


Ilikuwa ni siku ya Ijumaa ya Januari 7 2011 bendi maarufu ya muziki wa dansi 'Ngoma Africa Band' aka F.F.U yenye maskani huko Ujerumani, iliuweka muziki wa dansi la bongo katika historia ya aina yake pale ilipofanikiwa kuwachanganya mashabiki wa muziki huo katika maonyesho ya "Kunstendorf film and Music Festival" yaliofanyika nchini humo (zamani Yugoslavia).
Kiongozi wa bendi hiyo Ras Makunja aka kamanda wa FFU na kikosi chake waliwasili nchini Serbia Januari 6 2011 na kupokewa kwa shamra shamra kubwa zilizofungamana na msongamano wa mashabiki na mapaparazi.
No comments:
Post a Comment