Monday, May 3, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ

Banza: Yes, mnaweza kuniita Mr. Deiwaka
Galacha wa muziki wa dansi nchini, Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’ amechana transparent kwamba wadau wanaweza kumuita Mr. Deiwaka kwa sasa, hiyo ni kwa sababu yupo kwenye program ya kupiga deiwaka mpaka kieleweke.

Banaza a.k.a Jenerali, aliipa stori Abby Cool & MC George over the weekend kuwa hivi sasa atakuwa anasimama kwenye majukwaa mbalimbali kama vile Twanga, Akudo na mengineyo na kumwaga vocal mpaka hapo atakapopata kile anachohitaji.

“Usione Kobe kainama ujue ana jambo anatunga. Nipo makini sana. Tayari nina bendi yangu ambayo nimekwishaisajili lakini sijakamilisha vyombo. Sitaki kwenda resi yakanikuta kama yale ya Bambino, umenisoma?” Ndivyo alivyozungumza Banza ambaye katika kuthibitisha yeye ni mwalimu na anakuja vizuri, juzi-kati aliachia ngoma ya taarab ambayo ni project ya Thabit Abdul.
*****************************************

Mlela

Hemed
Yusuf vs Hemed: Bifu lao lapata tiba!
Mastaa wa filamu na mahasimu wa taji la Ijumaa Sexiest Bachelor 2009, Yusuf Mlela ‘the Real Artist’ na Hemed Suleima ‘The Multi Talented’, wamemaliza tofauti zao baada ya kuwekeana bifu kwa muda mrefu.

Yusuf ambaye ndiye Ijumaa Sexiest Bachelor 2009 na Hemed aliyetinga fainali, walikuwa kwenye bifu la ‘mtafutano’ kiasi cha kusemeana mbovu kwenye vyombo vya habari. Yusuf, aliliambia gazeti hili kuwa tayari wamekwishapata tiba ya ugomvi wao na kwamba hivi sasa wanaelewana.

Kuhusu kilichokuwa kinawagombanisha, no one knows! Ila inasemwa sijui ni demu, wengine wanasema madogo hao walirogwa na umaarufu ndiyo maana zikawa haziivi licha ya ukweli kwamba ni washakaji waliokua pamoja kitaa.

Hemed mbali na filamu ni mkali wa R&B, 2009 na mwanzoni mwa 2010 alisumbua sana na vibao Ninachotaka na Ulisema. Ngoma yake ya Alcohol ambayo ameigonga katika miondoko ya Reggae, imemuingiza katika Kili Music Awards.
***************************************


Pipi afanya birthday kichoyo
The real upcoming artist ambaye ni tunda la THT, Doreen Aurelian Ponera ‘Pipi’, wiki iliyopita alisherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa kimya kimya because hakuna aliyemualika.

Pipi, Jumatano iliyopita (Aprili 18, 2010) alitimiza umri wa 18 lakini kwa uchoyo, ikaliwa keki nyumbani kwao Tegeta, ikawashwa mishumaa ya kutosha akaizima, to make a wish! Alipogongwa swali na Abby Cool & MC George over the weekend, alijibu: “Yap, it was my birthday lakini sikuwa na mpango wa kufanya sherehe ndiyo maana nilisherehekea nyumbani, siyo kwamba nilifanya uchoyo.”
*******************************************************

Foxy Brown: Demu hardcore, atoa penzi kwa midume 10
Ni mzuka tena hapa Ebwana Dah! Ndani ya kuta nne, yumo staa wa Hip Hop kutoka pande za wenyewe ilikoanzia, Foxy Brown na hapa inakujia orodha ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti ameweza kudondoka nao kunako uwanja wa mapenzi.

Site ya kiwanja ambayo ime-specialize katika kufunua ishu za faragha za mastaa, inaweka transparent kwamba mdada huyo hardcore tayari amekwishaingia in bed na wanaume 10. Kudadadeki!

Allen Iverson ambaye nyota yake ni Gemini anatajwa wa kwanza, mtu mzima Jay-Z na nyota yake Sagittarius yumo kwenye ‘listi’, Nas Escobar (Virgo) na Ol` Dirty Bastard (Scorpio) kwa nyakati tofauti wamedondoka dhambini na Foxy, ingawa haielezwi ni lini na kwa staili gani.

Kurupt na nyota yake Sagittarius yeye alijiweka kuanzia mwaka 1996 hadi 2000. Hata hivyo Foxy ana skendo ya kuwapanga wanaume, kwani wakati yupo na Kurupt, mwaka 1999 alilegeza kwa Ricardo Brown ambaye pia 2000 walitemana.

Mwaka 2001 hadi 2004, Foxy alituliza mizuka kwa Spragga Benz, 2005-06 akapumzika na Tyson Beckford, pia Rick Ross naye akala kisela. Jina lake kamili ni Inga Fung Marchand, alizaliwa Septemba 6, 1976, Brooklyn, New York, Marekani.
******************

Kilimanjaro Music Awards Zimebaki siku 5
Ni siku tano tu zimesalia kwa ajili ya kukamilisha mpango mzima wa kupiga kura. Yap, Mei 8, 2010 ndiyo itakuwa mwisho na baada ya hapo, wadau watangoja matokeo ambayo yatawekwa plain ifikapo Mei 14, 2010 ambao ndiyo usiku wa Kili.

Sean Kingston atakuwa ndani ya nyumba siku hiyo ndani Diamond Jubilee na kushiriki kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya vizuri Bongo kwa mwaka 2009, halafu siku inayofuata (Mei 15), atagonga bonge la shoo pamoja na washindi wa Kili 2009. Changamka changamka basi kuwahisha kura yako. Hapa chini kuna baadhi ya categories na utaratibu wa kupiga kura.

Wimbo Bora wa R&B (G)

Belle 9 - Masogange 11

Diamond - Kamwambie 22

AT ft Stara Thomas - Nipigie 07

Maunda Zorro - Mapenzi ya Wawili 52

Steve - Sogea Karibu 72

Wimbo Bora wa Hip Hop (J)

Johmakini - Stimu Zimelipiwa 34

Quick Racka - Bullet 67

Chid Benz - Po Pom Pisha 15

Ngwea - CNN 46

Fid Q - Im a Professional 26

Wimbo Bora wa Afrika Mashariki (Q)

Blue 3 ft Radio & Weasel (Goodlife) - Where you are 12

Kidumu ft Juliana - Haturudi Nyuma 38

Cindy - Na wewe 18

Radio and Weasal (Goodlife) - Bread and Butter 68

Kidumu - Umenikosea 37

Mtunzi Bora wa Nyimbo (R)

Mzee Yusuf 61

Mrisho Mpoto 54

Lady Jaydee 41

Banana Zorro 08

Mzee Abuu 60

Fid Q 26

Prodyuza Bora wa mwaka (S)

Lamar 42

Marco Chally 48

Hermy B 30

Allan Mapigo 04

Man Water 45

Video Bora ya Muziki ya Mwaka (T)

Lady Jaydee - Natamani Kuwa Malaika 41

Diamond -Kamwambie 22

A.Y - Leo 01

Banana Zorro - Zoba 08

C Pwaa - Problem 13

Wimbo Bora wa Afro Pop (U)

Banana Zorro -Zoba 08

Alikiba -Msiniseme 03

Marlaw - Pii Pii (Missing My Baby) 49

Mataluma -Mama Mubaya 50

Chegge - Karibu Kiumeni 14

Msanii Bora Anayechipukia (V)

Belle 9 11

Diamond 22

Barnaba 09

Quick Rock 67

Amini 05

Wimbo Bora wa Kushirikiana (W)

AT ft Stara Thomas - Nipigie 07

Ngwea ft Fid Q - CNN 47

Barnaba ft Pipi - Njia Panda 10

MwanaFA ft Sugu, Prof Jay - Nazeeka Sasa 58

Hussein Machozi ft Johmakini - Utaipenda 32

Wimbo Bora wa Mwaka (Z)

Marlaw - Pii pii (Missing My Baby) 49

Diamond - Kamwambie 22

Banana Zorro -Zoba 08

Mrisho Mpoto - Nikipata Nauli 54

Hussein Machozi - Kwa Ajili Yako 31


Kupiga kura, unatuma SMS ukianza na neno KILI unaacha nafasi halafu unaambatanisha na herufi ya kipengele (category) kisha namba ya msanii baada ya hapo unatuma kwenda namba 15723. Mfano, kuchagua Sogea Karibu wa Steve kuwa Wimbo Bora wa R&B. Unaandika KILI G72 kisha unatuma SMS yako kwenda namba 15723.
******************************************


Bongo Fleva: Wakongwe wanawadharau underground, wanapigwa mwereka
Soko la muziki Bongo bado ni la kusuasua. Bongo Fleva hali ni mbaya lakini tunaweza kukupa in brief chanzo cha kuporomoka. Ni wasanii wanaoamini wao ni wakongwe. Hawa hawataki kukubali kwamba fani ni kipaji na wenye navyo ni wengi.


Hakuna anayebisha kwamba soko la muziki kwa sasa limeshikiliwa na underground. Muangalie Belle9, rudisha macho kwa Diamond, tupa shingo kwa Barnabas, geuka kwa Amin, Mataluma vipi? Pamoja na ukweli huo, wasanii ambao wanaamini ni wakongwe zaidi, wanawadharau wasanii hao chipukizi, hawataki kuwapa ushirikiano unaofaa ili kupeleka mbele gurudumu, matokeo yake wapo pale pale. Ni kwa sababu hiyo, ndiyo maana wakongwe hao wanashindwa kuwa na ujanja wa kunakshi nyimbo zao ili zikubalike, yaani ziwe na vionjo vipya.

Tazama sasa, Bongo Fleva inakuwa muziki wa awamu, anaingia huyu, muda wake ukiisha anakuja mwingine. Waliovuma jana leo ni historia, yaani wanashindwa kurudi vizuri. Ni kama Miss Tanzania na simulizi ya kukabidhi taji.

Hakuna msanii anayeweza kuvuma kwa miaka 10 mfululizo bila kuwa na vitu vipya, endapo mkongwe atamshirikisha chipukizi leo, ataweza kuweka vionjo ambavyo vitaonesha mabadiliko kwenye muziki wake. Ona hili, tafuta mkongwe aliyewahi kumshirikisha chipukizi. Unakuja kuona ni Afande Sele na Mr. II peke yao. Afande alimtoa Dogo Dito wakati Sugu yeye alimfanya Afande awepo kwenye ramani.

Muangalia FA, yeye anatoka na Jaydee, kesho Ngwair, keshokuta kamshirikisha Sugu na Prof Jay, akienda Temeke anaamua kwenda sambamba na Inspector Haroun.

Prof Jay naye akitaka kutoa shavu, ataanzia uwanja wa nyumbani na Simple X na Black Rhino ambao ni wadogo zake. Baada ya hapo utamkuta na FA, AY, Ngwair, Jaydee na mastaa wengine.

Hii inamaana kuwa wakongwe hawataki kujichanganya na wanaokuja. Hawana mpango wa kuvuna ladha mpya ambayo ni kitu muhimu katika maendeleo ya muziki.

Kwa kifupi ni kwamba hata staili ya maisha ya wakongwe wa kibongo, inawaweka mbali na underground, hawataki wawasogelee. Hili tunalijua lakini ukweli ni kuwa linawagharimu kwa kiasi kikubwa.

Wangeweza kuchukua mfano Marekani, kule tunda jipya huwa linaliliwa, Lil Wayne alipochomoka tu, wakongwe wakamgombea kufanya naye featuring mpaka amefungwa, tumkumbuke Pharrel William wa The Neptune na wengine.

Leo akina Jigga wanachanganya vionjo vya vya Rock kwenye Hip Hop hii yote ni kutaka kubadilika, kuendelea kuuza. Ona 50 Cent sasa hivi kasi yake ya kuuza imeshuka kwa sababu habadiliki. Ninyi Wabongo vipi?
***************************************************
Compiled by mc george/ijumaa wikienda

No comments: