MWENYEKITI wa Chadema wilayani Temeke, jijini Dar Joseph Yona,33, ameeleza A-Z sakata la kutekwa, kuteswa kwake na vijana sita wakati akienda nyumbani kwake Mtoni kwa Azizi Ally.
Akisimulia mkasa huo kwa mwandishi Jumanne akiwa
Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Yona ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu,
Taifa Chadema alikuwa na haya ya kusema:
“ Majira ya usiku nikiwa na baadhi ya vijana wa Chadema Tawi la Ukombozi lililopo karibu na kwangu maeneo ya Benki Klabu, Mtoni kwa Azizi Ally tulikuwa tukiongea.
“ Majira ya usiku nikiwa na baadhi ya vijana wa Chadema Tawi la Ukombozi lililopo karibu na kwangu maeneo ya Benki Klabu, Mtoni kwa Azizi Ally tulikuwa tukiongea.
“Ilipofika saa sita tukatawanyika mimi nikawa naelekea nyumbani,
kabla sijafika mbali nikashitukia vijana sita wakinivamia na kunikaba
kisha kunivua tisheti na kunifunga usoni, wakaniingiza katika gari
ambalo walikuwa wamepaki pembeni.
“Nilipowauliza
mnanipeleka wapi? Wakawa wanajifanya ni askari kwani walikuwa wanasema,
‘tumeshamkamata, tunamleta huko kituoni afande’, tukiwa njiani
waliniambia niseme Zitto ni msaliti badala yake nikawaambia kuwa hilo
waulizeni viongozi wa juu.
“Baada ya kuona tumesafiri kwa muda mrefu niliwauliza mbona hatufiki kituoni? Wakasema wewe ndiye tulikuwa tunakutafuta, utakiona cha moto, usipokufa utawasimulia wenzako. Walinipeleka mpaka kwenye msitu, baadaye ikafahamika kuwa ni Ununio, Tegeta wilayani Kinondoni. Huko walinipiga sana kisha kunitelekeza katika pori hilo nikiwa nimezimia.
“Baadaye nilipata fahamu nikajikokota kwa taabu hadi kwenye nyumba
moja, nikagonga lakini hawakunifungulia. Nikaenda nyumba ya pili kugonga
napo hawakunifungulia. Nyumba ya tatu nilipoigonga wakanifungulia.
Walinishangaa na kuniuliza kulikoni umelowa damu? Nikawaeleza
kilichonipata.
“Watu hao waliwasiliana na polisi ambao walikuja na kunichukua mpaka
hapa Muhimbili nilipofanyiwa uchunguzi nikahamishiwa Taasisi ya Mifupa
na Mishipa ya Fahamu (Moi). Lakini kule porini wale watekaji walichukua
vitu vyangu kama vile simu mbili na pochi yenye fedha na waliondoka
nazo.”
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA NA ULIKE HII PAGE
No comments:
Post a Comment