TAMTHILIA iliyowashika watazamaji kutoka Swahiliwood imerudi katika
staili nyingine inayotarajia kuwashika watazamaji kutokana na maandalizi
yake ilivyotengenezwa na kuwashirikisha wasanii wa awali na wasanii
wapya wenye majina katika tasnia ya filamu, awali kundi ambalo lilikuwa
likionyesha mchezo wake katika televisheni ya Taifa yaani TBC 1,
ilisimama na kuonyesha tamthilia nyingine ambayo imemalizika na kuanza
maandalizi ya Jumba la Dhahabu season 2 inayotarajia kuwateka
watazamaji.
“Siku zote tunajali maoni ya watazamaji wetu ambayo wanatoa kwetu
sisi, wapenzi wengi wameomba tamthilia ya Jumba la Dhahabu iendelee
baada ya kuona katika Dvd ambazo ziliingia mtaani kwa ajili ya mauzo,
kwa sababu tunaamini kuwa watazamaji siku zote ndio mabosi wetu basi
hatuna budi kutekeleza maoni yao na ukweli ni kwamba tunatarajia kuzoa
wapenzi wengi zaidi kuliko awali,”anasema Mr. Chuzi.
Tamthilia ya Jumba la Dhahabu inaandaliwa na Tuesday Entertainment
Ltd chini ya mkurugenzi Tuseday Kihangala na amesema kuwa moja ya sababu
ya Jumba la Dhahabu kujinyakulia umaarufu ilitokana na kuonyeshwa kwa
wiki mara tatu lakini kwa sasa igizo hilo litakuwa likirusha mara tano
kwa wiki yaani kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, pia wale wasanii wote
maarufu waliotamba na kuvuma katika tamthilia hiyo wamerudi wote, akina
Mzee Chilo, Bad boy, Jina Kabula, Winta, Mr. Chuzi na wengine wakali
wataoneka katika tamthilia hiyo itakayorushwa TBC1.
credits: http://filamucentral.co.tz
1 comment:
EEEh Mola, huyo msichana huko nyuma amevaa nini toba??! uwiiii
Post a Comment