Thursday, September 30, 2010

SASA UNAWEZA TAZAMA FILAMU,SERIES NA VICHEKESHO KUPITIA CHEKA UPASUKE...

NAPENDA KUWAPA TAARIFA WADAU WOTE WA CHEKA UPASUKE KUA, PAMOJA NA KUCHEKA PAKA KUPASUKA SASA WATAWEZA ANGALIA FILAMU BILA CHENGA FILAMU MPYA TOKA NJE NA ZENGINE KIBAO KILA SIKU, MTAPATA VINJALI NA KUTAZAMA MKIWA HAPA CHEKA UPASUKE. FILAMU ZOTE NI SALAMA HIVYO BASI KATIKA KUZIDI KUENDELEZA BURUDANI ZAIDI KWA WADAU WA CHEKA UPASUKE NAWASIHI TENA KUENDELEA KUWEPO ENEO HILI MAANA MAMBO ZAIDI PAMBA MOTO BILA KUSAHAU VICHEKESHO BADO VIPO KILA SIKU KAMA KAWAIDA PIA KATUNI . NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZANGU ZA PEKEE KWAKO MRISHO KWA KUENDELEZA GURUDUMU LA BURUDANI.PIA KUWASHUKURU WANANCHI WOTE KUENDELEA KUA PAMOJA KATIKA KUSOGEZA GURUDUMU. ASANTENI SANA.


JINA LA BLOG: CHEKA UPASUKE

JINA LA LINK: http://chekaupasuke.blogspot.com/

KWA PAMOJA TUNAENDELEZA BURUDANI NA HABARI

Wednesday, September 29, 2010

MISS CONGRESS INTERNATIONAL AREJEA BONGO

Mrembo Jullieth William, aliyekwenda kupeperusha bendera ya Tanzania nchini Italy, kupitia shindano la Miss Progress Internatinal lililofanyika Ijumaa iliyopita na kufanikwa kutwaa taji hilo kwa kuwa mshindi wa kwanza, amewasili mchana huu nchini na kuikabidhi bendera ya taifa kwa serikali, huku akipokewa na ndugu na jamaa, PICHANI akipokewa na mama yake mzazi
Akiwa na Mkurugenzi wa mashindano hayo hapa nchini, Beatus Kaboja wa kampuni ya Syscorp Managements.


ELDEE, NAETO C, M.I. and SOUND SULTAN PROCLAIM THEIR PRIDE IN NIGERIA WITH LAUNCH OF “REP 4 NIGERIA”

Naeto C
Naija’s music elite are celebrating Nigeria’s 50th anniversary of independence with the release of Rep 4 Nigeria - a stunning new urban anthem which celebrates the proud spirit of modern Nigeria.

Penned by Nigerian-American rapper and producer, Eldee, Rep 4 Nigeria is an original composition that features contemporary stars Naeto C, M.I. and Sound Sultan.

Commissioned by MTV base (DStv Channel 322) as part of the celebrations for Nigerian independence, Rep 4 Nigeria is a call for young Nigerians to 'rep' their country and their area with pride. Each of the artists involved wrote their own verse, with R&B artist and ‘Naija Ninja’ Sound Sultan writing and performing the infectiously catchy ‘hook’ and chorus.



The music video for Rep 4 Nigeria was directed by video ace Clarence Peters and filmed on location in Lagos, featuring Eldee, Naeto C, M.I. and Sound Sultan. The music video will premiere on MTV base (DStv Channel 322) on Monday 4 October before going on exclusive, A-list rotation on MTV base, guaranteeing at least 30 spins a week for the stirring track.


Commented Alex Okosi, Senior Vice President and Managing Director, MTV Networks Africa, “MTV Networks Africa is thrilled to be the catalyst in the creation of Rep 4 Nigeria, a poignant and inspirational track that shows Nigerian artists affirming their pride and optimism in the 50th anniversary of their nation.”

Music fans can watch the music video of Rep 4 Nigeria or download the track free of charge at www.mtvbase.com from 4 October 2010.

Tuesday, September 28, 2010

P-FUNKY APASUA JIPU!


Producer na mmiliki wa Bongo Records, P.Funky 'majani', ambaye wikiendi iliyopita aliingia katika 'bifu' na Mfalme wa Rhymes Afande Sele, amevunja ukimya na kuongelea tukio hilo. Majani anakiri kumchapa kibao Afande lakini anakanusha kumtolea bastola kama alivyodai Sele na kunukuliwa katika media, Hapa anaelezea kisa kizima na sababu zilizomfanya amuadabishe mfalme huyo wa Rhymes wa Bongo...Bonyeza player msikilize mwenyewe.......

P-funky

JIKINGE AU JITIBU ‘PRESHA YA KUSHUKA ’ KWA CHAKULA

Wiki mbili zilizopita tuliwaletea mfufululizo wa makala mbili kuhusu ugonjwa wa presha ya kupanda (High Blood Pressure) ambapo tuliona namna gani watu tunatembea nao ugonjwa huo bila kujijua, licha ya ukweli kwamba unachukua uhai wetu kila siku. Halikadhalika tuliona aina mbalimbali za vyakula vinavyotoa ahueni ama kinga ya ugonjwa huo. Leo tunaangalia ugonjwa wa presha ya kushuka (Low Blood Pressure) ambao nao ni hatari kama ule wa presha ya kupanda, ukitofautiana kidogo namna unavyomsumbua mtu.

DALILI ZA MTU MWENYE PRESHA YA KUSHUKA
Mtu mwenye ugonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara husumbuliwa na uchovu, mwili kukosa nguvu, kuwa mnyonge na kusikia kizunguzungu. Hali hii hutokea baada ya mzunguruko wa damu kwenye mishipa kuwa mdogo kutokana na kupungua kwa msukumo wa damu hivyo viungo kama moyo, ubongo na viungo vingine kupungukiwa au kukosa damu kabisa.

SABABU ZA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa mujibu wa wataalamu wetu wa masuala ya lishe, sababu kubwa inayochangia ugonjwa huu ni ukosefu wa virutubisho mwilini kunakosababishwa na ulaji usio sahaihi. Mtu anapokuwa na upungufu wa protini, vitamin C au moja kati ya Vitamin B hupatwa na tatizo hili. Aidha, ugonjwa wa presha ya kushuka, wakati mwingine husababishwa na kuvuja taratibu kwa damu mwilini kupitia kwenye utumbo, figo au kibofu. Mbali na matatizo hayo, pia hasira, kupatwa na msongo wa maisha na mawazo mengi, kunaweza kusababisha presha ya kushuka pia.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA PRESHA YA KUSHUKA
Kwa mujibu wa watatifi wa vyakula, wamegundua kuwa juisi ya Bitiruti (beetroot) ina saidia sana mgonjwa anayesumbuliwa na ugonjwa huu. Bitiruti ni aina fulani ya viazi pori ambavyo vinabapatikana kwenye masoko mbalimbali nchini. Mgonjwa anashauriwa kutengeneza na kunywa kikombe kimoja cha juisi hiyo kutwa mara mbilli na anaweza kuona mabadiliko ndani ya wiki moja tu.

KUOGA MAJI YA CHUMVI
Dawa nyingine inayoweza kutoa nafuu na ya haraka kwa mgonjwa wa presha ya kushuka ni kuoga kwa kujiloweka kwenye maji ya chumvi maalum. Chukua kilo moja na nusu ya chumvi, kisha weka kwenye beseni kubwa la maji ya uvuguvugu, koroga kisha ingia ndani ya beseni hilo na ukae kwa dakika 10 hadi 20. Fanya hivyo muda mfupi kabla ya kwenda kulala na usipatwe na baridi.

VIRUTUBISHO KAMA TIBA
Protini, Vitamin C na Vitamin zote za kundi B, vimeonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa kinga au ahueni kwa wagonjwa wa presha ya kushuka. Mlo kamili wowote ulioshehemi vitamini B na virutubisho vingine, ni muhimu kuliwa na mgonjwa wa presha ya kushuka mara kwa mara.

Matumizi ya chumvi nyingi kwa mgonjwa wa presha ya kushuka nayo ni muhimu. Mgonjwa anashauriwa kula vyakula vyenye chumvi nyingi. Aidha, anaweza kunywa maji yaliyochanganywa nusu kijiko cha chumvi kila siku, hadi hapo kiwango cha presha yake kitakaporejea katika hali ya kawaida.

Ili kuliondoa tatizo la presha ya kushuka moja moja, mgonjwa wa presha ya kushuka anatakiwa kuzingatia ulaji wa matunda kwa kiasi kikubwa. Kwa kuanzia, anatakiwa kula mlo wa matunda-matunda tu kwa muda wa siku tano mfululizo, huku akila mlo huo mara tatu kwa siku ukipishana kwa umbali wa masaa matano.

Baada ya hapo, mgonjwa huyo anaweza kubadilisha mlo na ukawa wa matunda na maziwa kwa muda wa wiki mbili hadi tatu. Na baada ya hapo, anatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vyenye virutubisho vya kutosha ili kuimarisha mfumo wa damu mwilini. Na hii ndiyo iwe staili yake ya maisha kila siku, bila kusahahu mazoezi mepesi mepesi, yakiwemo yale ya kuvuta pumzi na kushusha.

SIKU MWISHO ALIPOSEMA 'WILL U MARY ME?'

Mwisho na Mary ndani ya penzi motomoto...lkn litadumu?
...kila mmoja haishi hamu kumuangalia mwenzie
...mates waliwapa kampani, japo kwa tahadhari kubwa
..wawakilishi wa familia ya Mwisho (mwenye rasta) na shangazi wa Mery walioingia mjengoni kwenye engagement party hiyo..hebu angalia jamaa walivyoshangaa jinsi Mwisho anavyokisi na Meryl...wakati Mwisho anaonesha 'kaoza' kabisa kwa kufumba macho, Meryl anaonekana kumdhibiti Mwisho kwa kumuangalia macho yake...unaweza kuhisi kinachoendelea kichwani mwa Uti hapo?

Monday, September 27, 2010

MTV CELEBRATES NIGERIAN INDEPENDENCE WITH ‘I LOVE NAIJA’ WEEKEND

Lagos, 27 September 2010: To celebrate the 50th anniversary of Nigerian independence on 1 October, MTV base (DStv Channel 322, AIT, STV and DBN) is celebrating Nigerian contemporary music with a special I Love Naija themed long weekend running from 1-3 October.

I Love Naija will see MTV base paying tribute to Naija’s finest contemporary musicians with a schedule packed top-to-toe with Nigerian music, artists, interviews and more.

Highlights of the I love Naija weekend will include:

- A special Naija-themed edition of DJ Takeover, hosted by Naija legend DJ Snypes, official DJ to 2Face. Premiering on Friday 1 October at 22:00 CAT, DJ Takeover Nigeria sees DJ Snypes deliver his own mash-up of the finest Naija music videos from the last 5 years.

- Story of Sean Kuti – an intimate portrait of one of Nigeria’s most intriguing music stars (15:45 CAT on Sunday 3 October)

- Leaders of the Nigerian Nu Skool - an MTV base special focusing on the Nigerian hip hop scene at 21:00 CAT on Sunday 3 October

- A rundown of Naija’s Top 20 Best Videos – 18:00 CAT, Saturday 2 October

- A look back at the 2007 MTV/MTN VJ search which launched Cynthia Okpala to TV fame

- A retrospective on BNC Fashionably Loud, the fashion-and-music spectacular on Sunday at 22:00 CAT

- Classic episodes of MTV base Spotlight featuring Styl Plus /Positive Black Soul and 2FACE/Lebo Mathosa.



For MAMA fans anticipating the 2010 awards in Lagos, there will also be a screening of the 2008 MTV Africa Music Awards with Zain from Abuja, Nigeria on Saturday 2 September at 20:00 CAT, and a glance back at the Road To Mama - Lagos on Sunday 3 September at 19:00 CAT.

Later in the month, Naija music fans can look forward to the premiere of a mammoth new music collaboration featuring Dbanj, Eldee, Naeto C, MI, Wande Coal and Banky W on an as-yet un-named track commissioned specially by MTV base and produced by Eldee. The music video of the track, directed by Clarence Peters, will air exclusively on MTV base for a month starting mid-October.

Last but not least, from mid-October, MTV base will also debut Base Select, a hot new interactive weekly request show hosted by MTV VJ Cynthia C-VON Okpala.

WIKIENDA SHOWBIZ!

P. Funk: Bongo Records ni ofisi, si uwanja wa ngumi
Ukiwa pande za Nanjilikitili halafu unasikia sifa za Bongo Records unaweza kudhani ni studio iliyopo kwenye eneo kubwa kama Kariakoo nzima.

Anayepunguza, basi ataamini ni go-down kubwa halafu ndani yake kuna mitambo ya nguvu, Mkurugenzi Mtendaji wake, Paul Matthysse ‘P. Funk’ analindwa na wapambe 50, ukithubutu kumsogelea umeumia.

Bongo Records ina jina kubwa. Ambao hawajawahi kuiona halafu wanaifikiria kwa ukubwa wa kupitiliza wana sababu ya kuifikiria kwa ukubwa huo.

Imewatoa wakongwe wengi tu, Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’, Albert Mangwea ‘Ngwair’ na Jaffari Mshamu ‘Jaffarai’ na wengine wengi.

Mafanikio ya Joseph Haule ‘Prof. Jay’, Haroun Kahena ‘Inspector’ na Gangwe Mob, Wanaume Family na Halisi na utitiri wa wasanii wengi, kwa namna moja au nyingine, Bongo Records na mkono wa P. Funk ‘Kinywele Kimoja’ vimefanya waking’ara.

Tukumbuke kuwa kipindi kirefu Bongo Records ilibaki kuwa mtawala wa soko la Bongo Flava, ingawa kwa nyakati tofauti kulikuwa na ushindani na MJ Production ya Joachim Kimaryo ‘Master J’ na FM Studio wakati huo Mika Mwamba anasababisha.

Hata hivyo, kinachoonekana hapa ni kuwa P. Funk anashindwa kuiheshimu studio yake wala hajali ukubwa wa jina lake na ndiyo maana anakuwa na migogoro ya hapa pale na wasanii ambao wanakwenda kurekodi.

Ukiachana na vilio vya wasanii chipukizi, hata wakongwe nao imeonekana kasi yao ya kwenda studio hiyo imepungua. Kuna tatizo! Ipo sifa inayoenea mtaani kwamba P. Funk ni master wa kusimamia vipaji, kwamba wale ambao hawawezi huwa haoni mbaya kuwatoa nishai. Hataki tu kuchukua pesa ya mtu, anaangalia kwanza kazi anayotengeneza. Anahitaji pongezi!

Hilo sawa lakini migogoro na wasanii wake ya nini? Mastaa wengi wanamuogopa kwa sababu dakika mbili mbele anaweza kubadilika na kufanya kitu cha kushangaza.

Ijumaa iliyopita, Mfalme wa Rhymes, Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, alipita ofisini kwetu akiwa na furaha. Alikuja kutusabahi na baada ya hapo alitupa taarifa kwamba anakwenda Bongo Records kuchukua kazi yake kwa Majani.

Kwamba walikubaliana aende siku hiyo kazi yake ambayo Afande alirekodi na staa wa Ninao Ninao, Ferouz Mrisho Rehani. Dakika 10 nyingi, Afande akawa anazungumzia Kituo cha Polisi kwamba amekwenda kumfungulia mashtaka P. Funk kuwa alimtukana, akampiga kofi na kumtishia bastola.

Hilo ni moja la Afande na hatuwezi kuingia ndani zaidi ya kesi hiyo kwa sababu kada za sheria zinazohusika zitafanya uamuzi lakini hapa tunatoa ushauri kiduchu kwa P. Funk.

Aheshimu studio yake kama kweli muziki ni kazi yake. Migogoro na wasanii hatakiwi kuipa nafasi, zaidi studio iwe sehemu ya heshima (ofisi), siyo eneo ambalo wakati wowote linaweza kugeuzwa ringi ya ngumi.
********************
Blu: Aufuata mfupa uliomshinda Ray C
Bongo Flava legend, Hery Samir ‘Blu’ yupo njia moja kutua nchini Kenya ambako atagonga shoo ya pamoja na staa wa Kidato Kimoja, Juma Issa ‘JI’.


Blu, amepewa dili na promota maarufu Kenya, Sadat Muhindi ambaye hivi karibuni alizinguana na diva wa Bongo Flava, Rehema Chalamila ‘Ray C’.

Kwa mujibu wa Sadat kama alivyozungumza na kona hii wiki iliyopita, Blu atapiga shoo na JI katika shoo maalum ya kulipiga promo Kundi la Maliza Umaskini.
Alisema, Oktoba 8, 2010 Blu na JI watasimama jukwaa moja mjini Embu ambao upo kilomita 120 (maili 75) kutoka Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi.

Sadat alisema, baada ya shoo hiyo, siku inayofuata (Septemba 9), Blu atadondoka Nakuru na katika shoo zote hizo, Maliza Umaskini Family (MUF) watapanda jukwaani na kufanya onesho moja.

Maliza Umaskini ni mradi wa kupambana na makali ya maisha ambao umeanzishwa na Sadat nchini humo na katika kuupiga promo, promota huyo aliingia makubaliano na Ray C lakini walitofautiana na kuvunja mkataba.
***************************************************************

-Ipo siku Nick Minaj atatoana roho na Lil Kim, Foxy Brown
-Mambo yanazidi kukolea, upande mwingine Lil Kim naye ni chuki dhidi ya P Diddy na mkwewe, mama Notorious BIG
Nick Minaj
Nick Minaj
Rapa wa kike anayefanya vizuri zaidi dunini, Onika Tanya Minaj a.k.a Nicki Minaj yupo kwenye bifu la kutisha na mkongwe, Kimberly Denise Jones ‘Lil Kim’.


Bifu la Nicki na Kim limezidi kukolea siku baada ya siku, huku upande mmoja ukionekana kurusha makombora zaidi. Ikionekana Kim anasaka shari, kabla hajamalizana na Nicki, amewarudi Sean Combs ‘P Diddy’ na mkwewe, mama wa legend wa Hip Hop duniani, Christopher Wallace ‘Notorious BIG’, Voletta Wallace.

CHANZO BIFU LA NICK, KIM
Wigi ni alama ambayo imekuwa ikimtambulisha Kim tangu alipoanza kuuza jina lake kwenye muziki wa Hip Hop miaka ya 1995/1996.


Wakati huo, akitambulika kama first lady wa Kundi la Junior M.A.F.I.A pia malkia wa lebo ya Bad Boy Entertainment, Kim alitaka ajulikane kwa mikato yake mbalimbali lakini mwisho wa yote kichwani alimaliza kwa wigi.

Kuonesha kwamba wigi ni nembo ya Kim, katika video ya Hit em Up, Mfalme wa Hip Hop duniani, Tupac Shakur ‘Makaveli the Don’ anaonekana akimvua wigi mrembo aliyemchezesha mfano wa first lady huyo wa Junior M.A.F.I.A.

Nicki alipoanza kutoka, moja kwa moja naye akavamia staili ya kuupara wigi kichwani, Kim akaona hee: “Dogo anaingia kwenye anga zangu!”

Vurugu zikawa zinazagaa kitaani, chini kwa chini ikaelezwa kwamba Nicki aliamua kutoka na wigi kwa sababu ujio wake una maana moja kubwa muhimu, kumfunika moja kwa moja Lil Kim.

Kwa upande mwingine, Lil Kim yeye akawa anafyatua madongo ya wazi kuwa Nicki ni mdogo na hajiwezi, kwahiyo ni aibu kutaka kujifananisha naye.

KIM ALIVYOMCHANA NICKI BUFFALO
Katika shoo yake kwenye Ukumbi wa Buffalo, New York, Marekani Kim alitangaza kuwa anakwenda levo nyingine kwa sababu kuna kidudu mtu anamfuatafuata.


Kim alivua wigi na kuwatupia mashabiki kisha akadai kwamba analipenda lakini ni lazima aende matawi mengine kwa sababu hawezi kufanana na mtu ambaye inaaminika ni Nicki.

“Naenda levo nyingine,” Kim aliwaambia mashabiki wake. “Napenda wigi na kila kitu lakini mimi nipo juu sana ya hili. Nipo juu sana ya hili… nitarudi tena!”

RAY J, KIM WAMSHAMBULIA NICK
Akionesha kwamba hataki kimwana wake achokozwe, Willam Raymond Norwood ‘Ray J’ alipiga dongo kwa Nick wazi wazi kuwa hawezi kuwa sawa na Lil Kim.


Ilikwishawekwa wazi kwamba Ray J ambaye ni kaka mdogo wa staa wa R&B, Brandy Norwood ni mpenzi wa Kim, hivyo kuingia kwake kwenye vita hiyo ni wazi yanakuja mengine.

NI TISHIO LA TUPAC, BIGGIE WA KIKE
Jinsi mgogoro wao unavyokua ndivyo hofu kwamba si ajabu tunapoelekea, Kim na Nicki watarudisha kumbukumbu ya Tupac na BIG ambao mwisho wao kila mmoja ulikuwa kifo cha risasi. Wanazidi kuufanya umma uamini kuwa Hip Hop ni muziki wa fujo kwa sababu bifu kila siku zinaibuka, ingawa wengine hutetea kwamba ni biashara lakini mbona wanauana?

KIM VS P DIDDY & MAMA BIG
Kim kwanza hakubaliani na uundwaji wa filamu ya Notorious ambayo inaelezea maisha ya BIG. Mwana Hip Hop huyo anadai kuwa yeye kama mmoja wa washirika wa matukio muhimu ya BIG katika maisha yake alipaswa kushirikishwa. Analaumu pia kwamba muigizaji, Naturi Naughton ambaye amecheza kama yeye katika filamu hiyo, amemdhalilisha kwahiyo filamu nzima imemchafua.

Katika moja ya intavyuu zake, Kim analaumu kuwa filamu hiyo ni mchezo wa P Diddy na mama yake BIG, kutaka kujipatia fedha. Analaumu kuwa wameamua kwa makusudi kuchafua image yake ili kujipatia fedha.

Hata hivyo, Kim anasifia idea ya filamu hiyo na kuongezea kuwa endapo angeshirikishwa kama ambavyo uhalisia wake umetumika, angeweza kuboresha kwa namna nyingi.

Moja kati ya matukio ambayo yamemuudhi Kim ni pale ambapo mtu aliyeigiza kama yeye (Naturi) anaonekana studio akiwa anaingiza sauti, halafu prodyuza, Jamal Woolard aliyehusika kama BIG, anamkumbatia kwa furaha na kumbusu mkewe, Antonique Smith (kama Faith Evans).

Kwa uhalisia, BIG alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kim lakini baadaye alifunga ndoa na Faith moja ya vitu ambavyo viliibua mtifuano mkubwa miaka hiyo.

Kim anaamini tukio hilo kwamba yeye yupo studio anaingiza vocal halafu BIG anamkubatia na kumbusu Faith, halafu yeye anasita lakini baadaye BIG anamkaripia kwa kumwambia aendelee, limemdhalilisha.

NICKI VS FOXY BROWN
Hayupo kimya na anadisi kwa sana tu! Nicki anawaponda wakongwe wa kike ambao mwisho wa siku inatafsiriwa kuwa madongo ni wazi kwa Lil Kim na Inga D. Marchand ‘Foxy Brown’.


Nicki anarap: “Makahaba wa zamani wanabadili meno yao ya bandia, nilipoingia kwenye game wote wakachezea benchi, na huo urafiki wenu mbuzi naona mnanifuatilia.”

Mistari ya Foxy Brown: “Nawaua hao, nawaua hao, naupoteza upinzani wa kibwege nawaua.” Nicki ameijibu: “Unawaua, unawaua, wewe kahaba mbona mimi nimeshawaua?”

NICKI ALIPOTOKA
Alianza kusugua kwenye mixtapes lakini akapata ngekewa ya kuuza sura kwenye jarida la XXL. Mwaka 2008 alishinda tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike chipukizi ambazo zilitolewa na Undeground Music Awards.


Nicki pia alitoa Bean Me na Up Scotty kwenye mixtape nyingine na April 2009 zilipokelewa vizuri BET na MTV. Mwaka huu, alitoka na albamu yake ya kwanza Pink Friday na wimbo Your Love ndiyo uliomtambulisha vema kwa kupata airplay ya kutosha na kufika namba 14 katika Chati za Billboard Hot 200.

Alishirikiana na wana wa lebo yake ya Young Money kutoa albamu ya ushirika ambayo inaitwa We Are Young Money mwaka 2009. TUZO BET 2010 alibeba nne ambazo ni Mwanahip Hop Bora wa Kike, Msanii Bora Mpya, Kundi Bora (Young Money) Kundi Bora Jipya (Young Money), pia alipendekezwa kipengele cha Chaguo la Watazamaji akashindwa. MTV alipendekezwa kwenye kipengele cha Chaguo la Watazamaji, alipendekezwa pia Teen Choice Awarrds na Mombo Awards.

HUYU NDIYE MPENZI WAKE
Anahusishwa kutoka kimapenzi na mkali wa Hip Hop, Dwayne Michael Carter ‘Lil Wayne’ lakini uhusiano ambao unatambulika ni ule kati yake na mwanamuziki wa lebo za Young Money na Cash Money, Aubrey Graham ‘Drake’.

compiled by Mc Geroge/Ijumaa Wikienda

Sunday, September 26, 2010

TMK WAZIDI KUPASUA KWENYE KAMPENI

Mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Jakaya Kikwete akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni zake mjini Musoma jana na kuapmbwa na shoo kali za wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongo Flava.
Wasanii wa muziki wa Bongo fleva wanaounda kundi la TMK Wanaume Family, wakiongozwa na Mh. Temba (kulia) wakiwaburudisha wananchi wa Musoma wakati wa mkutano wa kampeni za JK jimboni humo jana.


Friday, September 24, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Chuchu Hans Ajifungia ndani saa 24
Nyota wa filamu kiwango ya ‘Roho Sita’ iliyowahi kutikisa Jiji la Bongo, kitambo kidogo kilichopita, Chuchu Hans amesema hivi sasa anaishi maisha ya kutokuonekana mtaani kutokana na kutumia muda mwingi akiwa kajifungia ndani akimuuguza mama yake mzazi anayesumbuliwa na vidonda vya tumbo, Hemed Kisanda alipiga naye stori.

Akizungunza na Ijumaa, Chuchu ambaye siku chache zijazo ataanza kuonekana tena kwenye ulimwengu wa filamu baada ya kushiriki kwenye muvi ya ‘Candle in the wind’ iliyotayarishwa na Kampuni ya Manhatan Production, aliweka wazi kuwa imemlazimu kutumia muda wake mwingi akiwa karibu na mama yake ili kumfariji na kumsaidia kwa kila anachokihataji kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa huo.

“Nampenda sana mama yangu hivyo siwezi kumuacha peke yake katika kipindi kama hiki, niko karibu naye na nina jitahidi kumhudumia kwa kila linalowezekana ndiyo maana hivi sasa sionekani kabisa mtaaani,” alisema Chuchu.

//////////////////////////////////

Will Smith Family: Waonyesha maajabu kwa vipaji, kuzunguka dunia
Nyota wa filamu nchini Marekani, Willard Christopher ‘Will Smith, Jr’ anatarajia kuanza ziara ya kuzunguka nchi mbalimbali duniani akiwa na familia yake kwa ajili ya kukusanya pesa za mfuko maalum wa kusaidia maafa ya kimbunga na mafuriko yaliyolizikumba nchi kadhaa za bara la Asia.

Kwa mujibu wa habari kutoka Miami yaliko maskani ya familia hiyo iliyojaaliwa vipaji kibao zinasema ziara hizo zitaanzia pembe ya kaskazini ya Afrika mapema mwezi Novemba na baadaye kwenye mabara mengine, kabla ya kumalizia huko Asia.

Miongoni mwa watu watakaokuwemo kwenye msafara huo ni pamoja na mke wa nyota huyo ambaye pia ni muigizaji mahiri wa filamu, Jada Pinkett, mtoto wa kwanza wa Willy aitwaye Willard Christopher Smith III, ambaye ni muigizaji na mwanamitindo, Jaden Christopher Syre aliyeigiza filamu ya Karate Kid na Willow Camille Reign ambaye hivi karibuni alisaini mkataba na kampuni kubwa ya Muziki ya Roc National inayomilikiwa na Shawn Carter ‘Jay Z.’

////////////////////////////////////

Kid Bwoy Ahamishiwa ICU!
Kutoka pande za Rock City (Mwanza), mtayarishaji muziki aliyekumbwa na balaa la kuumizwa na mtu asiyejulikana akiwa ndani ya studio yake na kulazwa katika Hospitali ya Bugando, Sandu George Mpanda a.k.a Kid Bwoy amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ‘ICU’.

Akipiga stori na kipindi cha Michano Time kinachorushwa na Kituo cha Radio Passion FM cha Mwanza, chini ya mtangazaji wake Phillbert Kabago katikati ya wiki hii, baba mdogo wa Kid Bwoy, Jose Mpanda alisema kwamba mgonjwa wao amehamishiwa ICU ili kumpa muda mzuri wa kupumzika tofauti na alipokuwa kwenye wodi ya kawaida.

“Napenda kuwatoa wasiwasi ndugu, jamaa na marafiki wa Kid Bwoy kwamba mgonjwa wetu anaendelea vizuri, lakini madaktari wamelazimika kumuhamishia kule kwasababu ya kumpa muda mzuri wa kupumzika. Unajua aliopokuwa amelazwa wodini watu wengi walikuwa wakija kumuona huku wengine wakitumia muda mrefu zaidi kitu ambacho kilikuwa kikimfanya apate muda mchache wa kupumzika,” alisema Jose.

Baba mdogo huyo wa Kid pia alisema kwamba, pamoja na mgonjwa wao kujitambua na kuanza kuongea, wameombwa na dokta anayemshughulikia wasimuulize maswali mengi hasa kuhusiana na tukio zima hadi pale afya yake itakapotengemaa zaidi. Kid alikumbwa na mkasa huo Jumatano ya wiki iliyopita saa 2 usiku akiwa ndani ya studio yake yenye jina la Tetemesha Records. ShowBz inampa pole za kutosha, inaendelea kumuombea apone haraka ili arudi katika hali yake na kulisukuma gurudumu la muziki wa Bongo Flava.

///////////////////////////////////

Diamond Musica Warejea tena stejini
Wakali wa miondoko ya ‘Bodaboda’ Diamond Musica International ‘Vijana Classic,’ kesho wanatarajiwa kurejea jukwaani kuonesha vitu vyao baada ya mapumziko ya wiki moja ya kuomboleza msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wao Msaidizi marehemu, Perfect Kagisa a.k.a P Diddy aliyefariki ghafla Septemba 7, mwaka huu kwa tatizo la shinikizo la damu. George Kayala anashuka nayo.

Mkurugenzi Mkuu wa bendi hiyo, Judith Moshi alisema jana jijini Dar kuwa, leo (Ijumaa) watapiga ndani ya Ukumbi wa Meeda Club – Sinza, na kesho watapagawisha Viwanja vya Leaders huku Jumapili wakionesha uwezo wao wa kucheza na kuimba pande za The River Between Mbezi.

“Baada ya kumpumzika kwa muda wa wiki moja tukiomboleza msiba wa P Diddy, kesho (leo) kama kawaida tutakuwa ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza, Jumamosi tutapiga Viwanja vya Leaders na Jumapili tutapagawisha pande za The River Between Mbezi,” alisema Judith.
///////////////////////


Top 20 Bamiza, ZINAZOTESA Magic FM 92.9
1. Mama ntilie -Jerry/Ray c/AT (1ST WEEK ON NO.1)
2. Bado tunapanda – Tip Top connection (3 WEEKS ON NO.1)
3. Teja - Lady JD
4. Karibu tena - Johmakini
5. Salasala - Godzila
6. Nauza kura yangu - Bonta
7. Shoga-Shaa (3WEEKS ON NO.1)
8. Chembambament-Noorah/Ngweair
9. Demu wangu-Jaffaray/TID (2 WEEKS ON NO.1)
10. Iveta-Sajna
11. Unikimbie-Amini
12. Ngosha the swaga Don-Fid Q
13. Mtoto mtundu-Juma Nature
14. Mkono mmoja - Chege, Wahu,
Temba (3WEEKS ON NO.1)
15. Sina raha-Sam
16. Usije mjini-Mwana fa/AY
17. Kisiwa cha ma lovedavi – Z-Anto
18. Songa mbele-Alpha/AY
19. Tamaa mbaya – 20% (NEW)
20. Mechi za ugenini – Roma (NEW)


compiled by mc george/ijumaa

Wednesday, September 22, 2010

TEARGAS, FALLY IPUPA, BANKY W & DADDY OWEN TO ROCK THE MTV AFRICA MUSIC AWARDS

Change is in the air as MTV and Zain Africa (acquired by Bharti Airtel in 2010) lock down Banky W, Fally Ipupa, Teargas and Daddy Owen to deliver a series of spine-tingling live performances at the upcoming MTV Africa Music Awards with Zain (MAMA). The four artists are the first performers to be announced for the 2010 edition of the Awards, which take place on Saturday 11 December 2010 at the Eko EXPO Hall, Lagos, Nigeria.

Smooth R&B artist Banky W is the first Nigerian artist booked to perform at this year’s show, while South African outfit Teargas will be representing the best of South African Hip Hop on their MAMA debut. Kenya’s Daddy Owen will make his mark as the first ever Gospel singer to perform at the MAMA Awards, showcasing the unique Gospel vibe that’s successfully made the cross-over into the mainstream music consciousness. Congolese star Fally Ipupa makes his second appearance at MAMA, after his exciting collaboration with Mozambique’s Lizha James and Uganda’s Blu3 at MAMA 2009 in Kenya.

Tuesday, September 21, 2010

PRESHA: Muuaji tunayelala na kutembea naye-2



WIKI iliyopita tuliangalia jinsi ambavyo ugonjwa wa presha ulivyo hatari na kuzungumzia dalili ambazo mtu mwenye ugonjwa huo anaweza kuwa nazo. Wiki hii tuangalie vyakula ambavyo mgonjwa wa presha au asiyekuwa na presha anatakiwa kuvila ili kuudhibiti au kujiepusha na ugonjwa huo. Endelea...

ZINGATIA VYAKULA HIVI
Ukisha kuwa mgonjwa wa presha, ulaji wa vyakula vitokanavyo na nafaka halisi, matunda na mboga za majani, linakuwa suala la lazima na siyo hiyari. Mgonjwa wa presha anashauriwa kula zaidi vyakula hivyo na kupunguza ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi, ikiwemo nyama kama ilivyoolezwa awali.

Katika orodha ndefu ya matunda anayopaswa mgonjwa kula na kupata nafuu, ni pamoja na hii ifuatayo, ambayo huweza kutumika pia kama tiba, kwani matunda haya yameonekana kuwa na virutubisho vingi zaidi vinavyoweza kudhibiti presha:

Vitunguu saumu
Kula vitunguu saumu kwa wingi, hutoa nafuu kubwa kwa mgonjwa. Unaweza kula punje mbili hadi tatu kwa siku na kuchanganya kwenye mboga pia.

Limau
Pia penda kula limau mara kwa mara, nalo ni miongoni mwa matunda yanayotoa nafuu kwa mgonjwa wa presha. Limau lina Vitamin P ambayo utaipata kwa kunywa juisi yake au nyama na maganda yake.

Zabibu mbivu
Zabibu nazo zimeorodheshwa miongoni mwa matunda anayotakiwa kula mgonjwa wa presha ili kupata nafuu, nayo yana vitamin P ambayo huzuia kuziba kwa mishipa ya damu.

Tikiti maji
Tikitimaji nalo ni miongoni mwa matunda anayopaswa kula mgonjwa wa presha. Halikadhalika, mbegu za tikiti maji zinaweza kutengenezwa na kuliwa kama dawa inayoweza kumpa nafuu kubwa mgonjwa. Kausha mbegu zake, kisha zikaange, ziliwe mara kwa mara kama karanga.

Mchele
Mchele una kiwango kidogo cha ‘fat’ na pia una kiwango kidogo cha ‘kolestrol’, hivyo kukifanya kuwa chakula bora kwa mgonjwa wa presha. Hivyo wali ni sawa kuliwa na mgonjwa wa presha, hasa ukipata ule mchele usioondolewa virutubisho vyake (brown rice).

Viazi vitamu
Viazi vitamu, hasa vile vya kupika na maganda yake, vinafaa sana kuliwa na mgonjwa wa presha. Viazi vitamu vina madini mengi ya ‘potasiamu’ na havina madini chumvi.

Juisi ya mboga majani
Ulaji wa mchanganyiko wa juisi ya mboga, hasa karoti na mchicha (spinach) ni nzuri sana kwa mgonjwa wa presha, huweza kutumika pia kama tiba. Kunywa glas moja kutwa mara mbili au tatu.

Kwa kuzingatia ulaji wa vyakula vilivyoanishwa hapo juu na kufanya mazoezi mara kwa mara, mgonjwa wa presha anaweza asisumbuliwe kabisa na tatizo hilo na kujihisi kupona hata bila kutumia dawa. Hata hivyo, hilo linawezekana tu iwapo utajitambua mapema na kuanza kuchukua hatua za ulaji sahihi wa vyakula sasa na siyo baadaye!

MWISHO.


Monday, September 20, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Mama wa Mjomba: Dini ya Shetani imempa nafasi kutawala muziki duniani”
Hofu kila kona ni tishio la utawala wa dini ya Shetani. Kwa upande wa muziki, mwana Hip Hop mwenye pesa nyingi zaidi, Shawn Cutter ‘Jay- Z’ au Jigga anatajwa kutawala game kupitia imani hiyo.

Anatajwa zaidi kuamini katika Illuminati au Secret Society (Jamii ya Siri), ingawa lipo tabaka linaloamini kuwa Jigga ni muumini wa Freemasonry. Katika interview tuliyoinasa kupitia YouTube Jigga akizungumzia kuhusishwa kwake na Dini ya Shetani (Illuminati, Freemasonry), anasema kuwa yeye haamini dini, haukubali Ukristo wala Uislamu.

“Watu wanatakiwa kunijua vizuri, waijue imani yangu. Namuamini Mungu, namuamini Mungu mmoja. Siamini dini, Ukristo wala Uislamu.” Mahojiano yapo kama ifuatavyo;

SWALI: Watu wanazungumza wewe ni mfuasi mwaminifu wa Illuminati, Freemason, Dini ya Shetani kitu kama hicho.

JIGGA: No, nashindwa kujua haya yametoka wapi, sijui yameanzaje, kwa kweli siwezi kusema.

SWALI: Watu wanasema kwenye video za nyimbo zako unatumia alama ya Illuminati, labda swali langu ni je, una uhusiano na watu wenye unabii na imani hiyo?

JIGGA: No, siyo mimi. Sijawahi kufanya hivyo. Nimekuwa nikitumia alama hizo kwenye nyimbo zangu kwa sababu naamini zinauza. Labda niseme na watu wajue imani yangu, namuamini Mungu mmoja, siamini dini, siamini jehanamu. Unajua hizi alama huwa nakisia, watu wananiunga mkono. Nafanya shoo na watu tunaonesha alama za kufanana.

SWALI: Umezijuaje wakati ni Jamii ya Siri? Illuminati (secret society).

JIGGA: Yeah, ila kwa sasa ni kundi kubwa. Halafu hizo alama, unajua mimi ni mburudishaji, nazitumia kuburudisha.

SWALI: Ukionesha hizo alama za dini ya shetani mashabiki wanapenda?

JIGGA: Bila shaka.

SWALI: Unafikiri imani hiyo ipo?

JIGGA: Sijui hasa ila watu wanaosafiri duniani wanaweza kufafanua. Sijui kuhusu Dini ya Shetani kwa sababu mimi siyo Tommy Hanks (staa wa filamu ya Illuminati) lakini kuna mtu wangu Young Jeezy ana kitu kuhusu dini hiyo. Nina uhakika Obama (Barack) ana watu hao.

JIGGA NA BEYONCE DINI MOJA
Galacha huyo wa Hip Hop anayeaminika ndiye tajiri zaidi akiwa anamiliki utajiri unaokadiriwa kufikia dola milioni 150 (shilingi bilioni 240), alifunga ndoa na staa wa R&B, aliye memba wa zamani wa kundi marehemu la Destiny’s Child, Beyonce Knowles.

Jigga na Beyonce wamekuwa wakionesha alama za dini ya shetani, hivyo kufanya wote wawili kuwekwa kundi mmoja kwamba like husband like wife wote ni Dini ya Shetani. Wakati mwingine, Beyonce amekuwa akionesha alama za Dini ya Shetani hata katika mazingira ya kawaida, hivyo kuzidi kuuthibitishia umma.

JIGGA NI NGUMU KUWAFANYA WATU WAMUAMINI
Ni ngumu kwa Jigga kuwafanya watu wamuamini yeye siyo Illuminati. Sababu ni hizi;

MOSI: Amesema yeye siyo Mkristo na haamini dini hiyo lakini mbona anavaa msalaba?

PILI: Anasema yeye siyo Freemasonry lakini mbona kwenye wimbo “Run this Town” amejitaja ni muumini wa imani hiyo, pia kwenye video yake amejaza alama za Dini ya Shetani?

TATU: Mbona anapenda kupiga pamba zenye nembo za Illuminati au Freemasonry na mikono yake kuonesha alama hizo?

CHANZO CHA BIFU LAKE NI TUPAC NI ILLUMINATI
Jigga alianza kumshambulia Mfalme wa Hip Hop, marehemu Tupac Shakur ghafla. Hakukuwa na chanzo kinachoeleweka. Katika kukoleza bifu, Jigga akaamua kufanya kazi kwa ukaribu na hasimu wa Tupac wakati huo, marehemu Christopher Wallace ‘Notorious BIG’.

Documentary inayoelezea kifo cha Tupac na dhana ya Illuminati (Tupac’s Death & Illuminati Conspiracy Theory), inafunuliwa kuwa Jigga alianza kumpiga vita gwiji huyo wa mauzo ya Hip Hop baada ya kuponda Dini ya Shetani.

Tupac aliiponda Illuminati. Akasimama mstari wa mbele kuipinga. Hiyo ikawa sababu ya Jigga kumrudi mfalme huyo wa Hip Hop. Documentary hiyo ambayo inahusisha mahojiano na wanamuziki na watu wengine wenye ushawishi nchini Marekani, inasema kuwa kifo cha Tupac kilisababishwa na Illuminati, dini ambayo inatajwa kuwa na nguvu nyingi za giza. Kwamba ili kumuua Pac a.k.a Makaveli The Don, Illuminati walipanda mbegu ya mauaji kwa watu waliotekeleza shambulio la risasi alizopigwa Septemba 7, 1996 kabla ya kufa siku sita baadaye (Septemba 13, 1996).

Inatajwa kwamba ndiyo maana mpaka leo wauaji hawajulikani. Mchongo mzima ulisimamiwa na Jamii ya Siri (Secret Society). Chanzo cha Pac ‘kuidisi’ Illuminati kabla ya Jigga kumgeuka ni kuwa akiwa jela, alipata taarifa kuwa dini hiyo ndiyo ilikuwa inashika mamlaka yote, ilikuwa inaenda kwa kasi na itatawala dunia nzima.

Hilo lilimuudhi Tupac kwa sababu hakutaka kutawaliwa na dini hiyo, kwahiyo akaanza kupambana nayo. Tupac, alikasirika zaidi alipoambiwa kuwa hata kufungwa kwake jela mwaka 1995 ilitokana na nguvu za Illuminati kwa sababu hakutenda kosa ila aliingizwa hatiani.

Skendo ya kubaka iliyompeleka jela ikaelezwa ni kutaka kuchafua sifa yake ya kutetea haki za watu weusi Marekani, kuwapigania wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasi. Moja ya disi, Tupac anaimba: “Mimi ni muuaji wa Bad Boy, Jay Z atakufa pia.” Kuhusu ujumbe wa Illuminati kummaliza, alijibu: “Sijui hayo maneno kapata wapi, kaambiwa na Papa?”

ANASAIDIA JAMII ‘SANA TU’
Nje ya muziki, Jigga hujihusisha katika shuhuli za uhisani. Agosti 9, 2006 alikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati huo, Kofi Annan ofisini kwake, New York na kumuahidi kufanya ziara ya kutoa elimu ya kuhusu upungufu wa maji duniani.

Alilitekeleza hilo, pia akashirikikiana na Umoja wa Mataifa pamoja na MTV kutengeneza documentary ya kampeni ya maji aliyoipa jina, Diary of Jay-Z: Water for Life, na ilirushwa hewani kwa mara ya kwanza Novemba 2006. Akishirikiana na Sean Combs ‘P Diddy’, Jay-Z alitoa dola milioni 1 (zaidi ya shilingi bilioni 1.4) kulichangia Shirika la Msalaba Mwekundu ili kusaidia waathirika wa Katrina.

ANASHIKA NAMBA TATU KWA MAUZO HIP HIP
Unapowaondoa Tupac na ‘mzungu kichaa’, Eminem, Jay Z ndiye anabaki juu yaw engine wote katika mauzo ya muziki wa Hip Hop. Anakadiriwa kuuza nakala kati ya milioni 40 na 50 duniani kote.

ALBAMU ALIZOTOA
Reasonable Doubt (1996), In My Lifetime, Vol. 1 (1997), Vol. 2… Hard Knock Life (1998), Vol. 3… Life and Times of S. Carter (1999), The Dynasty: Roc La Familia (2000), The Blueprint (2001), The Blueprint2: The Gift & The Curse (2002), The Black Album (2003), Kingdom Come (2006), American Gangster (2007) na The Blueprint 3 (2009).

MADEMU ALIOPANDA NAO KITANDANI
Mtu mzima Jigga kwenye sekta ya mapenzi ni mzuri pia, kwani ameweza kutimiza idadi ya wanawake 11 wanaojulikana aliopanda nao itandani.

Anayetajwa wa kwanza ni Blu Cantrell, Foxy Brown anafuatia, Karrine Steffans anaunga listi, pia Jigga alikosa heshima kwa kutoka na shemeji yake, Lil` Kim ambaye alikuwa tulizo la Notorious BIG enzi za uhai wake. Wengine ni demu gangster, Missy Elliott, rapa mgumu, Trina, Carmen Bryan, Amil All Money, Charlie Baltimore, Shenelle Scott na mke wake, Beyonce Knowles.

HOFU YA KUTAWALA DUNIA
Watu wanazungumza kwamba siku zijazo anaweza kutawala dunia kwa upande wa muziki. Baadhi ya video zinatoka sasa na kumchambua kuwa amepewa mamlaka makubwa na Freemasonry. Mahudhurio ya shoo yake ya hivi karibuni alipochangia jukwaa na Eminem kwenye Uwanja wa Yankees, New York, Marekani yalitia mshtuko baada ya kuingiza watu 52,000. Imetajwa kuwa hao walivutwa na Freemasonry, pia ni zawadi kwake.

HUYU NDIYE ZAY -Z
Jina lake kamilini ni Shawn Corey Carter, alizaliwa Desemba 4, 1969, Bedford Stuyvesant, Brooklyn, New York, Marekani, umri wake kwa sasa ni miaka 40. Alitekelezwa na baba yake akiwa mdogo, hivyo kuishi kwa nguvu ya mama. Akiwa na umri wa miaka 12, alimpiga risasi kaka yake begani kwa kumuibia kidani chake. Alisoma George Westinghhouse Career and Technical Education High School, Downtown Brooklyn ambako alikutana na wakali wengine wa Hip Hop, Big, AZ na Busta Rhymes, baadaye alijiunga Trenton Central High School, Trenton lakini akafeli, hivyo kuanza kukomaa na muziki, pia kujihusisha na kuuza dawa za kulevya.
************************************

A.Y: Nawashukuru Wa-TZ, nampongeza Maurice Kirya kwa kutwaa tuzo
Hatimaye zile tuzo za Radio France internationale discoveries 2010 zilizomuhusisha msanii Ambwene Yesaya A.Y zimefanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Jiji la Paris nchini humo huku msanii Maurice Kirya kutoka pande za Uganda akiiwakilisha Afrika vyema kwa kuibuka kidedea.

Akiwa ni msanii pekee kutoka Bongo aliyetajwa kuwania tuzo hizo, A.Y amesema na Abby Cool & MC George over the weekend kwamba anawashukuru Watanzania wote waliompigia kura japo hakufanikiwa kushinda na kwamba amekubaliana na matokeo kwa kumpongeza Maurice Kirya ambaye ni mmoja kati ya wasanii waliotambuliwa na mashabiki wengi Afrika kupitia ngoma yake yenye jina la Binadamu.

“Nawashukuru sana Wabongo, naamini mwakani kama nitachaguliwa tena watanisapoti vya kutosha, lakini pamoja na kushindwa nimefurahi Maurice kupata tuzo kwa sababu sisi Afrika ni mara yetu ya kwanza kuingizwa kwenye tuzo hizo, pia msanii huyo namchukulia kama ndugu yangu ukizingatia kwamba wimbo wangu, Binadamu ndiyo ulimtambulisha kwa mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo,” alisema A.Y.
*********************************

Mama wa Mjomba afariki dunia
MAMA mzazi wa mwimbaji mashairi mashuhuri nchini, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ Mwanaisha Mrisho, amefariki dunia asubuhi ya Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam.

Ijumaa Wikienda lilipata taarifa za msiba huo kupitia kwa msanii na mwongoza filamu nchini, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye alisema mama huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari.

“Mama mzazi wa Mpoto amefariki baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kesho Jumapili asubuhi (jana) tunatarajia kusafirisha mwili wake kuupeleka Rufiji, Ikwiriri kwa mazishi,” alisema Dude kwa majonzi wakati alipoongea na gazeti hili. Dude alisema kwamba mama huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa muda mrefu. Ijumaa Wikienda linampa pole Mpoto pamoja na wote walioguswa na msiba huo. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amen.
*****************************

JI wa kidato kimoja Kutua Bongo na misaada kibao
Staa wa Kidato Kimoja, Juma Issa ‘J.I’ ataporomoka Bongo mwezi ujao kutoa misaada kwa makundi ya watu wenye uhitaji kutokana na matatizo mbalimbali. J.I a.k.a J Inshu, atatua Bongo akiwa na msimamizi wake wa muziki nchini Kenya, Sadati Muhindi na misaada hiyo itatolewa kwa vituo vitano ambavyo vitachaguliwa.

Muhindi, alisema na safu hii wikiendi iliyopita kuwa kila kitu kinafanyika vizuri na kuongeza kuwa J.I nashuka Bongo baada ya kumaliza ziara ndefu Kenya na baadhi ya maeneo ya Kaskazini Mashariki, Tanzania. “J.I anafanya shoo Meru ambayo ni binafsi lakini tutapeleka mbele ziara yake kuanzia Oktoba 9 Malindi na Oktoba 10, Kilifi, Pwani,” alisema Muhindi. Kuhusu kuja Dar, alisema:

“Tutakuja mwezi ujao wakati J.I atakapokuwa anarekodi video ya Kidato Kimoja Remix. Pia ninampango wa kutembelea vikundi vitano vya wanawake na vitano vya watoto na kuwachangia chochote, tutafanya hivyo na J.I.”

J.I amepata shavu hilo la kupiga ziara Kenya kuchukua nafasi ya staa wa Bongo Flava, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye alitibuana na Muhindi. Dogo huyo wa Kidato Kimoja alianza kuusotea muziki tangu mwaka 2004 ambapo alitoa wimbo wa kwanza ulioitwa Malkia, baadaye akatoa Kwenye Tv lakini alibaki kusuasua lakini alipotoka na Kidato mambo yakawa byee.
*****************************
Compiled by mc george/wikienda

Saturday, September 18, 2010

MESHAK & ELINE WEDDING!

Meshak na Eline mambo yao saafi, cheki hapa uone mpango mzima ulivyokuwa: www.harusni.blogspot.com

FFU wa Ngoma Africa Band WAZIDI KUTESA ULAYA

The Ngoma Africa Band aka FFU! kama walivyozoeleka katika shughuli yao!waliacha historia ya kudumu kwa washabiki wa mziki walioudhuria katika maonyesho.

ALAFIA festival siku 29.08.2010 mjini Hamburg,Onyesho hilo la wazi lilifanyikakatika ya kitovu cha mji wa hamburg eneo la Altona,ambako washabiki wa umri tofoutiwaliweza kujimwaga uwanjani wakati bendi hiyo maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya,hilipokuwa ikidatisha hakili washabiki na mdundo wao "Bongo Dansi" kupenya katika kila ghorofa na kutingisha mji huo maarufu.

Ngoma Africa Band aka FFU watatumbuiza katika onyesho lingine AFRIKA FESTIVAL,mjini Jever,uko kasikazini mwa Ujerumani.kwa sasa wanatamba na CD mpya "Jakaya Kikwete 2010" www.myspace.com/thengomaafrica


Friday, September 17, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

Hotpot Family: “Tumerudi na damu changa, wakongwe hatuthaminiwi”
Baada ya kupotea kwenye game ya muziki wa kizazi kipya kwa takribani miaka kadhaa, familia iliyowahi kufanya vyema katika tasnia hiyo, Hotpot Family imerudi upya ikiwa na sura tofauti huku waasisi wake wakiwa na maneno kadhaa ya kuongea.

Akipiga stori na ShowBiz, kiongozi wa familia hiyo, Anselem Typhone Ngaiza ‘Soggy Dog’ alisema kwamba walichokifanya hivi sasa ni kuirudisha familia ikiwa katika muonekano mpya ili kuwapa nafasi chipukizi wanaoibuka waweze kuonekana.

“Unajua siku hizi chipukizi wanapewa nafasi kubwa kuliko sisi wakongwe, ndiyo maana tunakuwa kimya, siyo kwamba sina kazi, nina ngoma kibao ndani lakini sizitoi kwa sababu hiyo, sijajua ni kwanini wadau wanafanya hivyo. Ndiyo maana tumeamua kutoka na vijana.

“Mimi na Suma G kama wakongwe japo hatupewi heshima hiyo tumewapa nafasi kubwa wasanii wanaotoka kupitia Hotpot Family kwenye ngoma tuliyoiachia hivi karibuni ikiwa na jina la Wanamipango iliyofanyika Makavell Records,” alisema.

Kwa upende wake Suma G alisema na safu hii kwamba, Hotpot Family ilikuwa inajipanga na sasa ndiyo kipindi chao cha ‘kushaini’ kwakuwa wamerudi tofauti huku wakiwa na nguvu mpya kutoka kwa vichwa kama Another One, Young Page, Baby Baby, Chorus B, na Blast Salim.
//////////////////////////////////////////////////

Meseji za wasomaji kuhusu bifu la Mlela & Hemed
Kutokana na ufinyu wa nafasi leo imebidi tuwadondoshee baadhi ya meseji zilizotumwa na wasomaji wa ShowBiz kuhusiana na bifu la wasanii Yusuf Mlela na Hemed lililochukua nafasi kupitia baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni. Cheki na meseji hizo hpo chini.

Kadole wa Dar: Mimi nadhani anachokifanya Hemed ni kama ushamba , katika hali ya kawaida huwezi kujisifu mbele ya chombo cha habari kuwa umempiga fulani ngumi. Kwa hili nahisi hakuwa sawa.

Baba Calvin wa Kinondoni Dar: Hawa vijana walitakiwa kutumia busara zaidi kuamua suala lao kwani walinavyokashifiana kupitia vyombo vya habari wafahamu kwamba hata soko la filamu zao wanalichafua. Kama wanaweza bora wawe na wasemaji wao wenye uwezo wa kuchambua jambo la kuongea, ni aibu kwa tukio kama hilo, nathubutu kusema hakuna staa wala supa staa kati yao.

Saida wa Mwanza: Mimi nalipongeza gazeti la Ijumaa kupitia hapa ShowBiz kwa kuliona hilo. Ushauri wangu kwao nawataka kwanza watambue umuhimu wao kwenye jamii, pia watambue kuwa wanatazamwa na watu wengi, wakubwa kwa watoto, hivyo waache bifu zisizokuwa na maana.

Kulwa wa Temeke, Dar: Mlela na Hemed wote siyo mastaa, kati yenu hakuna anayemfikia Kanumba wala Ray. Badala ya kufanya kazi ili mzidi kupaa kisanii mnaanza kutuletea bifu zenu za ajabu, nyie bado ni chipukizi sana fanyeni kazi acheni hizo.

Mussa wa Kilwa Masoko: Hemed unajifanya unajulikana Afrika nzima kwa kipi? Acheni majigambo, nyie bado mna safari ndefu kwenye sanaa hamuwezi kuwafunika wakongwe kwa staili hiyo.

Kalunde wa ILALA, Dar: Nadhani hao jamaa hawajijui kama ni kioo cha jamii, nawashauri waende kwa madaktari kucheki vichwa vyao, kwa maana hadhi waliyonayo kama ni wazima kweli hawawezi kufanya ishu kama hizo za kurushiana maneno machafu kwenye vyombo vya habari.

Mama Idd wa Kigamboni, Dar: Nyie vijana wote ni kioo cha jamii, tumieni busara badala ya kuanza kutukanana ovyo. Hivi mnadhani watoto watajifunza nini kutoka kwenu? Acheni hizo.

Light wa Moro: Namshauri Mlela aachane na bifu kwani anashusha heshima yake katika jamii kwakuwa yuko juu na anajitahidi katika sanaa.

Manyama wa Musoma: Hao wote hakuna staa kati yao kwani tumeshajua hiyo ni janja yao tu ya kujitafutia umaarufu, zaidi wanataka kutujaribu akili zetu.

Paparazi Venance wa Dar: Kama mnafikiri kazi ya sanaa inaboreshwa kwa kuwa na bifu basi Kibongobongo mnajiharibia, hakuna jipya mnalolileta kwetu zaidi ya kutuzingua. Fanyeni kazi, acheni bifu zenu zisizo na malipo, hii Bongo msitake kujifananaisha na akina Kanye na 50 Cent nyie bado andagraundi. Kumbukeni ya Mr. Nice na Dudubaya walivyojimaliza kwa ugomvi wao.
/////////////////////////////////////////////////

Kina Diamond wajikusanya
Msanii Nassib Abdul a.k.a Diamond na wenzake wanaopiga mzigo kupitia lebo ya Sharobaro wameamua kujikusanya na kuunda umoja wenye jina hilo ili kwenda sambamba na makundi mengine yanayopiga mzigo pamoja katika game ya muzuki wa kizazi kipya, Gladness Mallya alicheki nao.

Akisema na ShowBiz kiongozi wa Sharobaro ambaye pia ni ‘mchawi’ wa Diamond kwa kumgongea ngoma za kijanja, Rahim Ramadhani a.k.a Bob Junior alitamka kwamba wameamua kufanya kazi pamoja ili kujiongezea nguvu zaidi tofauti na awali ambapo kila msanii alikua anasimama peke yake.

“Tuko wasanii nane, zamani kila mmoja alikuwa anasimama peke yake, tukaamua kuungana na kutengeneza ngoma yenye jina la Jiongezee ambayo itatutambulisha Sharobaro. Umoja wetu unaundwa na wasanii kama Diamond, Richard Mavoko, Ude Ude, Man Moe, Alinda, Nyoka, Malilo na mimi mwenyewe. Kwa pamoja tunaamini umoja ni nguvu,” alisema Bob Junior.
///////////////////////////////////////////////

Hatumwi mtoto dukani Mbeya, wana wa Uyole, Mafiati,Mwakibete, Mwanjelwa, Isanga, Nzovwe, Soko Matola, Ghana, Majengo na mitaa mingine ya jiji hilo, macho na fikra zao ni sehemu moja tu usiku wa leo. Ni ndani ya Ukumbi wa Mtenda Sunset.

Kunani? Jibu ni kwamba Mgombea Ubunge jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, leo anaweka kando gwanda na kuvaa jeans na baada ya hapo atasomeka katika shoo kali ya Hip Hop lakini atasindikizwa na wana wengine wa muziki wa kizazi kipya.

Sugu a.k.a Mr. II, atapiga mzigo mkali kuthibitisha ukongwe wake wa zaidi ya miaka 20 kwenye MIC, atasimama jukwaani zaidi ya saa nzima akikamua shoo ya kweli ya Hip Hop, lakini watakaoingia ukumbini pia wataburudika na Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, Ferouz Mrisho Rehani, Abbas Hamis Kinzasa ’20 Percent’, Danny Msimamo, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Gerald Mwanjoka ‘G Solo’, Mapacha ‘Maujanja’ na Isanga Family’.

Akifafanua kuhusu kupanda jukwaani na kuvua kombati ya CHADEMA, Sugu alisema nasi kuwa anafanya hivyo leo, ikiwa ni onesho maalum la kukusanya michango ya kampeni.

“Leo gwanda pembeni, navaa jeans na kushika MIC. Jukwaa moja na Afande, Ferouz, Mkoloni, 20 Percent, Msimamo, Isanga Family na wengine. Ni shoo maalum ya kuchangia kampeni. Tumegawa kadi maalum ambapo kuna maeneo zinanunuliwa kama njugu. Kila kadi tunauza shilingi 10,000.”
//////////////////////////////////////////////////

Jennifer Lopez Alamba dili ya Mil. 12 American Idols
Msanii wa R&B pande za Obama, Jennifer Lopez a.k.a J.Lo amelamba dili la kuwa mmoja wa majaji katika shindano la kutafuta vipaji vya kuimba, ‘American Idol’ litakalofanyika hivi karibuni.

Habari zilizoshuka mitandaoni zinasema kwamba J.Lo ataondoka na mkwanja kiasi cha dola milioni 12 kama mshahara wake kwa kazi hiyo kwa siku moja atakayokuwa katika meza ya majaji.

“Ilimchukua muda mrefu wa majadiliano na waandaaji mpaka akakubali kufanya kazi hiyo. Mbali na kuvuta mkwanja huo mrefu, mwanamuziki huyo atakaa katika safu ya majaji kwa mzunguko wa kwanza kisha nafasi yake itachukuliwa na Ellen Degeneres na Aerosmith Rocker.

Jaji pekee aliyefanikiwa kushika nafasi hiyo tangu mwaka jana ni Randy Jackson.

Compiled by mc george/ijumaa

Thursday, September 16, 2010

Nakaaya Sumari aikacha CHADEMA, ajiunga CCM!

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini ambaye alikuwa Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Arusha, Nakaaya Sumari, jioni hii ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Nakaaya katangaza hayo jioni hii mbele ya mgombea urais wa CCM,Dr. Jakaya Kikwete katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati wa mkutano wa kampeni za Wilaya ya Arumeru.

MORE THAN PAIN IKO TAYARI

Hii ni sinema mpya ya Kanumba inayotamba mitaani kwa sasa, wamo Lisa Jensen na Rose Ndauka humo!

Tuesday, September 14, 2010

The Ngoma Africa Band ndani !Afrika Festival,Mjini Jever,

Bendi maarufu ya mziki wa dansi "The Ngoma Africa band" aka FFU,
wanatarajiwa kutungisha jukwaa la AFRIKA Festival,litakalofanyika mjini Jever,Ujerumani ya Kasikazini Jumapili 19-09-2010. Usikose kuwasikiliza at www.myspace.com/thengomaafrica pia unaweza kuwatupia jicho at www.facebook.com/ngomaafrica au www.twitter.com/thengomaafrica

PRESHA: Muuaji tunayelala na kutembea naye


Kifo cha ghafla kinachotokana na shinikizo la damu hushtua watu na kinapotokea, maneno mengi husemwa na wakati mwingine kuhusishwa na imani potofu.

Lakini ni ukweli uliodhahiri kwamba shinikizo la damu ni ugonjwa hatari sawa na muuaji ambaye tunalala na kutembea naye kila siku bila sisi wenyewe kujijua. Wataalamu walioupachika ugonjwa huu jina la Silent Killer hawakukosea.

JITAMBUE
Binadamu hatuna budi kujitambua afya zetu na kuzingatia sana suala la kula vyakula sahihi ambavyo kila siku vinatajwa kuwa ni matunda, mboga, nafaka halisi, kunywa maji mengi na kufanya mazoezi. Mtu unapokuwa katika kundi la wale wasiozingatia masuala ya ulaji sahihi, huna budi kujitambua kwa kuangalia kama nawe unazo baadhi ya dalili zifuatazo:

Kuumwa kichwa mara kwa mara na kwa muda mrefu. Kusikia kizunguzungu mara kwa mara. Kusikia kichefuchefu na kutapika mara kwa mara. Macho kukosa nguvu na kuona maluelue, ni miongoni mwa dalili za shinikizo la damu. Ingawa dalili hizi zinaweza kusababishwa na jambo lingine, lakini kwa kiasi kikubwa ni ishara tosha ya kukufanya ukapime shinikizo lako la damu (presha).

Kama ukiwa na dalili hizo na ikawa ni kweli zinatokana na kuwa na shinikizo la damu, athari zake ni pamoja na mtu kupatwa na kiharusi (stroke), figo kushindwa kufanya kazi (kidney failure), kupatwa na upofu (blindness) au mstuko wa moyo (heart attack) na hatimaye kupoteza maisha mara moja.

JIKINGE
Mtu anaweza kujikinga na ugonjwa wa shinikizo la juu la damu (High Blood Pressure) kwa kufuata staili sahihi ya maisha na kuzingatia ulaji sahihi. Miongoni mwa vitu vya kuzingatia katika mlo ni kula vyakula vyenye virutubisho vya asili na kuepuka kula vyakula vya mafuta mengi.

Aidha, kuacha tabia ya kupenda kula sana chumvi na hasa kuongeza chumvi ya ziada wakati wa kula chakula mezani. Staili ya maisha unayotakiwa kuifuata ni ile ya kupenda kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuuweka mwili sawa.

Kama una uzito mkubwa, unatakiwa kupunguza uzito na kudumisha uzito unaoendana na umri pamoja na urefu wako. Halikadhalika, kwa wanaokunywa pombe, wanashauriwa kunywa kiasi kidogo na kuacha kuvuta sigara.

Kuwa na tabia ya mara kwa mara ya kucheki afya yako na hasa shinikizo la damu. Shinikizo la damu ni ugonjwa ambao unaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia lishe zaidi kuliko dawa, ingawa kwa wale ambao wameshaathirika kwa kiasi kikubwa, dawa ndiyo kimbilio lao la kwanza.

Mwenye kufuata masharti ya ugonjwa huu, huweza kuishi nao kwa maisha yake yote bila kupata athari zingine hatari, kama vile kupatwa na kiharusi, kuharibika figo au kupatwa na upofu na athari nyingine nyingi.

VYAKULA VYA KUEPUKA
Nyama na mayai ni adui mkubwa wa mgonjwa wa presha. Ni wagonjwa wangapi wanafahamu kwamba vyakula hivi ni hatari kwa maisha yao na wakaacha kabisa kuvitumia? Naamini ni wachache sana wanaolifahamu hili na kulizingatia, hasa ukizingatia utamu wa vyakula hivyo.

Inaelezwa kuwa katika vyakula ambavyo mgonjwa wa presha akivila huchangia kupandisha presha ni mayai na nyama, hasa ile itokanyo na ng’ombe, mbuzi, nguruwe na nyingine za jamii hiyo.
Itaendelea wiki ijayo

Monday, September 13, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Tupac: Dunia kumkumbuka leo, miaka 14 ya kifo chake, hasahauliki, ni nembo ya mapinduzi ya Mwafrika

Tarehe kama leo mwaka 1996, mchawi wa mauzo katika Hip Hop duniani, Tupac Amaru Shakur alifariki dunia baada ya kuishi duniani miaka 25 tu.

Alifariki dunia baada ya kutawala ‘game’ kwa miaka 6 mfululizo lakini kazi yake imeendelea kumuweka chati ya juu mpaka leo. Wachambuzi wengi wanapendekeza Tupac a.k.a Makavelli The Don kuwa Mfalme wa Hip Hop Duniani wa muda wote.

Tupac anapewa cheo hicho kwa kutazama vitu vingi, tungo zake zilivyobamba, mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika Hip Hop, jinsi alivyoweza kubadili vijana wengi Marekani ambao waliishi kwa itikadi zake lakini yote kwa yote, Tupac a.k.a King Killuminat anasimama kuwa mtetezi wa haki za binadamu.

Alikuwa na kipaji kikubwa, aliweza kurap kila kitu alichohitaji, alipoamua kuimba jiwe aliandika mashairi yanayojitosheleza na kukuvutia usikilize. Staili yake ngumu imebaki kumuweka wa kipekee, kwani wengi wamejitahidi kumuiga wameshindwa.

Uwezo wake wa kuandika mashairi siyo tu ulitokana na kipaji, bali pia ulinolewa na shule. King Makaveli baada ya kumaliza Paul Laurence Dunbar High School, alipelekwa na mama yake kwenda kusomea sanaa Baltimore School for the Arts ambako alijifunza kuigiza, kuandika mashairi, staili ya Jazi na kucheza kwa kuigiza bila kutoa sauti (ballet).

Alivyorap kiitikio cha Hit em Up imebaki mtihani hata kwa mastaa wakubwa wa Hip Hip wa sasa, wengi wamejaribu wameshindwa lakini inaaminika Eminem peke yake ndiye anayeweza. Alikuwa mwana Hip Hop aliyefungua njia kwa wengine kwa kukamata namba moja mfululizo kila alipotoa rekodi zake.

Gazeti la Blender lilifanya tathmini na kumtaja Tupac kwamba ndiye mtu anayeheshimiwa zaidi kwenye muziki duniani (Most Overrated Person in Music). Maajabu yake makubwa ni kwamba aliuza nakala nyingi baada ya kufa kuliko akiwa hai, hii imetokana na hazina ya mamia ya nyimbo alizoacha amerekodi studio lakini akafa kabla hajaziachia.

Ameuza zaidi ya nakala milioni 75 duniani na hiyo imemuweka kwenye kundi la wanamuziki bora kwa mauzo duniani. Katika Hip Hop anashikilia nafasi ya pili nyuma ya Eminem, lakini Pac anapewa heshima kwa sababu alifanya muziki kwa muda mfupi mno.

Akina Jigga, P Diddy na wengineo licha ya kuishi muda mrefu kwenye muziki lakini hawajaingia kwenye rekodi ya kuuza. Walikuwepo wakati Pac akitawala soko la Hip Hop enzi za uhai wake na ameendelea kuwapiga bakora sokoni akiwa kaburini.

Sifa kuu ya Tupac ni kwamba hajawahi kuharibu sokoni, albamu zote akiwa hai ziliuza Gold na Platinum. Ni albamu moja tu ya mwaka 2006, iliyotoka miaka 10 baada ya kifo chake “Pac’s Life” ndiyo haikufikia hadhi ya Gold lakini zilizotangulia alifumua Multi-Platinum za kutisha. “Alistahili kila alichopata. Umaarufu na fedha.

Alikuwa milionea akiwa kijana mdogo (miaka 19), alistahili kwa sababu kichwa chake ni madini,” hii ni comment iliyotolewa na mdau wa muziki kusindikiza kifo cha mwanamuziki huyo. Kuna wanaoamini kuwa mapinduzi ya Tupac kwa kumtetea mtu mweusi Marekani hasa kupitia albamu yake ya kwanza ya mwaka 1991 (2Pacalypse Now) yana maana kubwa kuliko hata maajabu ya Barack Obama kuchaguliwa kuwa Rais wa taifa hilo kubwa duniani. Kwamba Tupac alibadili fikra za watu, akawapandisha watu mizuka na kuishi kwa itikadi zake.


SAFARI YA KIFO: Septemba 7, 1996, Tupac alihudhuria onesho la ndondi la Mike Tyson na Bruce Seldon kwenye Ukumbi wa MGM Grand, Las Vegas. Picha za mwisho zinamuonesha akikumbatiana na Tyson baada ya pambano. Baadaye wakiwa MGM, mpambe wa prodyuza wa Pac, Suge Night alimwambia Pac kwamba Orlando Anderson ‘Baby Lane’ alikuwepo ukumbini hapo.

Pac alimshambulia Anderson ambaye alikuwa memba wa Kundi la Southside Crips kwa kushirikiana na Suge pamoja na wapambe wao. Walipotoka hapo walielekea Klabu ya Death Row inayoitwa 662 na alikuwa anaendeshwa na Suge kwenye gari aina ya BMW 75il sedan 1996 (toleo jipya kwa wakati huo).

Walikuwemo pia wapambe kibao. Saa 4:55 usiku gari likiwa limesimama kwenye taa nyekundu za barabarani, Tupac alishusha kioo akapigwa picha na ‘kameramani’ aliyemwomba. Kati ya saa 5:00–5:05 usiku, walikamatwa Las Vegas Blvd na polisi wa pikipiki kwa kuendesha gari wakiwa wameweka sauti kubwa na kutokuwa na leseni ambayo baadaye ilipatikana, hivyo wakaachiwa bila faini yoyote.

Saa 5:10 usiku walisimama kwenye taa nyekundu kwenye Barabara ya Flamingo, Tupac alisimama kupitia rufu ya gari na kuzungumza na warembo wawili kwenye gari nyingine, akawaalika Klabu 662. Saa 5:15 usiku gari toleo la zamani aina ya Cadillac ambalo lilikuwa na namba isiyojulikana, lilishusha kioo usawa wa Tupac na kumshambulia kwa risasi kifuani. Moja ya risasi ilipiga kwenye pafu la kulia la Pac.

Alipelekwa Hospitali ya University Medical Center ambako alifariki siku sita baadaye (Septemba 13) baada ya upasuaji wa kubadilisha pafu lililoharibika kufeli. Miezi sita baadaye, yaani Machi 1997, Biggie naye aliuawa kwa risasi, shambulio ambalo linadaiwa kufanywa na watu wa Pac.


MAJIVU YAKE YAVUTIWA BANGI Tupac alianzisha Kundi la Outlawz Immortalz mwaka 1995 ambalo alilitumia kwenye matamasha yake pamoja na kulishirikisha katika kibao cha kihistoria, Hit em Up.
Mwili wake ulizikwa kwa kuchomwa. Kituko ni kwamba memba wa Outlwaz walichukua sehemu ya majivu yake na kuyachanganya na bangi ambazo walivuta kama kumpa heshima.

HESHIMA Marapa karibu wote wanamtukuza. Herford, Ujerumani kuna mnara wa heshima uliojengwa kwa sanamu la Tupac ili kumuenzi. Marekani pia mnara huo upo na una sanamu lake. Bishop Lamont katika kitabu chake How to Rap, aliandika: “Tupac alikuwa na kila kitu, heshima, matarijio, kipawa cha kurap.

Alikuwa juu mno.” Fedro Starr wa Kundi la Onyx alisema: “Tupac alikuwa masta wa kurap, hakuna wa kumfikia.” 50 Cent: “Kila rapa aliyekua miaka ya tisini ana kitu kuhusu Tupac. Alikuwa na kitu cha kipekee kuliko yeyote kabla yake.” The Game: “Tupac ni rapa bora duniani. Alikuwa na ataendelea kwa maisha yangu yote.” About.com uliandika kuwa Tupac ndiye rapa anayekubalika zaidi.

ALITOKA KIMAPENZI NA MADEMU 10
Warembo ambao Tupac alipokuwa hai alijivinjari nao kwa nyakati tofauti ni Arnelle Simpson, Jada Pinkett Smith, Jasmine Guy, Salli Richardson, Lisa Lopes ‘Left Eye’, Janet Jackson, Rosie Perez, Keisha Morris, Faith Evans (mke wa Biggie) na Kidada Jones ambao jumla yao ni 10.

NUKUU YA PAC
“Siwezi kusema kuwa naweza kuibadilisha dunia, ila nina uhakika kwamba nitapanda mbegu kwenye fikra za watu ambao wataibadilisha dunia.”

NANI ALIMUUA TUPAC?
Ni swali gumu kujibika na maumivu yanayoendelea ni kwamba hakuna hata mtu mmoja aliyeshikiliwa kwa kuhusika. Hata hivyo kuna watu wanabaki kutuhumiwa. Biggie Katika interview ya siku chache kabla Tupac hajauawa alisema kuwa alikuwa anachanganyikiwa na ‘ukigeugeu’ wa Tupac. Alisema:

“Hii inanichanganya kabisa, kwanza anasema, likimtokea lolote anamgeukia Mungu, mambo yakitulia anaongea tena. Inaniudhi, sasa nimeamua mimi na Junior M.A.F.I.A hatutaki tena majadiliano.”

Mbali na kauli hiyo, Biggie anahusishwa kwa sababu kwenye wimbo wake Who Shot Ya? Uliotoka baada ya Tupac kupigwa risasi mwaka 1994, anasikika akiponda kwamba mtu (Tupac) amepewa alichostahili na asicheze na wajanja wa Brooklyn. Wimbo huo ndiyo sababu ya Tupac kurekodi Hit em Up ambapo kiitikio anasema: “Nani alinishuti? Lakini takataka zenu hazikunimaliza.” Anaendelea:

“Nazidi kuwa juu, natengeneza mamilioni ya dola zaidi yenu.” Tupac ameeleza ndani kuwa alitoka kimapenzi na mke wa Biggie, Faith Evans pamoja na malaya wake ambao inadhaniwa anatajwa Lil Kim. Biggie alitajwa kuhusika kwa sababu ya uhasama wao wa muda mrefu, ishu ya mkewe na jinsi alivyoachwa ‘uchi’ kwenye Hit em Up lakini ushahidi haukutosha. Ikaonekana kuwa siku Tupac anapigwa risasi Las Vegas, Biggie alikuwa studio na Jay Z pamoja na kundi la Junior M.A.F.I.A ingawa inasemekana alilipa fedha nyingi kwa kikundi fulani ili kutekeleza mauaji.


Orlando Anderson
Huyu jamaa alipigwa na Tupac kwa kushirikiana na Marion ‘Suge’ Night kwenye Hotel ya MGM, lakini hakwenda kuripoti polisi, kwahiyo ikahisiwa kuwa si ajabu aliamua kulipa kisasi kwa staili hiyo.

Suge Night
Mtendaji Mkuu wa Death Row Records. Aliwekeza kiasi cha dola milioni 14 ili kuhakikisha Tupac anakuwa huru alipokuwa amefungwa gerezani mwaka 1995. Inadhaniwa alipanga njama za kumuua Tupac kwa sababu mwanamuziki huyo ndiye alikuwa anashikilia pumzi ya Death Row. Iliingiza mamilioni ya dola kwa rekodi za Tupac tu!
Kwanini anahisiwa alimuua?

Tupac alikuwa amekwisharekodi mamia ya nyimbo zilikuwepo studio, kwahiyo anadaiwa alimuua ili apate kumiliki utajiri wa nyimbo hizo. Aidha, ikaelezwa kuwa Tupac alikuwa na mpango wa kuanzisha kampuni yake ya muziki baada ya kumaliza mkataba na Death Row wa kurekodi albamu tatu ambao mwanamuziki huyo aliingia na Suge kufidia fedha alizotumia kumchomoa jela. Inaelezwa kwamba Suge alihofia Death Row ingekufa endapo Pac angejitoa.
P Diddy

Anatajwa kupitia mtiririko wa matukio ya kuanzia mwaka 1994. Alitajwa kwa sababu Bad Boy ilikuwa na upinzani na Death Row ambayo ilikuwa juu mno kwa wakati huo, kwahiyo inahisiwa kuwa Diddy aliweka mpango wa kumuua Pac kwa sababu ndiye mtu pekee aliyeipa Death Row jeuri ya kutamba Marekani na dunia nzima katika Hip Hop, kwahiyo aliamini Pac akifa Bad Boy itatawala.

WAZAZI WA BIGGIE & PAC Mwaka 1999 mama wa Tupac na Biggie walitangaza kuwa kitu kimoja kufuatia kumbukumbu ya watoto wao.
****************************************

GENEVIVE MISS TANZANIA 2010
Genevieve Mpangala - Miss Tanzania 2010/11
Pichani chini, akiwa na washindi wa pili na watatu, Glory mwanga (kulia) Concolata Lukos

AY stejini
THT stejini
Waziri wa nihsati na madini, William Ngeleja (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar, William Lukuvi walikuwa miongoni mwa wahudhuriaji

compiled by mc george/wikienda