Monday, April 26, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Hasheem Thabeet: 16 years, aanza mapenzi!
Mzozo unaendelea na safu yako namba moja kwa ishuz za uhusiano wa kunako kitanda Ebwana Dah, inaendelea kusababisha! Utaratibu ni ule ule, jamaa gani, katoka na nani kwa staili na alimrukiaje?

This week hatuendi mbali, tunacheza uwanja wa nyumbani.
Anayejaa kwenye kuta za Ebwana Dah! Ni Diamond Boy wa Bongoland, Hasheem Thabeet Manka. Kwa mujibu wa kauli yake mwenyewe kama tulivyomnasa kutoka Redio ya Watu, Clouds FM, Hasheem alianza mapenzi akiwa na umri wa miaka 16, tena kwa siri sana huku akikwepa mama yake asijue. Hata hivyo, Hasheem akasema kuwa yeye huwa hapendi kuzungumzia mapenzi huku akikazia pointi kwamba mama yake huwa hajui kama mwanaye huwa anayachangamkia mapenzi.

Baada ya hapo, hapa chini kuna nukuu za Hasheem akihojiwa na vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini, pia ‘tall boy’ huyo anayempoteza Shaq … kwa urefu katika ligi ya NBA kwa sasa wiki iliyopita alikuwa ndani ya mjengo wa magazeti pendwa a.k.a Jumba kubwa la udaku (Global).

Aliwahi kukatishwa tamaa “Wakati nipo nafanya mazoezi ya kikapu pale Chuo Kikuu kuna watu walikuwa wanaona napoteza muda, wakawa wanaponda kwa kusema, basket Bongo?” Alivyopewa assignment ya kucheza NBDL, hivyo kuipa kisogo kwa muda NBA, watu wakapoonda! “Watu waliongea sana, walijua mimi nimeshushwa daraja wakati ile ni assignment ambayo nilikuwa nimepewa nimepewa kwa ajili ya kuangalia kile nilichonacho kama naweza kukifanyia kazi.

Nilipewa mechi sita, nikafanya vizuri nne na kurudi NBA ambako nimecheza michezo yote. “Wakati ule nilikuwa sichezi ndiyo maana nikapelekwa NBDL. Ukiwa NBA kila mchezaji ni muhimu wakati nilipokwenda NBDL mimi ndiyo nilikuwa man of the game.

Nilifanya vizuri, hivyo nikathibitisha kwamba kiwango changu kilikuwa sawasawa. “Kuna watu waliponda wakacheka sana, wengine wakamfuata mama, wakawa wanaongea kwa kumkejeli, wakamuuliza, yupo wapi huyo mwanao aliyekuwa anajifanya yupo juu anakuja hapa anazungumza Kiingereza?”

Anavyotaniwa NBA
“Nikiwaambia Tanzania huwa wanasema mimi ni Mfalme, wananitania kwamba nimetoka kwenye eneo langu ambako namiliki watu. “Kobe alinitania, akaniambia yeye huwa anaisikia Zanzibar, eti huku huwa ana dada yake, kwahiyo siku moja atakuja kutembea.”

Safari ya ghafla Bongo
“Nimekuja ghafla, tumepata likizo ya wiki mbili, nikaona nimsapraiz mama. Nililala usiku, asubuhi nikaona nije nyumbani, kwahiyo hata mama alikuwa hajui. Nilijisikia tu kuja nyumbani, you know, nyumbani ni nyumbani.”

Nikiondoka watu wasichonge
“Nimekuja kuna magazeti yataandika Hasheem aingia kinyemela, mimi nimekuja ghafla na hata kuondoka itakuwa hivyo hivyo. Nipo hapa lakini wakati wowote nitapigiwa simu kuwahi mazoezi, kwahiyo watu wasishangae wakiona sipo kwa sababu sitoaga.”

NBA si mchezo
“NBA ni ngumu na ni ligi yenye ushindani, ndani ya miezi sita, tunacheza game 82.”

Saluti kwa Saleh Ally
Alifika Global Ijumaa iliyopita asubuhi, akazungumza machache na kujibu maswali ya waandishi. Kikubwa akiwa mjengoni, Hasheem hakuona soo kumkubali Mhariri Kiongozi wa gazeti la Championi, Saleh Ally. Hasheem alisema kuwa yeye na Saleh wametoka mbali. KALI YA HASHEEM Gari lake halina namba za usajili za kawaida. Lina special number, T SSS 101.
**************************

King of Kiduku wiki ijayo
Ishu iliyodondoka pande hizi hapa kutoka kwa Waandaaji wa Shindano la Mkali wa Kiduku, zinasema kwamba fainali inanukia na kwamba siku si nyingi mshindi atapatikana na kujinyakulia dola 250 za Kimarekani.

Kauli ya Afisa Uhusiano wa Manywele Entertainment anayekwenda kwa jina la Maimartha Jesse amesema, ishu itakuchukua nafasi Jumapili ijayo katika Hoteli ya Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Mchakato wa kupata washiriki wa fainali hizo ulihusisha zaidi ya washiriki 85, ambao baada ya mchujo mkali, makundi matano ndiyo yaliyofuzu kuingia fainali.

Aliitaja zawadi ya mshindi wa pili kuwa ni Music System ‘brand new’ wakati mshindi wa tatu ataambaa na jezi za ukweli. Burudani ya nguvu kutoka kwa Mfalme Mzee Yusuf akiwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab itadodoshwa, huku Mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Simba Sports Club wakiwa ndani na kombe lao wakishuhudia.
*************************


Kili Music Awards 2010: Jaydee, AY, Banana macho kumchuzi!
Ni kama ule msemo wa kitaani, macho kumchuzi akili kukichwa. Mastaa wenye heshima tele katika himaya ya Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘AY’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ na Banana Zorro wote wanaelekeza macho sehemu moja kuwania heshima ya Kili Music Awards 2009.

AY, Jaydee na Banana wakipigana vikumbo na CPWAA pamoja na underground Diamond, wote wanasaka heshima moja kupitia Video Bora ya Muziki ya Mwaka. Category hiyo imepewa herufi T, na kila msanii amepewa code yake ambapo Jaydee na wimbo wake Natamani kuwa Malaika ni 41, AY, Leo ni 01, Diamond, Kamwambie 22, Banana, Zoba 08 na CPWAA, Problem 13.

Kupiga kura kumchagua msanii unayemtaka hapo, unaandika SMS ukianza na neno KILI unaacha nafasi, unaambatanisha na herufi ya kipengele (category), kisha namba za msanii na baada ya hapo unatuma kwenda namba 15723. Mfano, kuuchagua Leo wa AY kuwa Video Bora ya Mwaka, unaandika KILI T01 kisha unatuma SMS yako kwenda namba 15723.
*********************************************


Compiled by mc george/ijumaa wikienda

No comments: