
Hakuna kitu muhimu kwa mtu mwenye matatizo ya kiafya
Katika makala ya leo, tunaangalia aina ya vyakula anavyopaswa mwenye ugonjwa wa moyo kula, ambavyo vinaweza, ama kudhiti hali yake isiendelee kuwa mbaya ama kupona kabisa, hali kadhali kuepuka vyakula ambavyo akila hufanya hali yake kuwa mbaya zaidi.
ZABIBU
Matunda na mbogamboga kwa ujulma wake, ndiyo vyakula muhimu kwa magonjwa mengi ya moyo, vyakula hivyo vina uwezo wa kudhibiti ugonjwa na kuimarisha moyo, lakini zabibu ndiyo tunda linaloongoza kwa ubora linapokuja suala la kuimarisha afya ya moyo.
Apple
Tunda lingine lililo bora kwa mgonjwa wa moyo, hasa wenye matatizo ya kuwa na moyo dhaifu, ni epo (apple), pendelea kula epo mara kwa mara, ikiwemo juisi yake na matokeo yake yatakuwa mazuri.
KITUNGUU
Unaweza kukidharau, lakini kitunguu kina faida kubwa kwa mgonjwa wa moyo, wataalamu wetu wamekifanyia uchunguzi na kugundua kwamba kitunguu kina uwezo mkubwa wa kurekebisha mafuta ya kolestro mwilini na kuuweka mwili katika hali yake ya kawaida. Kwa matokeo mazuri, kunywa kijiko kimoja (cha chakula) cha juisi ya kitunguu, kila siku asubuhi kabla ya kula.
ASALI
Asali ina virutubisho vya ajabu
Baada ya kuvijua vyakula vya mgonjwa wa moyo, ni vyeme pia kuelewa vyakula unavyotakiwa kuviondoa kwenye orodha yako ya mlo wa kila siku, ambavyo ni pamoja na abidhaa zote zitokanazo na unga mweupe, chai, kahawa, sigara, chumvi, sukari na vitu vingine vitamutamu.
Hayo yakizingatiwa, mgonjwa anaweza kuishi na tatizo la moyo pasinakusumbuliwa kwa kiasi kikibwa na hata dawa anazopewa na daktari wake zitafanyakazi vizuri zaidi. Kwa kila ugonjwa ulionao, ni vyema ukajua nini kizuri, nini kibaya kwa afya yako.
No comments:
Post a Comment