Baada ya kubadilishwa kuwa secondary tukahamishiwa Gongoni primary kwa mwl Rupiya wakati tulikua tukimwita ticha bigi.
Hapo ndipo tulipo anza mazowea na huyu mdada, baada ya miaka kadhaa kupita tuliwa darasa la 7, ndipo ulipo ubuka mchezo wa (kitoto) kuweka kioo chini ya dawati la wasichana na kuanza kula chabo. Huyu dada kwakua nilimzowea na sikumuogopa nilimfanyia mchezo huo nikiwa na rafiki yangu wa siku hizo, dada akaenda kutushtaki kwa mwl Rupia na bila maelezo tukafukuzwa shule.
Nimekutana na huyu dada mwaka 2013 April pale mwanza, tuliongea mengi na kukumbushana ya kale, akanipeleka lunch kisha tukaachana akarudi kazini kwake, mimi nikaendelea na mambo yangu huku tukiwa tayari tumebadilishana namba.
Baada ya miezi 7 tangu tulipo kutana tumekya na mawasiliano ya karibu kilasiku, lakini chakushangaza jana kanitumia ujumbe kwamba ananipenda sana tena kutoka moyoni na anaomba nimfikirie.
Niko njiapanda wadau, Ushahuri wenu nahitaji...
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA NA ULIKE HII PAGE
No comments:
Post a Comment