Wednesday, June 13, 2012

TAMASHA LA 'USIKU WA TUMAINI' KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA

Meneja Matukio wa Ukumbi wa Dar Live, Abdalah Mrisho, akitangaza tamasha hilo mbele ya wanahabari leo (hawapo pichani) katika ofisi za Global Publishers, zilizoko Bamaga Mwenge jijini Dar es Salaam. Kulia ni promota wa ndondi Siraju Kaike na kushoto ni bondia Japhet Kaseba
Mwakilishi kutoka Shirikisho la Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC), Ally Makaranga, akimkabidhi promota wa ngumi, Kaike Siraju (kushoto), kibali kwa ajili ya mpambano kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba kwenye tamasha hilo.
Kaseba akijitapa kumchakaza Cheka kwenye pambano hilo.
 
Diamond akiahidi kutoa bonge la shoo tofauti na alizowahi kuzifanya.
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Jacob Steven ‘JB’, akiahidi kuchezesha wasanii maarufu kwenye kikosi chake. Kulia ni Meneja Matukio wa Dar Live.
Mhariri wa gazeti la Championi, Phillip Nkini, (kushoto) akiuliza swali kwenye mkutano huo.
Kaseba na mpambe wake wakiondoka eneo la tukio baada ya kumaliza mkutano.
Tamasha kubwa la burudani liitwalo ‘Usiku wa Matumaini’ linatarajiwa kufanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Julai 7 mwaka huu. Katika tamasha hilo burudani mbalimbali zitakuwepo zikiwa ni pamoja na mechi ya soka kati wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Flava, mechi kati ya wabunge wapenzi wa Simba SC na wapenzi wa Yanga SC, muziki kutoka wanamuziki mbalimbali akiwemo mkali wa Bongo Flava, Naseeb Abdul ‘Diamond’, na pambano la ngumi kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba. Wasanii wataletwa uwanjani hapo kwa kutumia usafiri wa helikopta.

1 comment:

Anonymous said...

Sasa nimeelewa kwanini blog ya global publishers imegeuka kuwa blog ya dar live...