"Kiukweli ni shindano zuri, najisikia furaha kushindanishwa na kufikia katika hatua hii. Kwa kifupi nalikubali shindano na nina uhakika wa kuibuka na ushindi.
Shindano la kumtafuta staa wa kike mwenye mvuto wa kimapenzi, ‘Ijumaa Sexiest Girl’ leo linakuletea majigambo kutoka kwa washiriki wawili, Wema Sepetu na Irene Uwoya ambao wamebaki kunako mpambano, kila mmoja akiwania kuibuka na ushindi siku chache zijazo."
_________________________________________________________Shindano la kumtafuta staa wa kike mwenye mvuto wa kimapenzi, ‘Ijumaa Sexiest Girl’ leo linakuletea majigambo kutoka kwa washiriki wawili, Wema Sepetu na Irene Uwoya ambao wamebaki kunako mpambano, kila mmoja akiwania kuibuka na ushindi siku chache zijazo."
Kwa mujibu wa Mratibu wa Shindano, Oscar Ndauka washiriki hawa waliyoingia kwenye fainali kubwa wamepewa nafasi ya kuongea na kujigamba ili wasomaji na mashabiki wa shindano hili wapate fulsa nzuri ya kumchagua mmoja wao ambaye wanadhani anastahili kuibuka na heshima ya kuitwa ‘Ijumaa Sexiest Girl’.
“Unachotakiwa kufanya msomaji ni kuandika ujumbe mfupi (SMS) ukimtaja mshiriki ambaye unadhani anastahili kuibuka na ushindi, kisha tuma kwenda simu namba 0784-275 714,” alisema Ndauka.
________________________________________________________
"Yah! Ni shindano zuri ambalo linakubalika na watu mbalimbali. Naamini lipo bomba kutokana na linavyozungumziwa mitaani. Mimi kama Irene Uwoya nina uhakika kuwa nitaibuka na ushindi kutokana na jinsi nilivyo."
*******

Siku chache baada ya kuachia ngoma yake ya kwanza yenye jina la 2008-2009, kiongozi wa Kundi la TMK Wanaume Family, Said Fella tayari amekamilisha video ya wimbo huo, ambayo pia imeanza kuonekana kunako vituo kadhaa vya televisheni.
Akisema na ShowBiz, Said alitamka kwamba, sasa ameingia kwenye game rasmi, ili kuliongezea nguvu kundi lao badala ya kuwa pembeni akiwaongoza washikaji kwa kidole.
“Ndani ya video hiyo ambayo imefanyika kwa kiwango kikubwa, kiongozi huyo ameonesha uzoefu wa kutosha kwa kupiga shoo kadhaa kana kwamba alikuwa akiimba tangu zamani. Swali linakuja, je, Fella ataweza kubamba kama ilivyo kwa mastaa wengine wa Bongo Flava?
compiled by: mc george
No comments:
Post a Comment