilizo nazo maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na
wasingenifuata.
ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.
ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi
kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.
Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya
‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter.
Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo
zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV. Kusoma
mahojiano yote Bofya Hapa
No comments:
Post a Comment