Sunday, December 21, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

bongo aambulia namba 2, Miss EA

Mwakilishi wa pili wa shindano la Miss East Africa Burundi, Claudia Nuyimana juzi usiku alitawazwa kuwa Miss East Africa baada ya kuwabwaga wenzake 19 walioshiriki kunako michuano hiyo.

Claudia ambaye ni mwanafunzi wa Stashahada ya Uandishi wa Habari , pia ni mfanyakazi wa kituo cha televisheni cha serikali ya Burundi, alitumia nafasi ya kuwa wa mwisho kujibu swali na kuwafunika washiriki wenzake watano waliomtangulia.

Nafasi ya pili ilikwenda kwa Mtanzania, Annette Mwakaguo wakati Anais Veerapatren wa Mauritius alishika nafasi ya tatu. Kwa matokeo hayo, Claudia amejinyakulia gari aina ya Lexus lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 na mkataba wa kufanya kazi na kampuni ya Rena Events ya Dar es Salaam.

Annete amejinyakulia dola za Marekani 5000 na mkataba wa kufanya kazi na Rena Events wakati Anais alijinyakulia dola 3000 za Marekani na mkataba kama washindi wengine wawili waliomtangulia.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Laura Grenouille wa Mauritius, huku nafasi ya tano ikichukuliwa na Rahwa Ghidey wa Eritrea.

Shindano hilo lilifanyika ndani ya Hoteli ya Club Deluc, nchini Burundi.
**********************************************
Muvi ya from china with love inagombewa kama mpira wa kona
Siku mbili baada ya kudondoka kitaani, filamu ya kimataifa, From China With Love imeonekana kugombaniwa kama mpira wa kona na wapenzi wa sanaa hiyo ambapo wengi waliopata kuiangalia wametoa ushuhuda kwamba ni muvi ambayo haijawahi kutokea nchini na huenda ikaleta mapinduzi makubwa.

Filamu hiyo ambayo tayari imesambazwa karibu nchi nzima, imewafanya baadhi ya watu watamke kwamba, hivi sasa sanaa hiyo Bongo iko juu na huenda siku kadhaa zijazo tutakuwa mbali zaidi tofauti na mwanzo wakati tunaanza, huku Watanzania wengi wakivutiwa zaidi na muvi za nje zikiwemo za Kinigeria.

“Ebwana, From China ni noma, yaani ukiiangalia huwezi kuitofautisha na filamu za nje, tena siyo Nigeria, mbali zaidi, tofauti ni lugha tu. Kwa staili hii hawa Tollywood wataleta mapinduzi makubwa, yaani ni kama wamefungua njia, itabidi wengine wafuate,” alisema Paparazi Venance wa Vingunguti, Dar es Salaam.

Mpenzi mwingine wa filamu za Kibongo aliyepata kuichungulia From China ni Farida Makamba wa Sinza Dar ambaye alisema kwamba, kwa kifupi muvi hiyo haina mpinzani kwani tangu ameanza kuangalia sinema za Kibongo hiyo inaweza kuwa ya kwanza kwa ubora, zaidi amewapongeza waandaaji, Kampuni ya Tollywood.

Muvi hiyo ambayo iliingia sokoni Desemba 20, mwaka huu imewashirikisha mastaa wa nchi tatu tofauti, namzungumzia Aileen, binti kutoka Philippene anayeishi China, Jeff kutoka Canada, Ray, Johari, Jokate, Natasha, Bi. Mwenda, Jokate mwigelo na wengine kibao kutoka Tanzania. Kwa kifupi siyo muvi ya kuikosa kwa wale ambao bado hawajakamata kopi yao.

4 comments:

Anonymous said...

sis wa huko ugaibuni tutaipataje mie niko UK

Anonymous said...

na mimi nilitaka kuuliza swali hilo hilo na sisi huku tutaionaje tuone kazi nzuri unayoisifia ili na sisi tukusifie kama kweli ni nzuri

Unknown said...

Tupatie anwani ya Tollywood, ili tuweze kuagizia hiyo DVD.

Unknown said...

Tupatie anwani ya Tollywood ili tuweze kuagizia hiyo DVD!