Friday, February 13, 2009

Sasa ni zamu ya Mbeya, Valentine's Day kesho!

Bushoke
Chid Benz stejini
Dogo Mfaume na mwenzake
Maunda Zoro
Ngwea...ilivyokuwa stejini Mwanza uwanja wa Kirumba Jumamosi iliyopita

Baada ya kuangusha shoo mbili kali kwa ajili ya utambulisho wa albamu yake, ‘Dunia njia ‘ mkoani Mwanza wiki iliyopita, msanii Rutta Maximilian Bushoke akiwa na msafara wa mastaa kibao sasa tayari wameshadondoka Mbeya kwa shughuli kama hiyo.

Akipiga stori na ShowBiz, msanii huyo akiwa na vichwa kama Mr. Blue, Ngwea, Squeezer na Steve kutoka Zizou Entertainment, bila kuwasahau Chid Benz, Maunda Zorro na Dogo Mfaume wataangusha shoo ya nguvu kesho ikiwa pia ni siku ya wapendanao (Valentine's Day).

“Pamoja na kupiga shoo ya kuitambulisha albamu yangu, Dunia Njia, pia itakuwa ni shoo maalum kwa ajili ya siku ya wapendanao (ambayo hufanyika Februari 14 kila mwaka),” alisema Bushoke.

Albamu hiyo ya Bushoke imesheheni kazi zaidi ya kumi zikiwemo, Chupa ya Coca, Wanashindwa lala, Nimeshafika, Hala, Dunia Njia uliyobeba jina la albamu na nyingine kibao. Ziara hii inadhamniwa na kampuni ya simu ya Zantel

******
compiled by mc george

No comments: