Tuesday, November 2, 2010

SUGU ASHINDA KWA KISHINDO MBEYA MJINI!

hapa akiwa mitaa ya kwa Obama Marekani
...hapa akiwa na mwana hip hop mwenzake Mwana FA (kati) alipomtembelea nchini Marekani hivi karibuni
Ukisikia kizaazaa ndiyo hiki! Mwaka huu tunashuhudia mapinduzi makubwa katika ulimwengu wa siasa baada ya wakongwe na vigogo kushindwa vibaya na kizazi kipya katika nafasi za ubunge nchini. Moja ya mapinduzi hayo ni ushindi wa mwanamuziki wa kizazi kipya na mwanaharakati Joseph Mbilinyi au maaruufu kama Mr II ambaye ameshinda Ubunge Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema...amekuja na matumaini mapya baada ya kukumbwa na misukosuko mingi ya kimaisha katika siku za hivi karibuni...!

1 comment:

emu-three said...

Kabla ya kutoa hoja, naomba niwaimbie kidogo...mmmh, kweli wapo humo akina Komba, ...kwahiyo sio shaka kuwa ipo siku wataanzisha bendi yao ya wabunge!
Lakini msisahau kilichowapeleka, kuachia kazi ya jimbo, au kata lakini pia mpiganie maswala ya `hati miliki ya wanamziki na kazi zao...'