MATEJA WAAMBIWA WACHAGUE
MOJA KATI YA KIFO AU KUACHA MADAWA YA KULEVYA.
MO BLOG: Tupe
histioria fupi ya maisha yako..!
MWIRU: Naitwa Zakaria
Antony Mwiru nikiwa mzaliwa wa Kusini mwa Tanzania lakini wazazi wangu
walihamia Dar es Salaam nikiwa na umri wa miaka 2, hivyo nimekulia Dar es
Salaam na kusoma Shule ya Msingi Kinondoni A na Nikasoma Shule ya Sekondari
Kinondoni Muslim mpaka Kidato cha 4 bahati mbaya nilifeli hivyo nikajiunga na
Chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa muda wa miaka 3 nikasoma sanaa za ‘Wood Carvings’,
‘Sculpture’, ‘Painting’ na ‘Ngoma za Utamaduni’.
Baada ya kuhitimu kwa miaka mitatu nilifanya shughuli zangu
za sanaa kwa muda wa kama miaka mitano hivi, na baadae nikajikuta nimeingia
katika sakata la dawa za kulevya.
MO BLOG: Badala ya kuendelea na sanaa uliyojifunza
Bagamoyo ilikuaje ukaingia katika mkumbo wa matumizi ya dawa za kulevya.
MWIRU: Nahisi sababu
iliyonipelekea kuingia kwenye mkumbo wa dawa za kulevya ni kutohisi kuwa na furaha
kwa maisha ninayoishi na nikategemea kwamba nitapata furaha zaidi kama
nitatumia ulevi, kwa hiyo nikaanza na bangi kisha pombe na baadae nikaingia katika matumizi ya Heroin.
Lakini vile vile sikupata ile furaha niliyokuwa naitegemea
na matokeo yakawa mabaya zaidi na baada ya muda mrefu nilichoshwa na ile hali
iliyojaa mateso ndani yake. Kusoma
Mahojiano yote Bofya hapa.
No comments:
Post a Comment