Friday, December 19, 2008

From China with Love: Sinema ya kimataifa itakayovunja rekodi kesho...

Aileen Francisco, katika filamu hiyo



Na Joseph Shaluwa
Sinema mpya ya Kitanzania ambayo ipo katika kiwango cha Kimataifa inayokwenda kwa jina la From China With Love inatarajiwa kuvunja rekodi sokoni ambapo itaanza kupatikana rasmi mitaani kuanzia kesho Desemba 20, 2008 nchini kote.

Filamu hiyo ambayo imeandaliwa na Kampuni mama ya kudurufu, kutayarisha na kusambaza filamu nchini, Tollwood Movies imechezwa na mastaa wa tasnia hiyo nchini wakishiikiana na wasanii wengine kutoka Ufilipino, China na Canada.

Akizungumza na Championi Ijumaa, jana ofisini kwake Sinza ya Bamaga, jijini Dar es Salaam, Meneja Mradi wa sinema hiyo alisema kila kitu kipo tayari hivyo mashabiki wajiandae kupokea filamu hiyo hapo kesho.

“Haikuwa kazi rahisi kuandaa filamu hii, lakini tunashukuru sasa imekamilika, mashabiki wa sinema Tanzania wasiwe na shaka kwani kesho kutwa (kesho) ni siku yao ya kupata kitu kipya kitakachosuuza nyoyo zao.

“From China With Love ni filamu ya aina yake, imezingatiwa taratibu zote za utayarishaji filamu duniani. Ni filamu ya Kimataifa,” alisema Meneja mradi huyo.

Hii ni sinema ya pili kutayarishwa na Tollywood Movies ikitanguliwa na Fake Pastors ambayo bado inafanya vizuri sokoni hadi hivi sasa.

Stori ya sinema hiyo inasimulia kisa cha msichana wa Kifilipino Aileen (Aileen Fransisco) ambaye alizama mapenzini kwa kijana wa Kimasai Rei (Vincent Kigosi ‘Ray’) ambaye alikutana naye nchini China.

Mapenzi ya wawili hao yalitawaliwa na simanzi hasa baada ya Aileen kukataliwa na mama yake na Rey ambaye alikuwa akimlazimisha amuoe binti wa Kimasai Makule (Jokate Mwegelo ‘Miss Tanzania 2, 2006/2007).

Kutokana na kulemewa na mapenzi kwa Rei, Aileen analazimika kukubaliana na mateso yote ikiwemo kufanyishwa kazi ngumu kama kusafisha zizi la ng’ombe, kusanya kuni porini na kazi nyingine ngumu.

Kubwa zaidi ni pale Aileen alipokeketwa tena kwa kukwanguliwa sehemu kubwa ya mlango wake wa uzazi hivyo kumsababishia matatizo makubwa.

Hadithi ya sinema hiyo imeandikwa na nguli wa hadithi nchini Eric Shigongo na kuongozwa na Muongozaji mkali Hamie Rajab.
Nenda kanunue kopi yako kesho mapemaaaaa!


Ray akimtambulisha mchumba wake Aileen (kulia) kijijini kwa wazazi wake


Jokate (kushoto) akiongea na Ray kuhusu uchumba wao

2 comments:

Anonymous said...

hivi jamani hicho kiwango cha kimataifa mnachozungumzia ndio kipi hicho ama kweli hiki ni kichekesho, kituko,jinsi sanaa ya sinema tanzania ilivyoshushwa hadhi ,tengeneza nyingi ili tuuze zaidi,halafu duh babb kubwa manake hii movie kama ya nigeria vile,bab kubwa ,hivi hizo ni feature films melodrama au ni soaps kama takataka za nigeria .kwa mtaji huo wa mwongozaji hammie rajabu,actors akina jokate ,akina vincent kweli kuna kila sababu ya kuendelea kwa kutokuendela ktk industry hii hapa nyumbani tena
Shigongo ni creative san nina mwa-admire sana isipokuwa hadithi zake ni zile zile zinazoitwa "already done" dizaini za obvious fulani.
haya kwaherini

Anonymous said...

Unajua kuna Sinema na Mchezo wa kuigiza kama ile ya akina Ray ile mingine na hizi naz ndio hizo hizo, maana jamani Sinema si mchezo na hizi Camera zenu za Kitchen Party na Taa za Security Light acheni nyie kutania kazi za watu!!
Ila hongera kwa hatua hiyo.
Major Jr.