Dkt.
Alberic Kacou akizungumza na waandsihi wa habari baada ya kumaliza
zoezi la kujitolea damu ambapo amezungumzia changamoto Umoja wa Mataifa
unazokabiliana nazo katika kufanikisha zoezi la kuhamasisha watu
kujitolea damu ambapo ametaja moja wapo kuwa ni ugumu uliopo katika
kuwashawishi watu kujitolea kutokana na fikra watu walizonazo kuhusiana
na kujitolea damu.
Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu akifanyiwa vipimo
vya awali kabla ya kuchangia damu. Kulia Mtaalamu kutoka mpango wa Taifa
wa Damu Salama Bi. Edith Senga.
Hoyce
Temu akiandika taarifa muhimu zinazohitajika kabla ya kuchangia damu.
Kulia ni Data Clerk kutoka mpango wa Damu Salama Janeth Laswai.
Edith Senga akitoa tathmini kwa waandishi wa habari kuhusiana na zoezi zima la utoaji damu linavyoendelea nchini.
Na.MO BLOG TEAM
Umoja
wa Mataifa umetoa wito kwa watanzania wote kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi kujitolea damu ili kufanikisha azma ya serikali ya kuwa na damu ya
kutosha katika benki ya akiba ya damu.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika kituo cha kijitolea damu kilichopo
katika zahanati ya UN iliyopo Kinondoni, Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa Dkt. Alberic Kacou amesema Umoja huo unashirikiana bega kwa bega
na serikali katika kuhamasisha kampeni ya Mpango wa Taifa wa Damu
Salama.
Katika
kufanikisha kampeni ya kitaifa ya Kujitolea Damu, Umoja wa Mataifa
umeweka utaratibu wa kuwa na vituo katika sehemu mbali mbali ambapo
wananchi watakuwa wakijitolea damu, ambapo kwa kuanzia leo kituo kipo
katika klinik ya UN ambako kwa kuonyesha mfano Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa Dkt. Alberic Kacou amejitolea damu.
Afisa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu akizungumza na
MoBlog, amesema kesho tarehe 14 June 2012 ambayo ndio kilele cha Siku ya
Kujitolea Damu Duniani, shughuli hiyo itafanyika katika Ofisi za
Shirika la Afya Duniani – WHO zilizopo mkabala na Hospitali ya Saratani
ya Ocean Road.
Aidha
amewataka wananchi jijini Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi ili
kufanikisha lengo la Siku ya Kujitolea Damu Duniani, na kuwatoa hofu
kuwa sio kweli kwamba ukijitolea damu unapimwa virusi vya ukimwi au damu
yako itapungua.
Viongozi katika ngazi mbalimbali na watu wote mashuhuri wanatakiwa kutumia nafasi walizonazo kuhamasisha watu kuchangia damu.
No comments:
Post a Comment