Thursday, August 16, 2007

SHOWBIZ!

Ikiwa na kauli mbiu yake, 'Shangwe boda kwa boda' tamasha kubwa la Fiesta, katika Jiji la Dar es Salaam linatarajiwa kufanyika kesho kwenye Viwanja vya Leaders Club, huku Mwanamuziki Kevin Lyttle (Pichani) kutoka Jamaika akiwa ni miongoni mwa wapiga shoo kunako shughuli hiyo.

Kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo la kihistoria, msanii huyo aliyepata kutamba na kazi yenye jina la Turn Me On anawasili leo akitokea Miami, Marekani. "Kelvin atawasili na timu ya watu watano, mwanzo tulikuwa na taarif atatokea New York, lakini ukweli ni kwamba safari yake imeanzia Miami," ilisema sehemu ya taarifa kutoka kwa waandaaji.

Mbali na Kevin, msanii nguli wa muziki wa dansi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Watu wa Congo, Koffi Antonie Olomide ambaye tayari yupo nchini na bendi yake ya Quarter Latin ni miongoni mwa wasanii kutoka nje watakaowapa raha Wabongo, wakati Ngoni atawakilisha kutoka Uganda.

Wasanii wengine watakaokandamiza stejini ni pamoja na D.N.A kutoka Kenya, TMK Wanaume Family na Halisi, Fid Q, Banana Zorro, Z-Anto, MB Dog, Madee, Q-Jay na wengine kibao kwa upande huo wa muziki wa kizazi kipya. Tukirudi kunako sebene (muziki wa dansi), bendi kama FM Academia, Akudo Impact, DDC Mlimani Park (Sikinde) na nyinginezo zitaonesha uwezo wa hali ya juu kesho.
Kutoka katika Familia ya Chamber Squard, msanii Moses Bushangana 'Mez B' aliyepata kutamba na wimbo wenye jina la 'Kikuku', uliokuwa katika staili ya 'Takeu' ameiambia ShowBiz kwamba aina hiyo ya muziki siyo dili tena, ndiyo maana ameamua kubadili muelekeo.
Msanii huyo alitamka kwamba hana mpango wa kuendelea na Takeu kwa sababu hivi sasa hauna soko na sio muziki wa kweli, isipokuwa wakati ule aliimba kwa sababu za kibiashara tu.
"Baada ya kuachana na Takeu, sasa nakuja na staili yangu yenye jina la Bongo R&B na tayari nimeshaanza kuitumia katika kile kibao changu kinachokwenda kwa jina la 'Nimekubali' ambacho ndani yake nimemshirikisha Mheshimiwa Temba.
"Kazi yangu nyingine iliyopo hewani kwa sasa ya 'Tuheshimiane' nayo nimeimba kwa Staili ya Bongo R&B na ndani yake nimekamua na AY (Ambwene Yesaya) na Prof. Jay (Joseph Haule)," alisema Mez B.
Aidha, Moses aliongeza, ameamua kuwashirikisha wakongwe hao katika 'pini' hiyo kwakuwa ni watu wazima wenzake: ÒSasa hivi niko bize na maandalizi ya video ambayo itaanza kuonekana siku si nyingi, hiyo ni utambulisho wa albamu yangu mpya itakayoitwa 'Kasuku wange'.


Msanii Rehema Chalamila, Ray C, ambaye bado yuko ziarani Ulaya, ameiambia ShowBiz kwamba atakaporejea kutoka Mamton atafanya maajabu katika anga za muziki wa kizazi kipya, inaletwa kwenu na Mariam Mndeme.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya barua pepe (internet) binti huyo alisema kwamba ameamua kutoa kauli hiyo kwa sababu shule anayoendelea kuipata katika ziara yake hiyo ni ya nguvu, kwani amekuwa akikutana na mastaa wakubwa duniani katika baadhi ya shoo anazofanya, "Lengo siyo kufanya shoo peke yake, pia najifunza ni vipi wenzetu waliondelea wanafanikiwa katika shoo zao jukwaani kwa kuwateka mashabiki wengi.

Na wale wanaosema siku hizi nimepunguza kukata mauno waje kwenye shoo zangu, nitakaporudi.

No comments: