
Shinikizo la chini la damu (LOW BLOOD PRESSURE):
LISHE NDIYO SULUHISHO PEKEE
Kama ilivyo shinikizo la juu, shinikizo la chini la damu (Low Blood Pressure) nalo ni miongoni mwa matatizo ya kiafya yanayowakumba watu wengi. Tatizo hili pia nalo, kama tutakavyoona katika makala haya, linasababishwa na kukosekana kwa virutubisho muhimu mwilini kotokana na mtu kuwa na staili mbaya ya ulaji.
MTU MWENYE LOW BLOOD PRESSURE HUJISIKIAJE?
Watu wenye tatizo la shinikizo la chini la damu hujisikia kuchoka choka kila wakati na kuhisi mwili kuishiwa nguvu. Wakati mwingine mtu huyu huweza kuanguka na kuzimia kama kiwango cha shinikizo la damu kikishuka sana.
Chanzo kikubwa cha tatizo la shinikizo la damu la chini, kama lilivyo lile la juu, ni ulaji wa vyakula usio sahihi na staili mbaya ya maisha. Mwili unapokosa lishe inayotakiwa, husababisha matatizo ya kiutendaji katika mfumo mzima wa mishipa ya damu, hasa kwenye tishu. Mara nyingi watu wenye tatizo hili huwa na upungufu wa kalori, protini, vitamin C na B.
SABABU NYINGINE ZA LOW BLOOD PRESSURE
Licha ya ukosefu wa lishe mwilini kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha tatizo hili, lakini pia kuna sababu zingine, ikiwemo upungufu na uvujaji wa damu kidogo kidogo mwilini yanayosababishwa na matatizo ya kiafya aliyonayo mtu.
KIAZIKISUKARI KAMA TIBA YA LOW BLOOD PRESSURE
Kama kuna zao ambalo linaongoza katika kutoa ahueni na tiba ya shinikizo la damu la chini, basi ni juisi ya Kiazikisukari (beetroot). Anachotakiwa kufanya mgonjwa, ni kunywa kikombe au glasi moja ya juisi ya Kiazikisukari mara mbili kwa siku na ataona mabadiliko makubwa ndani ya wiki moja tu.
Zao hili halijulikani sana nchini, lakini linapatikana katika baadhi ya sehemu, kwa Dar es salaam linapatikana kwenye soko la kisutu au Kariakoo na linajulikana kwa jina la 'bitiruti'. Bila shaka zao hili linatoka mikoani lakini sijajua ni mkoa upi unalima kwa wingi.
VIRUTUBISHO KAMA TIBA YA LOW BLOOD PRESSURE
Ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi, Vitamin C na makundi yote ya Vitamin B, ndiyo suluhisho pekee la kudumu katika kuzuia na kutibu ugonjwa wa shinikizo la chini la damu. Virutubisho hivyo utavipata kwa kula aina mbalimbali za mboga na matunda kwa wingi na kiasi fulani cha maziwa, samaki na kuku.
CHUMVI KAMA TIBA YA LOW BLOOD PRESSURE
Kwa watu wanaokabiliwa na shinikizo la damu la chini, ulaji wa vyakula vyenye chumvi kwa wingi ni muhimu kwao hadi hapo shinikizo la damu linaporejea katika hali yake ya kawaida. Pamoja na kula vyakula vyenye chumvi, pia unywaji wa glasi moja ya maji yaliyochanganywa na chumvi nusu kijiko cha chai, husaidia katika kupandisha kiwango cha presha.
Tiba ya shinikizo la chini la damu kwa kutumia lishe, haina budi kulenga katika kuhuisha mfumo mzima wa mwili. Kwa kuanzia, mgonjwa wa tatizo hili, anatakiwa kula mlo wa matunda pekee kwa muda wa siku tano mfululizo, kwa siku ale mlo huo mara 3 na mlo mmoja upishane masaa 5 na mlo mwingine.
Baada ya kula matunda kwa muda wa siku tano, mgonjwa anaweza kuanza kula lishe ya maziwa na matunda kwa wiki mbili au tatu. Baada ya hapo, mgonjwa ale mlo kamili wenye mazao ya nafaka, kama karanga, korosho, mahindi na bila kusahau mboga za majani.
MAZOEZI NA MAPUMZIKO
Mbali ya kula lishe iliyotajwa hapo juu, vile vile mgonjwa wa Low Pressure anashauriwa kufanya mazoezi mepesi ya kutembea, au kuogelea, au kuendesha baiskeli na atumie muda wake mwingi kupumzika kwenye hewa safi na ya asili. Asipende kufanya sana kazi na ajiepushe kujiweka kwenye mazingira ya kuwa na wasiwasi kila wakati.
No comments:
Post a Comment