Unene wa mwili wa kupita kiasi (obesity) ni miongoni mwa matatizo ya kiafya yanayowasumbua watu wengi. Kuna njia nyingi za kufanya ili kupunguza unene, yakiwemo mazoezi ya viungo na kutumia baadhi ya vyakula kimpangilio.
Unene wa kupita kiasi ni hali inayomtokea mtu pale mafuta yanaporundikana kwenye ‘tishu’ za mwili hivyo kusababisha matatizo kwenye moyo, figo, ini, viungio vya mwili kama vile magoti, n.k.
Halikadhalika, watu wenye matatizo ya uzito wa kupindukia huweza kupatwa na matatizo pia ya shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya msuli, ini na hata kibofu cha mkojo. Kwa ujumla unene siyo mzuri na ni chanzo cha maradhi mengi hatari. Kama unajali afya yako, unene ni wa kuogopwa kama ukoma.
Habari njema kuhusu tatizo hilo ni kwamba unaweza kujikinga nalo kwa kutumia asali na kama tayari unalo unaweza kulitibu au kulidhibiti kwa kutumia asali kwa kuchanganya na limau kwa utaratibu maalum.
Asali ni tiba nzuri ya kiasili ya kutibu tatizo la unene pamoja na shinikizo la damu, kwani hupunguza mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol) kwa kuyageuza mafuta ya ziada kuwa nishati ya mwili. Mtu unaweza kufunga kula vitu vingine na badala yake ukatumia asali na limau tu kama tiba ya unene, bila kupoteza hamu yako ya kula au nguvu ya mwili.
JINSI YA KUTENGENEZA ASALI NA LIMAU
Kuna imani potofu kwa baadhi ya watu kuhusu limau na asali kuwa ni sumu. Ukweli ni kwamba mchanganyiko huu ambao ni wa ‘alkalaini’ mwilini siyo sumu bali ni tiba kwa matatizo mengi ya kiafya, likiwemo tatizo la unene.
Ili kupata mchanganyiko sahihi, weka asali mbichi kwenye kijiko kimoja kidogo kwenye glasi yenye maji ya uvugu uvugu (siyo yaliyochemka), kisha weka vijiko viwili vya juisi ya limau (saizi ya kijiko cha chai) halafu koroga na unywe mchanganyiko huo.
Kunywa mchangayiko huo asubuhi kabla hujala kitu chochote au unaweza kunywa mchangayiko huo kila baada ya mlo mkubwa au ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi, mchanganyiko huo husaidia usagaji wa chakula na uondoaji wa sumu mwilini.
Katika kutekeleza mpango huu kwa lengo la kupunguza unene, usisahau kuzingatia suala la ulaji wa vyakula vyenye faida mwilini na vinavyoruhusiwa kiafya. Itakuwa ni kazi bure iwapo utatumia tiba ya asali huku ukiendelea na ulaji wa vyakula usiyokubalika kiafya. Halikadhalika mazoezi ya mara kwa mara ni suala muhimu kuzingatiwa.
COCKTAIL YA MATUNDA NA ASALI
Aidha, katika kuimarisha kinga na kuondoa sumu zaidi mwilini, unaweza kutengeneza mchangayiko wa matunda mengi (fruit cocktail) pamoja na asali na kisha ukanywa. Kufanikisha hilo, chukua matunda kama vile epo, nanasi, zabibu, machungwa, karoti na mapera, yaandae vizuri kisha weka kwenye blenda na tengeneza juisi, bila kusahahu kuweka vijiko viwili vya asali mbichi. Tengeneza kiasi cha glasi moja na kunywa wakati ule ule kwa lengo la kupata vitamini zote bila kupotea.
Mwisho, ili kujiepusha na unene wa kupindukia, usipende kula kupita kiasi, hasa vyakula vyenye mafuta, ili hali hufanyi mazoezi wala hufanyi kazi yoyote ya shuruba. Unene ni dalili ya maradhi, jiepushe nao.
6 comments:
Asante kaka kwa ushauri wako mzuri.
mimi nina swali.
Sasa kuna ubaya wowote kunywa hiyo asali na ndimu baada ya kunywa maji? mimi nikiamka tu Kitandani lazima ninywe nusu lita ya maji kabla hata sijashusha miguu yangu chini kutoka kitandani.
kazin njema.
nafikiri haitakuwa na matatizo kwani vyote ni vimiminika, isipokuwa haiwezi kufanyakazi kwa ufanisi zaidi, kwani inashauriwa kunywa limau na asali on 'empty stomach'
asante Bazi
Nashukuru wa ushauri wako, nisaidie jambo moja huku nilipo kupata asali mbichi ni tatizo, sasa nifanyeje kwa hilo, maana asali inayopatikana ni ambayo imeshasindikwa.
Asante
Rukia
Je mchanganyiko wa asali na vitunguu saumu pia unasaidia nini??
Asanten kwa elimu menu
asali mbichi ipoje
Post a Comment