Rene Meza - Mkurugenzi Mtendaji
Taarifa kwa
Vyombo vya Habari
·
Waandishi wa mitandao ya kijamii na
tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio yao.
·
Tuzo hizo kuitwa “ Tuzo za umahiri wa
digitali za Vodacom”
Dar
es Salaam, 11 julai, 2012....
Kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya
kijamii kutokana na umahiri wao.
Tuzo
hizo ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”,
zitatolewa kwa washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni
kwa mara ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa
mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani
ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo
waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali
kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii
ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko
waliochangia katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi ya sifa
ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni
ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia ueledi wa uandishi na
uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa,
umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
Waandishi wa
mitandao ya kijamii watashindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha
kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
Kampuni ya
Vodacom Tanzania pia itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali,
Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha
kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.
“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa
M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza
shughuli zao”, Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila
mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi
zao nasi tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
1 comment:
Je mtu huyo atajulikanaje, aua kuna jinsi ya kujiunga?
Post a Comment