Pichani
kati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy Mapunda
akikabidhi kombe kwa viongozi wa timu ya Bunge na Timu ya Baraza la
Wawakilishi.Pichani kulia ni Kapteni wa timu ya Bunge,Mh Amos Makala na
kushoto ni Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani
Juma.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda (kulia), akikabidhi vifaa
vya michezo kwa baadhi ya viongozi wa timu ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibar,Mwenyeki wa timu ya Baraza la Wawakilishi,Mh Hamza Hassani
Juma,Meneja Msaidizi wa timu,Mh.Ali Nassor Jazira pamoja na Mh.Dau Hamad
Maulid.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano kampuni ya SBL.Teddy,Mapunda akizungumza mbele ya
wanahabari mapema leo Makao Makuu ya ofisi hizo zilizopo
Oysterbay,jijini Dar,kuhusiana na udhamini wa mechi kati ya Timu ya
Wabunge na Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar,itakayofanyika 9
Desemba kwenye Uwanja wa Uhuru,ikiwa ni sehemu mojawapo ya kusherehekea
miaka 50 ya Uhuru,aidha Teddy amesema kuwa udhamini wa timu hizo
umegharimu kiasi cha zaidi ya milioni 65.
Kapteni
wa Timu ya Wabunge,Mh Amos Makala akizungumza ni namna gani wamejipanga
kuhusiana na mechi hiyo itakayokuwa ya kusisimua dhidi ya mahasimu wao
Timu ya Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar.
Mwenyekiti
wa timu ya Baraza la Wawakilishi nae akifafanua zaidi namna
watakavyowakabili wapinzani wao Desemba 9 mwaka huu ndani ya Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Mawasiliano kampuni yaSBL.Teddy,Mapunda (katikati), akizungumzia
namna udhamini wao utakavyokuwa kwa timu hizo, wengine kulia na kushoto
ni Nahodha wa timu ya Bunge, Mh Amos Makalla na Mwenyekiti wa timu ya
Baraza la Wawakilishi, Mh Hamza Hassani Juma.
No comments:
Post a Comment