Monday, February 9, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

H.BABA ALA MZINGA NA NDINGA YAKE
2009 umeendelea kuanza vibaya kwa baadhi ya mastaa wa Bongo Fleva, baada ya gari la Joseph Haule ‘Prof. Jay’ aina ya Benz kula mzinga hivi karibuni, msanii hamisi Ramadhani ‘H.Baba’ naye ameponea chupuchupu baada ya gari lake (sports car) kulivaa gari lingine kwa nyuma.
Akipiga stori na safu hii juzi, msanii huyo ambaye bado anaendelea na matibabu baada ya kubanwa na usukani kifuani alisema kwamba, balaa hilo lilitokea majira ya saa sita mchana, Jumapili ya wiki iliyopita kunako Barabara ya Ally Hassan Mwinyi, wakati akitokea kwenye Viwanja vya Leaders Club alipokuwa akifanya mazoezi na timu yake ya Break Point.
“Nilikuwa kwenye spidi kali, ghafla gari moja lililokuwa mbele yangu likafunga breki ghafla, bila kutegemea nikashitukia nimelivaa kwa nyuma, kuna mshkaji mmoja nilikuwa naye mbele akajigonga kwenye kioo, lakini hali yake siyo mbaya sana. Pia taa zote za mbele na shoo yote kwa ujumla ikawa nyang’a nyang’a. Hivi tunavyoongea gari bado lipo gereji na mimi nipo home nauguza maumivu ya kifua.
Sisi Abby Cool & MC George Over The Weekend tunampa pole H. Baba na mshkaji aliyekuwa naye katika gari hilo, ni imani yetu kwamba Mungu atawasaidia, watarudi katika hali zao za kawaida.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@


ANNA PETER KUSEPA REDIONI KAMA RAY C?
Mtangazaji wa Kituo cha East Africa Radio, Anna Peter, ambaye ameamua kujiongezea mkwanja kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, tayari amedondosha ngoma yake ya kwanza yenye jina la ‘Naomba’ akimshirikisha kijana Laurance Malima ‘Marlaw’.


Akiwa amefanya ngoma hiyo chini ya mtayarishaji muziki, Allan Mapigo huku video yake ikiwa imegongwa kupitia Kampuni ya Visual Lab na mtayarishaji Adam Juma, binti huyo amedhamiria kuangusha kazi nyingine kadhaa akiwashiriki baadhi ya mastaa waliyopo kunako mradi huo wa muziki wa Bongo Flava.

Swali lililopo vichwani mwa wapenzi wengi wa burudani ni kwamba, mtangazaji huyo mwenye sauti ya kuvutia akifanikiwa kusimama vyema kunako game hiyo ataendelea kutangaza redioni au atasepa kama alivyofanya msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyekuwa mtangazaji wa Radio Clouds FM?



ANGELINA JOLIE; KABLA YA BRAT PITT ALIJIACHIA NA MASTAA WA KIUME 13
Angelina Jolie ndiye staa wa muvi duniani ambaye tunamcheki leo kupitia safu hii ‘Ebwana Dah!’ yakiwa ni maombi ya wasomaji kibao ambao walitamani kufahamu mrembo huyo aliwahi kuwa na uhusiano na mastaa gani wa kiume kabla hajajiweka kwa Brad Pitt ambaye ndiye mumewe kwa sasa.


Kwa mujibu wa mtandao unaodili na uhusiano wa kimapenzi kwa mastaa mbalimbali duniani, Jolie alianza kujiachia na Daniele Patini, kisha Jared Leto, Michel Comte, Jenny Shimizu, Jonny Lee Miller, Timothy Hutton, Misty Cooper na Billy Bob Thornton.Wengine ni Antonio Banderas, Nicolas Cage, Olivier Martinez, Colin Farrell, Val Kilmer na hatimaye akadondokea kwenye ndoa na Brad Pitt tangu mwaka 2005 hadi hii leo.

No comments: