Inapoelezwa kuwa Bw. Lupoe wa Los Angeles Marekani, alifikia uamuzi wa kuwapiga risasi watoto wake wote watano, mkewe na hatimaye yeye mwenyewe kwa madai ya 'hali ngumu ya kiuchumi', unashindwa kuelewa! Tukio hilo imetokea Marekani, nchi inayoaminika kuwa ni ya Kitajiri na yenye nguvu duniani. sembuse Africa, especially Tanzania? Mlioko ughaibuni, hii imekaaje? Ni kweli kuna maisha magumu kuliko Africa hadi mtu kuona bora afe? tena yeye na familia yake yote? Tunatatizika!
1 comment:
Mrisho, usifanye mchezo na nje ya nchi hususani MAREKANI, ambapo kuna kodi kila kona, maisha ya kiwa magumu ni boa ufe kuliko kuteseka , kwani huko hakuna kuombana wala mjomba wala leo nitaenda kula kwa shangazi ,kesho ka rafiki wiki ijayo naenda kijijini kwa wazazi kuwaacha watoto.
Afrika kuna raha kwani maisha tunayoishi hayatufungi na kukufanya uwe mpweke , unaridhika na ulichonacho na hakuna anayekucheka,
TUKO HUKU lakini tunatamani kurudi huko hata kesho ila jinsi ya kurudi yenyewe ni kasheshe kama sisi tunaosoma tunaomba miaka ipae, asikudanye mtu ABROAD hakuna raha ,raha ziko wapi wakati bila kazi, huli wala hunapa kulala lakini huko kuna watu wanazaliwa hawajui shida, wazazi wako kwaajili yao na hata wakifa wanwarithisha.
Kwani hata wazungu wakija huko afrika hawatamani kuondoka hujiuliziii...
Post a Comment