Monday, November 24, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Joe Thomas
Boyz II Men
Boyz II Men, Joe Thomas, Tanya Stephens,Tanto Metro & Devonte kwenye jukwaa moja Leaders Club Dar

Tumewahi kushuhudia shoo kibao za Likizo Tyme tangu ilipoanzishwa miaka kadhaa iliyopita, lakini ya mwaka huu inaweza ikawa kama maajabu. Nasema maajabu kwasababu kwa mara ya kwanza katika tamasha hilo wasanii kibao kutoka pande za Marekani na Jamaika watapanda katika steji moja itakayofungwa ndani ya Viwanja vya Leaders Club, Dare es Salaam Desemba 5, mwaka huu.

Kwa mujibu wa waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Entertainment Masters (EM), shoo hiyo itaanza majira ya saa moja kamili usiku itawakutanisha mastaa kama Joe Thomas, kundi zima la Boyz II Men, mwanadada Tanya Stephens na vijana wanaokomaa katika game ya muziki wa Dancehall, Tanto Metro & Devonte.

Wabongo watapata fulsa ya kujirusha na mastaa hao kwa viingilio vya shilingi lakini moja (VIP A), elfu hamsini (VIP B) na elfu ishirini sehemu ya kawaida. “Hiyo ni kwa wale watakaokata tiketi zao mapema, na watakaokatia getini siku ya tamasha watalipa shilingi lakini moja na elfu ishirini (VIP A), Elfu sitini (VIP B) na elfu thelathini kawaida,”.

Je, wewe mpenzi na shabiki wa wasanii hao, utakubali kushindwa kwenda kuwashuhudia laivu Boyz II Men wanapokuwa jukwaani, Joe Thomas je? Huu ni wakati wako sasa kujiachia na mastaa hao wa R&B huku ukirushwa kwa Dancehall kali kutoka kwa Tanya na Tanto Metro & Devonte. Ebwana Likizo ya mwaka huu usiipimie kabisa.
*****************************************

TMK Family wamwaga misaada kwa wazazi Lindi
Wakiwa ziarani katika Mikoa ya Kusini, TMK Family walifanikiwa kupiga shoo sehemu mbalimbali kama Newala, Masasi, Nachingwea, Liwale, Mtwara na Lindi ambako pia walitoa misaada kama chandalua, nepi za watoto na unga wa ulezi kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Sokoine.

Baada ziara hiyo wataelekea nchini Kenya ambako wataungana na maelfu ya wananchi wa huko katika tamasha kubwa la kumpongeza Rais mteule wa Marekani, Barack Obama litakalofanyika Desemba 6, mwaka huu.
************************
Rihanna: Miaka 20, midume saba!
Ebwana Dah! Unaweza usiamini, hasa wale wasomaji waliotutumia ujumbe mfupi (SMS), huku wengine wakitupigia simu wwakitaka kufahamu, staa wa muziki wa R&B nchini Marekani, Robyn Fenty a.k.a Rihanna amewahi kujiachia na nani kabla ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Chriss Brow hivi saa.

Kakiwa na umri wa miaka 20 tu hivi sasa, kabinti hako kamewahi ‘kujiramba’ na mastaa saba wa kiume. Kwa mujibu wa mtandao wa intaneti kalianza na mchizi wa kundi la Outkast, Andre Benjamin a.k.a Adre 3000 mwaka 2003 hadi 2005, baada ya hapo kaliingilia penzi la Jigga (Jay-Z) na Beyonce kwa kujiachia na Rais huyo wa Roccafella kwa mwaka mzima.

Kabla mwaka 2007 haujakatika vizuri, Rihanna alidata kwa staa wa filamu, Shia LaBeouf ambaye pia aijirusha naye kwa miezi kadhaa kabla hajajiweka kwa ‘Hendsamu boi’, Omarion Grandberry ambaye nyota yake ni Nge. Ndani ya mwaka huo huo, 2007 binti huyo alianzisha uhusano wa kimapenzi na kijana Josh Hartnett, ilipofika 2008 kijana wa ‘masauti’, Chriss Brown aliyegonga ngoma kali ya ‘Gime That’ alimzidi kete mshikaji na kumchukua mrembo huyo.

Huwezi kuamini, wakati ‘Chriss Beez’ akiendelea kujiachia na Rihanna, kijana Dieter Bahlen alimchezea faulo kali kwa kuangusha gari na binti huyo, hatimaye jina lake likaingizwa kwenye listi ya waliowahi kula malove dave na staa huyo wa Umbrella. Mpaka tunakwenda mitamboni haikujulikana mara moja kama kijana huyo aliendelea kuvuta mzigo au la, badala yake tetesi zilizoenea kupitia vyombo mbalibali vya habari zinasema kwamba kabinti hako kana ujauzito wa Chriss Brown. Ebwana Dah!
**********************************

2 comments:

Anonymous said...

its not true for some of them,shia,andre 3000 etc..sio ukweli

Anonymous said...

hata ukibania msg, haisaidii wacha kufatata mambo ya watu.