Friday, April 30, 2010

IJUMAA SHOWBIZ

Kingstone Yuko njia moja kudondoka Bongo
Dogo mwenye heshima kubwa a.k.a full respect kunako music game over the world, Sean Kingstone, yuko njia moja kuja Bongo na anatarajiwa kudondoka soon kwa ajili ya kupafomu after party ya Tuzo za Kili Music Awards 2009 zitakazofanyika Mei 14, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa waandaaji wa mpango mzima, Sean anaye-deserve kukanyaga Walk of Fame, atatua Bongoland siku moja kabla ya tukio hilo ambalo litachukua nafasi ndani ya Ukumbi wa Diamond Jublee, jijini Dar, Mei 14, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba, wadau wanatakiwa kuendelea kupiga kura kwa wingi hadi Mei 8, mwaka huu kwa kuandika neno KILI ikifuatiwa na herufi ya kategori kisha namba ya msanii, mwisho unatuma kwenda 15723 ili kumpa ushindi msanii aliyefanya vizuri 2009. Baadhi ya kategori za waliyotajwa kuwania tuzo hizo ni kama ifuatavyo.

Wimbo Bora wa Taarab (D)
Jahazi Modern Taarab - Daktari wa Mapenzi 21
5star Modern Taarab - Wapambe Msitujadili 77
5star Modern Taarab- Riziki Mwanzo wa Chuki 69
Jahazi Modern Taarab - Roho Mbaya Haijengi 70
Coast Modern Taarab- Kukupenda Isiwe Tabu 40

Wimbo Bora wa Kiswahili (E)
Machozi Band- Nilizama 63
African Stars Band - Mwana Dar es Salaam 57
Top Band - Aisha 06
FM Academia - Vuta Nikuvute 75
Extra Bongo - Mjini Mipango 53
African Stars Band - Shida Darasa 79
Wahapahapa Band - Cheichei 76
K-Mondo - Magambo 80

Wimbo Bora wa Ragga (M)
Dully Sykes - Shekide 71
Bwana Misosi - Mungu Yupo Bize 56
Drezzy Chief - Wasanii 78
Benjamin wa Mambo Jambo - Fly 28
*******************************************

Nature Shavu dodo!
Unbelievable! King wa Miondoko ya Kwaito Bongo, Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’, ameibuka na bonge la surprise akiwa shavu dodo opposite na alivyozoeleka kuwa hawezi kunenepa.

Nature ambaye washkaji flani wa kitaa wanadai kwamba ubonge kwake ni msamiati, alikutana na ShowBiz pande za Ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar last weekend ambapo kulikuwa na shoo ya Habari Ndiyo Hiyo iliyoandaliwa na Vodacom.

Pamoja na kwamba mchizi alionekana fat kimtindo, alikamua ngoma zake mpya na zile za long na kufanikiwa kuwapagawisha maelfu ya mashabiki wake waliofurika siku hiyo akiwa na kundi lake, TMK Halisi mpya.
**********************************************

Mlela Ajitoa Selebuka
Exclusively! Icon wa Bongo Movies aliye pia Ijumaa Sexiest Barchelor 2009, Yusuf Mlela ‘Angelo’, amejitoa kwenye Kinyang’anyiro cha Serebuka ambacho huwa kinachukua nafasi every Tuesday pale Club ya kimataifa ya Billicanas, jijini Dar na kurushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha TBC1 kila Jumapili.

Akistorisha na Showbiz jijini Dar juzi, Mlela ali-reveal kwamba reason ya kuchukua uamuzi huo inatokana na kuhisi kuwa ndani ya mpambano huo kuna mizengwe na kwamba kuna uwezekano mshindi amekwishaandaliwa.

“Truly nahisi kama kuna mizengwe inaendelea na si ajabu mshindi amepangwa. Kwa mfano wiki iliyopita kabla sijajitoa majaji walinilazimisha nicheze wimbo ambao sijaufanyia mazoezi kwa madai kwamba ule niliokuwa nimeufanyia mazoezi umeshachezwa na mshiriki mwingine, hiyo ni sababu nyingine ambayo ilinifanya nihisi nachezewa rafu.” –Mlela.
************************************

Fella Sasa bifu free
Kiongozi wa Crew ya TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa’ ambaye hivi sasa amerudi hewani na video ya ngoma yake mpya ‘Bila kampani’ yuko against na ishu za bifu kati ya kundi lake na wasanii wengine bali anachoangalia ni maisha bora.

Akipiga story na Showbiz jijini Dar juzi, Mkubwa Fella aliweka plain kwamba, kundi lake liko bifu free na ndiyo maana ame-change staili ya ngoma zake na kuhamia kwenye mistari ya kuisaidia jamii zaidi badala ya kuwadisi watu kama alivyofanya kwenye ngoma hiyo mpya.

“Unajua kuna wasanii wengine wanaanzisha bifu makusudi ili waendelee kusikika, kitu ambacho sitaki tena kukisapoti ndiyo maana mimi na TMK kwa ujumla katumebadili aina ya nyimbo zetu. Hivi sasa tunazungumzia matatizo ya kijamii zaidi,” -Fella.

*************************************************

Warembo, wasanii kuvuta tuzo hizi
Kwa mara ya nyigine tena Kampuni inayodili na ishu za burudani, Sliming faces inasimama na tamasha kubwa kwa ajili ya kutoa tuzo kwa wana habari waliotoa mchango mkubwa kwa jamii kupitia vyombo vyao yakiwemo magazeti litakalofanyika Jumapili ya wiki hii kwenye Hoteli ya Regency, Dar es Salaam.

Akipiga stori na ShowBiz Dar es Salaam, juzi, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Carolyine Luyumba alisema kwamba mbali na wana habari wengine watakaoambulia tuzo hizo ni wasanii wa maigizo na wadau mbalimbali wa burudani.

“Wengine ni warembo waliowahi kunyakua mataji mbalimbali, waimbaji, wabunifu wa mavazi na wengine. Lengo kubwa ni kuthamini na kuheshimu mchango walioutoa kwa jamii yetu,” alisema Luyumba.
***************************************

Fainali za talent show kutoa gari leo
Kampuni ya MP Production inayojihusisha na kuinua vipaji vya wasanii wachanga, leo inatarajia kuhitimisha shughuli yake ya kumsaka mshindi ambaye atakabidhiwa gari mpya aina ya Toyota Corola kupitia fainali za talent show search itakayopigwa ndani ya Ukumbi wa Travertine, Magomeni, jijini Dar.

Akistorisha na Showbiz, Bosi wa kampuni hiyo, Martha Rock alisema kwamba, shoo hiyo itasindikizwa na wasanii kibao akiwemo, Aisha Ramadhan ‘Aisha Mashauzi,’ TMK Wanaume, Mashujaa Bendi na Tox Star.

Shughuli hiyo inakujia chini ya udhamini wa Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Championi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda bila kusahau dawa ya Super Gold, Kiboko ya Uchafu.
***********************************************
compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: