Sunday, August 12, 2007

NGONO KWENDA MBELE!!


RICHARD BUKOS NA CHRISTOPHER LISSA
kamera ya Ijumaa Wikienda ikiwa kazini, wikiendi iliyopita iliwanasa njemba moja na mrembo aliyefahamika kwa jina la Prisca Michael wakifanya vitendo vya ngono uchochoroni.

Fumanizi hilo lilitokea usiku wa manane wa kuamkia Jumamosi, katika moja ya vichochoro vilivyopo karibu na Klabu ya High Way Night Park ‘Kwa Macheni’, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Timu ya Wikienda ambayo ilikuwepo maeneo hayo, ikikusanya matukio yanayojiri usiku huo ili kuijuza jamii, ilifuatilia kwa karibu ‘mkandamizo’ huo bila kupoteza pointi hata moja.

Kabla ya fumanizi, aliyekuwa wa kwanza kuonwa na waandishi wetu ni Prisca ambaye alikuwa akizunguka zunguka katika maeneo jirani na klabu hiyo kana kwamba alikuwa akitafuta kitu.

Majira ya saa saba na dakika kadhaa za usiku, ilitokea njemba hiyo ambayo haikufahamika jina mara moja na kuanza kuongea na Prisca, maongezi ambayo timu yetu haikufanikiwa kuyanasa.

Hata hivyo, maongezi kati ya wawili hao hayakuchukua muda mrefu, kwani kitambo kidogo, walishuhudiwa wakiongozana kuelekea gizani. Timu yetu, baada ya kuvutiwa na mkanda huo, ilijigawa na kuanza kufuatilia nyendo za Prisca na mwenzake ili kujua mwisho wao.

Aidha, waandishi wetu wakiwa wameandaa kamera tayari kwa kazi mbele yao, waliweza kuwaona wawili hao wakiwa wamejibanza uchochoroni huku wamekumbatiana. Bila kufanya ajizi, kamera yetu ikiwa mbali kidogo kutoka walipokuwa Prisca na mwenzake, ilifanikiwa kupata picha nne zilizopigwa bila kushtukiwa.

Baada ya kukamilisha zoezi la upigaji picha, timu ya gazeti hili iliwasogelea wawili hao kwa lengo la kuwauliza sababu ya kufanya vitendo hivyo uchochoroni, lakini njemba hiyo ilitimua mbio baada ya kujua kwamba watu waliokuwa mbele yake ni waandishi wa habari.

Hata hivyo, ilifanikiwa kumpata Prisca ambaye kabla ya yote alianza kulaumu kwa kukimbiziwa mteja wake. “Nyie wadaku vipi? Mbona mnaingilia anga za watu? Mnaona mpaka mteja wangu amekimbia, bahati yenu ameshanipa changu, vinginevyo tungekabana mashati,” alifoka Prisca.
Mrembo huyo ambaye alikuwa amekolea kilevi aliongeza: “Msione watu wanapeana raha, nyie mnawashwa, haya semeni kama mnataka ‘mchezo’ niwasaidie.”

Alipoulizwa kwa nini alikuwa akifanya mapenzi uchochoroni, mrembo huyo alijibu kwamba hakuna mtu anayeweza kumpangia. “Mapenzi popote, kama aibu mnazo nyie, mimi naangalia biashara, nakubaliana na mtu wangu, tunazama sehemu yoyote anayotaka, kama hana hela ya gesti je, nyie vipi?” Alihoji mrembo huyo.

Hata hivyo, baada ya kutuliza munkari, mrembo huyo alisema, hafanyi biashara ya kuuza mwili kwa shida kwa sababu anatoka kwenye familia inayojiweza kifedha. Alisema, anafanya ukahaba kama ‘hobi’ na kuongeza kuwa wazazi wake wameshajitahidi kumfanya aache lakini imeshindikana.

“Nyumbani kwetu ni Kimara, mimi naitwa Prisca Michael, baba yangu ni mtu mwenye uwezo tu, kwahiyo msinione hapa mkadhani labda shida ndiyo zimenifanya niwe changudoa,” aliongeza mrembo. Baadaye, waandishi wetu walimpiga picha mrembo huyo akiwa amepozi, baada kuomba afanyiwe hivyo kwakuwa endapo ataonekana gazetini, basi wateja wataongezeka.

Huu ni uchafu ambao haupaswi kufumbiwa macho, Ukimwi unazidi kushika kasi, lakini miongoni mwa tabia hatarishi za ugonjwa huo ni biashara ya ngono. Jamii bado inahitaji kuelimishwa zaidi ili yapatikane mapinduzi ya fikra, vitendo vinavyofanyika usiku vinatisha, hatuwezi kuzuia Ukimwi kama tunafumbia macho uchafu utokeao usiku. Mhariri



Mariam Mashauri aeleza yaliyomkuta gerezani

Wanza Temu na Imelda Mtema

Aliyekuwa Mshiriki wa Shindano la Muziki la Bongo Star Search (BSS) mwaka 2006-07, Mariam Mashauri, ameeleza yaliyomkuta gerezani sambamba na kusimulia picha halisi ya maisha ya mfungwa wa kike.

Kwa mujibu wa mahojiano kati ya waandishi wetu na mwanamuziki huyo, Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam, Mariam pia alimshukuru Mungu kwa kuachiwa huru ikiwa ni miezi mitatu tangu alipohukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Mariam ambaye alikuwa katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, aliongea mambo kadhaa kuhusiana na maisha ya ufungwa, katika mahojiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni B, ikiwa ni saa kadhaa baada ya kuachiwa huru.

Mahojiano hayo yalikuwa kama ifuatavyo;
Wikienda: Habari yako Dada Mariamu na hongera kwa kuachiwa huru.
Mariamu: Ahsante sana, namshukuru Mungu yeye ndiye muweza wa yote.

Wikenda: Sisi ni waandishi wa habari kutoka Gazeti la Ijumaa Wikienda, kwanza tunakupa pole kwa matatizo yaliyokupata, lakini ni vizuri kama utatueleza unajisikiaje kuwa huru na imekuwaje leo umeachiwa?

Mariamu: Ahsanteni, nimeachiwa kwa sababu baada ya kuhukumiwa, nilikata rufaa kwa sababu sikutendewa haki kwenye hukumu ya kwanza, kwahiyo nimeshinda, mimi ni Mtanzania na cheti cha kuachiwa hiki hapa (anawaonesha waandishi).

Wikienda: Unadhani nini chanzo cha kuenea habari kwamba wewe siyo Mtanzania na kusababisha ukafungwa?

Mariamu: Watu siyo wazuri, wapo wasiopenda maendeleo yangu, wanasema lafudhi yangu, lakini hiyo ni kuongea tu wala haina maana kuwa mimi ni mgeni wa nchi hii, chanzo cha hayo yote ni rafiki yangu mmoja, yeye ndiye aliyenichongea hadi nikapata matatizo yote, ukweli ni kwamba mimi ni Mtanzania, baba yangu ni Msambaa wa Tanga ila mama ni Mzambia.

Wikienda: Kwa maana hiyo unamjua adui yako, sasa unatarajia kuchukua hatua gani dhidi yake?

Mariamu: Nimeshamsamehe, sitochukua hatua yoyote, haki ipo mbele ya Mungu peke yake.

Wikienda: Zipo taarifa ambazo zimezagaa kila kona kuhusu jela kwamba kuna vitendo viovu, ushoga kwa wanaume, usagaji kwa wanawake, uvutaji wa bangi na wafungwa wa kike kulazimishwa ngono na askari magereza wa kiume, je, wewe yalikukuta hayo?

Mariamu: Namshukuru Mungu sana, mimi sikuwahi kukutana na vitendo hivyo, huwa nasikia hata nilipokuwepo gerezani nilisikia watu wakisema mambo hayo, lakini haikutokea kwangu, Mungu ni mkubwa, alinikinga kwa yote.

Naweza kusema jela imenisaidia kwa kiasi fulani, imenifunza mambo mengi, kule kulikuwa na ngoma ya gereza, kwahiyo nilikuwa nacheza sana, pia nimejifunza kushona masweta na mambo mengine.

Wikienda: Kuna vitu gani ambavyo vilikuwa vikikukwaza katika kipindi chote cha miezi mitatu uliyokuwepo gerezani?

Mariamu: Washiriki wenzangu katika Shindano la Bongo Star Search hawakuja kuniona hata siku moja, kwa kweli ilinisikitisha sana kuona hata majaji wetu hawakunijali angalau kuja kunipiga jicho hata mara moja, hata hivyo, sina kinyongo, nimewasamehe wote.

Wikienda: Ukiambiwa utaje vitu ambavyo utavikumbuka sana gerezani, utaorodhesha nini na nini?

Mariamu: Mimi nilikuwa nikitunga nyimbo na kuimba, mpaka sasa nina albamu yangu ambayo imekamilika kwa nyimbo tano, pia wafungwa wenzangu, niliwazoea sana, mimi nilikuwa mpole kwahiyo nilielewana na kila mtu, wakawa wakarimu kwangu, niliwafundisha kumjua Mungu na kutubu dhambi na leo nilipowaaga, wengi wamelia machozi.

Wikienda: Vipi 'msosi' wa gerezani, ulikuwa unapanda au ulikuwa ni adhabu kwako?

Mariamu: Nilikuwa nakula chakula bila kudengua, nilijua kila kitu ni mapito tu.

Wikienda: Tunafurahi upo huru tena, tunakupongeza, lakini tunataraji kukuona ukiwasha moto mkali kwenye fani yako ya muziki.

Mariamu: Ahsante, kazi ipo.

WADAU WA UREMBO BONGO: MNAMKUMBUKA MREMBO HUYU?


Leo Abby Cool & MC Geroge Over The Weekend imeamua kukufanyia bonge la surprise, imetega na mitego imemnasa na kumuibua Miss Tanzania namba 2 mwaka 1999 - 2000, Ayan Hassan(pichani juu) kisha kupiga naye stori.

Akiongea kupitia mtandao wa internet, mnyange Ayan alisema kwamba, muda mrefu aliotoweka nchini yupo kwenye ardhi ya Malkia Elizabeth, UK, akilisongesha gurudumu la maisha na amekuwepo nchini humo kwa miaka mitano sasa.

Aidha mlimbwende huyo aliyepata kutingisha kunako sanaa ya urembo alisema kuwa, akiwa nchini humo tayari ameshamaliza masomo yake ngazi ya diploma, yaliyomgharimu miaka mitatu katika chuo cha Hammersmith and West London cha London, England na sasa hivi anajipanga kwenda kutembea USA.

Pia nina mpango wa kurudi nyumbani na ninamatumaini ya kufungua biashara yangu mwenyewe, japo sijaamua nifanye bishara ya aina gani. Kuhusu masuala ya urembo kwasasa nimeyaweka kando, sina mpango wa kuendelea na mambo ya urembo kwa sasa, labda baadaye.

"Ningependa kuwashauri washiriki wa urembo wajitahidi kujihadhari na gonjwa la ukimwi. Ningewaomba kwakuwa wao ni jicho la umma wawe mstari wa mbele katika kuielimisha jamii kuhusu HIV hasa vijana."Rais Kikwete (Jakaya) kashatoa mfano naomba tumuunge mkono", alisema Ayan Hassan.

USIKU WA TWANGA, JAMAA ZIII!

Iron Lady.. mamaa Asha Baraka akifuatilia vijana wake wa African Stars huku akiteta na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mh. Juma Kapuya..!
Jamaa ziii'''ndani ya Mango Garden, usiku wa Twanga Pepeta...ina kuwaje!

AROBAINI YA AMINA, VILIO VYAIBUKA UPYA!

Marehemu Amina Chifupa, kipenzi cha wengi, jana alitimiza siku arobaini tangu aiage dunia na katika kisomo cha arobaini hiyo kilichofanyika nyumbani kwa mzee Chifupa Mikocheni vilio viliibuka tena wakati ndugu na jamaa walipokutana tena. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi, DAIMA ATAKUMBUKWA!
Mama mzazi wa Amina akiwa katika majonzi mengine ya kumkubuka kipenzi chake wakati wa Arobaini ya mwanae jana jijini Dar es salaam.
Familia ya Mpakanjia, kati ni mama mzazi wa Meddy, mtoto anayeiangalia kamera ndiye Rahman mtoto wa marehemu Amina. Meddy mwenyewe hakuhudhuria arobaini hiyo na kuna habari zinasema 'yu mgonnjwa'.
Mzee Chifupa (kushoto) akiwa na kaka yake pamoja na 'daruwesh' maarufu jijini Dar (kulia) kwenye Arobaini ya marehemu Amina

Saturday, August 11, 2007

VITUKO VYA 'GOAT RACE'

Mbuzi wa kijana Hassan Mpole ndiye aliyeibuka mshindi katika mashindano ya mbio za Mbuzi yaliyofanyika Leaders Club jijini Dar es slaam Jumamos mchana. Mbuzi nambari nne mgongoni aliibuka na kitita cha 1.2m za bongo!
Mshike mshike wa mbio za mbuzi, Leaders Club Jumamosi mchana
Hawa ni 'minjemba', usidhani ni akina aunt, kundi lao linajiita AYAM GOAT RACING na ndio wenye mashindano haya bongo

Taarifa maalum kwa Chahali, gazeti la Kulikoni

Kampuni ya Global Publishers & General Entreprises wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi, imesikitishwa sana na makala iliyoandikwa katika Gazeti la Kulikoni linalotolewa na Kampuni ya Media Solutions Ltd ya jijini Dar es Salaam.

Makala hayo yaliyochapishwa katika toleo lake la Jumatano ya Agosti 8, mwaka huu, yaliyokuwa na kichwa cha habari ‘Magazeti ya Udaku yanaandika habari feki’, iliushutumu uongozi wa gazeti hili kuwa waliandika habari ya uongo katika toleo lake la Julai-20, mwaka huu.

Habari ambayo mwandishi huyo alidai kuwa ni ya uongo ilikuwa na kichwa kisemacho, ‘Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu’.

Pamoja na shutuma hizo, Kulikoni pia kupitia kwa mwandishi wake anayejiita Evarist Chahali, mwanafunzi Mtanzania anayesoma katika Chuo cha Aberdeen, nchini Scotland, lilidai kuwa, mhariri alitumia picha za wasichana watatu ambao alielezwa na rafiki yake kuwa ni wacheza filamu za ngono (Porn stars) nchini Marekani na si Watanzania wanaojiuza kama gazeti hili lilivyoandika.

Kupitia makala yake, mwandishi huyo amediriki pia kulishambulia gazeti hili waziwazi akidai kuwa yeye binafsi linamkera sana kwani linaandika habari za kuzusha.

Maelezo aliyoandika mwandishi huyo kwa kweli yanatufanya tuamini kuwa, digrii alizonazo zina mashaka kutokana na kushindwa kwake kufanyia uchunguzi wa kutosha kabla ya kufikia hatua ya kutoa shutuma kama hizo zenye lengo la kuchafuliana.

Kwa ujumla, tungependa kusisitiza kuwa habari iliyoandikwa kwenye gazeti hili ni ya kweli na kwamba wasichana waliochapishwa wametambulishwa katika mtandao huo kuwa ni watanzania wanaojiuza kwa njia ya kupiga picha chafu na si Wamarekani kama alivyodai Chahali.

Tunaamini kuwa Chahali ni msomi, hata kama si katika nyanja ya uandishi, hivyo hakupaswa kuandika shutuma zile baada ya kumnukuu mtu kwa maneno ambayo hakuyafanyia uchunguzi, kwani hatua hiyo inaweza kumfanya ashindwe kuthibitisha mbele ya sheria.

Kimsingi picha za wasichana waliochapishwa kwenye gazeti hilo ni Watanzania kama walivyojieleza wenyewe kupitia tovuti ambayo tumelazimika kuiweka wazi mwisho wa taarifa hii, ili kuuthibitishia umma kuwa hatuandiki, hatujaandika na wala hatutaandika habari ‘feki’.

Chahali anapaswa kuelewa kwamba habari tuliyoiandika haikuwa jambo geni sana ambalo haliwezi kufanywa na Watanzania wa leo, hayo mambo yapo, tena mengine ni mazito zaidi na hayaandikiki kwenye gazeti.

Aidha, asifikiri wasomaji wetu ni wajinga ambao wanaweza kudanganywa kirahisi kwa kuwaandikia habari za uongo. Hayo ni mambo ya kawaida katika jamii yetu hivi sasa, lakini Chahali anaonekana kuwa ni mgeni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa kufikiri kwamba kitu kama hicho kinafanywa na Wamarekani pekee.

Tunapenda kumfahamisha Chahali kuwa sisi hatuna haja ya kutunga habari ‘sensational’ wakati hizo zipo nyingi katika jamii tunayoishi na kama yeye hazijui haina maana kuwa hazipo. Hivi inawezekana kweli yeye tu ndiye awe ameiona habari ile ni ya uongo miongoni mwa mamilioni ya Watanzania wa ndani na nje ya nchi walioisoma?

Tunawaheshimu sana wasomaji wetu na wao ndio vyanzo vyetu vikuu vya habari tunazoziandika. Chahali anapaswa kuelewa kwamba tunachokiandika, siku zote huwa kinatoka kwa wasomaji hao na ndio maana wamekuwa wakituamini kwa miaka karibu kumi sasa.

Kwa kumrahisishia kazi Chahali na kumjuza kuwa hatuna sababu ya ‘kutunga’ habari ili tupate pesa, atembelee tovuti hii: http://swallowmyjuice.hi5.com ili akajionee mwenyewe wasichana hao anaodai ni Wamarekani, ili siku nyingine aache kuropoka na kuingilia mambo ya watu asiyoyajua.

Hatukatai kila mtu ana uhuru wa kutoa mawazo yake ilimradi havunji sheria, lakini si vizuri kutoa shutuma nzito dhidi ya mtu mwingine kwa chuki binafsi na ‘roho ya kwa nini’, kama vile ambavyo Chahali mwenyewe amesema katika makala yake, eti ‘mmeshatengeneza faida ya kutosha’!

Kimsingi magazeti ya Udaku yanafanya kazi sambamba na vyombo vingine katika kupasha habari, kuelimisha na kuburudisha jamii na kwamba hayapo Tanzania tu bali hata katika nchi nyingine kama Uganda, Marekani, Uingereza na kwingineko na yanapendwa kama yanavyopendwa ya hapa nchini.

Mwisho, kwa taarifa hii tunawaomba wahariri wa Kulikoni, ambao tunawaheshimu sana, kuwa makini na waandishi wanaotaka kutumia gazeti hilo kwa manufaa yao binafsi kwa lengo la kuchafuliana na kushushiana hadhi mbele ya jamii.

Imetolewa na kusainiwa na:
Abdallah Mrisho
Meneja Mkuu
Global Publishers & General Enterprises Ltd

CHAHALI, VYA KUMUNG’UNYA UNATAFUNA, INAKUWAJE?

Na Tulizo Kilaga
(MAKALA MAALUM KWENYE GAZETI LA RISASI -AGOSTI 11,2007)

JUMATANO ya wiki hii, yaani Agosti 8, 2007 nilisoma, nikashtuka, nikapata uchungu kutokana na makala iliyoandikwa na Evarist Chahali, iliyokuwa na kichwa cha habari ‘Magazeti ya Udaku yanaandika habari feki’. Nililazimika kusoma makala hayo zaidi ya mara tano na kila nilipofika kwenye neno “ shame on you!” niligadhabika na kutafuta nguvu ya kujenga hoja, hatimaye nikajiridhisha na sasa naomba niweka sawa haya yafuatayo.

Evarist Chahali amedhihirisha wazi kuwa ana uelewa mdogo katika uandishi, anadhani kujua kusoma na kuandika pekee kunatosha mtu kuwa mwandishi, najua wapo wengi wasioamini kuwa uandishi ni taaluma kama huyu mkurupukaji Chahali, hivyo nataka niwathibitishie kuwa uandishi ni taaluma.

Binafsi nimefadhaishwa sana na maneno nitakayoyanukuu hapa chini kutoka kwenye makala yake “Hivi ni uzembe wa mhariri kucheki ukweli wa habari husika au ndiyo kuwafanya watanzania wajinga kwa kuwapa habari “sensational” ambazo hazina ukweli? Nyie ni watu wazima ambao mmeshatengeneza faida ya kutosha kwa kuandika udaku lukuki wa kweli, sasa tamaa ya nini hadi mfikie hatua ya kunyofoa mapicha kwenye mtandao na kuzusha habari? Shame on you!”

Mwandishi huyo amesahau kuwa Risasi ni gazeti lenye jukumu kubwa la kuhakikisha linaipa jamii habari iliyo sahihi na ya kuaminika.

Nikiwa kama mhariri msaidizi wa gazeti hili, nasema Chahali ni muongo! Amenisikitisha kwani mtu mzima kuanza kuzusha na kusema uongo kwa faida ya vitu vidogo vidogo vyenye shibe ya kitambo, ni mambo ya kuhuzunisha na kujidhalilisha.

Mimi nasema kuwa, Chahali kwa elimu yake kubwa, alipaswa kujua kuwa katika kutoa hoja mtu anatakiwa kufuata taratibu za fikra sahihi na si vionjo kama alivyofanya!

Nakumbuka vema katika miaka mitatu niliyokesha kutafuta Shahada yangu ya kwanza katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Tumaini- Iringa Mkufunzi wangu wa Physchologia Marehemu Prof. Samuel Mshana (Mungu amlaze mahala pema peponi) alipenda kunisisitizia maneno ya mwanafalsafa Plato kuwa ulimwengu umegawanyika katika makundi mawili, yaani ulimwengu wa busara na akili na ulimwengu wa muonekano/maoni.

Kimsingi Plato anamaanisha kuwa wale wenye busara na fikra sahihi wapo kwenye ulimwengu wa ukweli na wale wenye vionjo kama Chahali wapo kwenye ulimwengu wa maoni!

Chahali ni mchangiaji wa habari katika gazeti la Kulikoni anayeishi Scotland, nchini Uingereza ambako anasomea Udaktari wa Falsafa katika Siasa za Kimataifa, hususan kuhusu Afrika na anafanya utafiti kuhusu Uislam na harakati za vikundi vya Kiislam nchini Tanzania.

Huyu ni msomi kwani alipata Shahada ya Kwanza katika Elimu ya Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ‘Mlimani’ kabla ya Kupata Shahada ya Uzamili katika Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kisha kufuatiwa na Shahada ya Uzamili wa Utafiti (Master of Research-MRes) katika Utafiti wa Siasa (Political Research) huko aliko sasa.

Hakika Chahali ni msomi lakini kuna maswali mengi najiuliza, hivi huyu ni msomi wa aina gani, anayethubutu kuandika makala bila kuifanyia uchunguzi? Mbaya zaidi ndugu yangu ana taaluma ya Shahada ya Uzamili wa Utafiti, lakini hataki kwa makusudi kuitumia! Msomi wa namna hii ni sawa na mwandishi asiyeweza kuona mwanga gizani.

Nakumbuka siku namaliza shahada yangu ya uandishi wa habari, mkufunzi wangu aliyekuwa akinifundisha ‘teaching methodology’ Fredy Nyamubi aliniambia kuwa, ili ujue elimu uliyonayo inakusaidia ama umeelimika lazima uweze kutumia taaluma ulionayo katika maisha yanayokuzunguka. Hivyo, kila ninapotaka kufanya kazi zangu huyakumbuka maneno haya.

Chahali anapaswa kujua kuwa, zipo kanuni zinazomuongoza mwandishi yeyote kuweza kupata habari iliyo sahihi, hivyo ukitumia vema kanuni hizo pamoja na mambo kadhaa ya msingi yanayoifanya habari kuwa habari, basi habari itakayoandikwa huwa sahihi.

Tasnia ya habari duniani kote huzingatia kanuni nne ambazo ni ukweli, utii, uthibitisho na kuwa na imani na unachokiandika, hivyo Chahali lazima azingatie kanuni hizi, lakini kwa kuwa watanzania hawana utamaduni wa kujisomea wanaweza kupata Gazeti la Rai la Alhamisi ya Juni 28 – Julai 4, 2007 Uk. 9 ambapo kuna makala iliyoandikwa na mkongwe wa habari, Muhingo Rweyemamu.

Katika makala hiyo Rweyemamu anasema “Uandishi wa habari una tofauti na uandishi wa barua au malalamiko. Anayelalamika hata kama analalamika kwa rais, hana sababu ya kumpa nafasi anayemlalamikia vivyo hivyo kwa mwandishi wa barua.”

Nirudi kwa Chahali, hivi ni kweli hajui kuwa nidhamu ya msingi ya mwandishi wa habari duniani kote ni ile inayompa nafasi mtuhumiwa? Sitaki kuamini kuwa nawe ni miongoni mwa watu wanaoamini nidhamu hii huitajika kwenye habari kubwa ya kuuzia gazeti tu! Hata makala hutakiwa kuzingatia hili kwani nayo ni habari.

Hainiingii akilini, kwanini Chahali hakutaka kutoa nafasi kwa wahariri wa gazeti hili ili kujua ukweli wa habari iliyochapishwa katika toleo na. 400 la Julai 18-20 yenye kichwa cha habari “ Warembo TZ wapiga picha za x tupu? Anadai kinachomsikitisha siyo kama habari hiyo ni ya kweli au ya kubuni bali ni picha zilizotumika.

Chahali anaamini kuwa anajua kila kitu! Jambo ambalo siyo kweli na haliwezekani.

Hata hivyo, nataka nimfahamishe kuwa habari inayoandikwa na mwandishi anayejifanya kuwa na taaluma zote kichwani ina madhara makubwa kwa jamii kwa sababu huweza kumuumiza mtu ama kumsababishia kifo.

Hivi Chahali alitaka tuambatanishe na mtandao wanaopatikana warembo hao ili athibitishe kuwa ni watanzania? Haoni kuwa kwa kufanya hivyo ni ‘kuwapromoti’ mabinti hao? Kama kulikuwa na ulazima kwanini yeye hakuweka bayana mtandao aliodai kuwa alitumiwa na rafiki yake uliokuwa ukikanusha habari yetu?

Nawaheshimu sana watanzania na siwezi kamwe kuwafanya wajinga kwa kuwapa habari “sensational” ambazo hazina ukweli! Nataka kuwathibitishia watanzania wote kuwa RISASI ni gazeti linalozingatia kanuni na maadili ya uandishi wa habari.

Baada ya kusema hayo, naomba niweke wazi ‘link’ za mtandao ambao kila mwenye nafasi aweze kuupitia ili kuona nani ni muongo kati ya Chahali na Gazeti la Risasi. Mtandao huo ni http://swallowmyjuice.hi5.com ambapo wote wanadai ni wakazi wa Dar es Salaam, Tanzania sasa Risasi limedanganya nini?

Kimsingi simkatazi Chahali siku nyingine kuandika maoni yake, kwani maoni ni miongoni mwa njia za kupata ukweli, lakini mara unapoupata unapaswa kuhakikisha unaufuata!

Kama Chahali alikuwa hajui basi nichukue nafasi hii kumfahamisha kwa ufupi kuwa, kuna baadhi ya mambo ambayo hufanya habari kuwa habari ‘elements that make news to be newsworthiness’ ambazo ni kama zifuatazo.

Kwanza kabisa kuna (proximity) ukaribu wa habari husika na jamii lengwa, (prominence) inamhusu mtu gani maarufu, (impact) madhara ama umuhimu wake kwa jamii, (conflict) mkingamo wa mawazo, (timeliness) limetokea lini, (novelity) je tukio hilo ni la kawaida ama si la kawaida na (human interest) uvutaji wa hisia za watu.

Kutokana na sifa hizo ni ukweli ulio wazi kuwa wahariri wa gazeti la RISASI tulikuwa na kila sababu ya kutoa habari ile kwani tukio lenyewe si la kawaida katika jamii yetu labda Chahali anaona ni jambo lisilowezekana kutokea nchini kwetu na kusahau kuwa tukio hilo ni moja ya athari za utandawazi.

Sitaki kutumia muda mwingi kuelezea sifa zote zilizosababisha kuchapisha habari hiyo ila kimsingi Chahali ni miongoni mwa watu wanaosemwa na mwanafalsafa wa siku nyingi, Permanides kuwa kuna watu wanachanganya kati ya ukweli kadiri unavyojitokeza kwao na ukweli halisi na kusisitiza kuwa ni vizuri kuangalia kitu kama kilivyo na si vinginevyo.

Tanzania ni nchi yetu na tuna jukumu kubwa sana mbele yetu katika dunia hii tuliyopo ya ‘information age’ ambalo ni kuhakikisha tunaandika habari za uhakika ili kuiwezesha jamii yetu kupata maisha bora! Sasa kaka Chahali, vya mung’unya, unatafuna, inakuwaje?

Kuna kila sababu ya uongozi wa gazeti hili kuamini kuwa Chahali aliamua kutuchafua ili aweze kupata umaarufu kwani alijua kuwa akifanya hivyo ataandikwa sana na magazeti hivyo, kuanzia hapo atajulikana kwani tangu mwaka 2006 hadi sasa ana watu 2000 tu waliotembelea blog yake, wakati watanzania wengine hupata watu zaidi ya 500 kwa siku.

Mwandishi wa makala haya anapatikana kwa namba +255 0715 888887. mwakilaga.blogspot.com

DENTI AFUMWA 'AKIKANDAMIZWA KIBARA' USIKU WA MNANE


Catherine Kassally na Mariam Mndeme waliokuwa Morogoro

Mwanafunzi wa darasa la tano wa shule moja ya Msingi, mkoani
Morogoro aliyefahamika kwa jina moja la Emmy, amefumwa akiwa na

jamaa mmoja ‘mtu mzima’ wakiponda raha na mambo mengine machafu.
Denti huyo alifumwa na waandishi wetu, saa nane usiku, Jumatano
wiki hii kwenye sherehe za wakulima Nane Nane, katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere, mjini Morogoro.

Denti huyo akiwa anaonekana ‘kuunyaka mtindi’ alikuwa
amekubatiwa na jamaa huyo ambaye jina lake halikuweza
kupatikana mara moja mbele ya kadamnasi ya watu katika grosari
moja iliyomo uwanjani humo.

Binti huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 na 14,
ambaye haikufahamika shule aliyokuwa akisoma, alikuwa amepakatwa
na jamaa huyo huku wakibusiana.

Waandishi wetu pamoja na baadhi ya watu waliokwenda katika
viwanja hivyo, waliwashuhudia binti huyo na jamaa yake
anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35-40 jambo
lililowafanya wawashangae na kulaani kitendo hicho kichafu.

Hata hivyo, baada ya vitendo hivyo kuendelea kukithiri baadhi ya
watu waliokuwepo katika eneo hilo walianza kuwakemea kwa
kuwataka waondoke, vinginevyo wangewaitia polisi.

Licha ya tishio hilo, wawili hao waliendelea kufanya uchafu wao
huku wakidai kuwa wasingewafanya chochote kwani walikuwa katika
raha zao.

Hata hivyo, jamaa aliyekuwa na denti huyo naye alianza kufoka
akidai kuwa wanawaonea kwavile ni waswahili kwani wangekuwa
wazungu wagewaacha.

‘’Hata kama mtawaita polisi, hawawezi kutufanya kitu kwani nyie
ndio mnaotutazama, kama mnaona noma basi msituangalie,
wangefanya wazungu mngesemasema maneno hayo?,” Alihoji jamaa
huyo.

Aidha, watu hao walishangaa wakidai kuwa jamaa huyo ni kubwa
kiumri hivyo alikuwa akimuonea kwa kumrubuni binti huyo
kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza binti naye alianza kutoa

maneno ya kuwashambulia watu hao na kudai kuwa wawaache kwani
jamaa aliyekuwa naye anammudu licha ya kuonekana mkubwa kuliko
yeye.

“Mwacheni mpenzi wangu mwenyewe ninammudu na wala si mkubwa
kwangu mimi namuona kama mtoto mwenzangu,” alisema denti huyo.
Baada ya kuona wapenzi hao wanaendelea kufanya uchafu huo,
waandishi wetu walipowapiga picha ambapo awali waliduwaa lakini
baadaye walishtuka na kuacha.

Waandishi wetu pamoja na watu wengine waliokuwepo hapo
walipowasogelea, jamaa alinyanyuka na kumwacha binti huyo
ambaye aliomba msamaha baada ya kuambiwa kuwa picha yake
ingechapishwa kwenye gazeti.

“Mnisamehe dada zangu, haya ni maisha yangu na ni siri yangu,
shuleni kwangu hawajui, wala nyumbani kwetu hawafahamu sasa
mkitoa picha hiyo nitapigwa hadi kuuawa, niko tayari kuwapeni
hata fedha” alisema msichana huyo huku akimwaga chozi.
Msichana huyo aliondoka baada ya kuona kuwa ombi lake
halisikilizwi na wanahabari hao.

Tumelazimika kuziba sura ya binti huyo kutokana na sababu za
kimaadili - Mhariri.

Friday, August 10, 2007

THOMAS MLAMBO WA SUPER SPORT ATUA BONGO!

Jamaa ni miongoni mwa watu wanao 'uza sura' sana barani Afrika na baadhi ya nchi za Ulaya,hasa kwa wale wapenzi wa michezo na watazamaji wa chaneli pekee ya mpira barani afrika 'SUPER SPORT', huyu si mwingine bali ni THOMAS MLAMBO! Katua Bongo kwa ziara fupi ya kikazi,hapa akifanya press conference katika hoteli ya Holiday, jijini Dar,Ijumaa mchana.
Thomas Mlambo akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano namedia. Uwanja Mpya utakapoanza kutumika, jamaa wa Super Sport watakuwa wakirusha mpira LIVE!

Lucy Kiwhele (kushoto) naFuraha Samalu, viunganishi vikubwa vya media na MultiChoice Tanzania


Angela Msangi (kushoto) mwandishi wa TVT akihojiana na Meneja Uhusiano wa MultiChoice TZ, Lucy Kiwhele, katika Hoteli ya Holiday Inn, mapema Ijumaa



Mazagazaga ya kula ya Holiday Inn




Mhariri wa gazeti la michezo, Sport Starehe, Masoud Sanani (kushoto) akipozi Thom





Thomas Mlambo (kulia)akiwana 'mdau' wa blog hii,Mrisho

Thursday, August 9, 2007

The Sexiest Girl yawa gumzo!


NA JOSEPH SHALUWA
Shindano la kumsaka msichana mwenye mvuto zaidi wa kimahaba linaloendeshwa na gazeti la Ijumaa (The Ijumaa Sexiest Girl), limekuwa gumzo miongoni mwa wasomaji wetu.

Hilo limedhirika baada ya wasomaji wengi kutupigia simu wakionyesha kimuhemuhe cha kufuatilia shindano hilo, hata hivyo wengi wameshindwa kutabiri mshindi kutokana na washiriki wote kuwa na mvuto wa kimahaba.

"Yaani washiriki wote ni bomba sijui ni nani ataibuka mshindi, yaani hapo sina la kusema, nitafuatilia mpaka mwisho hadi nijue ni nani ataibuka kidedea maana wote ni wakali," alisema Bahati Mlawa mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam.

Naye Benedict Joseph wa Moshi mkoani Kilimanjaro, alidai kuwa mshindi wa mwaka jana Jacqueline Ntuyabaliwe 'K-Lyn alikuwa na vigezo vyote vya kuwa mshindi ila mpambano wa mwaka huu hautabiriki.

"K-Lyn yupo bomba sana kwakweli, ilikuwa rahisi sana mwaka jana kutabiri kuwa angekuwa mshindi lakini mwaka huu ni vigumu sana kutabiri mshindi,” alisema.

Katika kuonyesha kuwa wasomaji wetu wanafuatilia shindalo hilo kwa makini na kuonyesha upenzi kwa wale wanaodhani wana mvuto zaidi wa kimahaba, shabiki mmoja alisema kuwa atakuwa tayari
kupiga kura nyingi awezavyo kwa yule anayeamini anavutia zaidi.

“Ni kweli mpambano wa mwaka huu ni mkali sana, lakini pamoja na hayo kwenye mashindano lazima kuwe na mshindi!

“Yupo mrembo mmoja kati yao ambaye nahisi anaweza kuibuka kinara, siwezi kumtaja jina ni siri yangu, nitakuwa nikimpigia kura nyingi kadri niwezavyo," alisema.

Shindano la 'Ijumaa Sexiest Girl' lilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka jana, ambapo Miss Tanzania mwaka 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe aliibuka kidedea.

Mrembo auawa!


NA DOTTO MWAIBALE
Mhudumu wa Baa ya Salama Beach iliyopo Kiwalani Bombom jijini Dar es Salaam, Lightness Johnson (17), amefariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingoni na kijana mmoja aitwaye Good luck Saria nayedaiwa kuwa mpenzi wake kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mrembo huyo amekumbwa na mauti usiku wa kuamkia Agosti 7, mwaka huu majira ya saa 5.00 za usiku, wakati wateja wakiendelea kupata vinywaji katika baa hiyo.

Akiongea na Mwandishi Wetu mhudumu mmoja wa baa hiyo aliyeshuhudia tukio hilo aitwaye Amina Mbaraka alisema kuwa, siku hiyo akiwa na marehemu walifika kazini majira ya jioni.
Amina alisema walipowasili walianza kuwahudumia wateja wao huku wakitolewa vinywaji na Good luck Saria mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye alikuwa 'counter'.

Aliendelea kusema kuwa Good luck na Lightness walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miezi miwili na wote walikuwa wafanyakazi wa baa hiyo.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa, waliendelea kuwahudumia wateja waliofika katika baa hiyo hadi saa 8.30 usiku ambapo wengi wao waliondoka na kubakia wachache wakimalizia vinywaji vyao.

Amina alisema wakiwa wanawasubiri wateja wamalizie vinywaji vyao, Good luck alitoka 'counter' na kwenda kusimama nyuma ya kiti alichokuwa amekaa marehemu.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya dakika kadhaa kupita, mtuhumiwa aliingia 'counter' kisha baadaye akatoka na kwenda kusimama eneo alilokuwa amesimama awali ndipo walimsipomkia Lightness akilalamika kuwa alichomwa kisu na Good luck.

Aidha aliongeza kuwa, mwanzo walifikiri aliwatania lakini waliamini baada ya kumuona amelala chini huku damu nyingi ikichuruzika sakafuni ndipo walimwita mmiliki wa baa hiyo, Respis Francis Mrosso.

Mmiliki huyo alitafuta gari kwa ajili ya kumpeleka majeruhi hospitalini, lakini kwa bahati mbaya alifariki njiani.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya Good luck kufanya mauaji hayo, alitoroka na kwenda kusikojulikana ambapo mpaka sasa anasakwa na polisi.

Akizungumza na Ijumaa, mmiliki wa baa hiyo, Mrosso alisema kuwa, Good luck ni mwenyeji wa Old Moshi mkoani Kilimanjaro na kwamba alimpatia kazi baada ya kuletwa kwake na kijana mmoja wa kijijini kwao.

"Good luck aliletwa kwangu na kijana mmoja wa kijijini kwetu ambapo nilimpatia kazi, lakini baada ya muda wakawa na uhusiano wa mapenzi na marehemu, hivyo wakawa wanaishi pamoja," alisema Mrosso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Masindoki Masindoki amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kuahidi kufuatilia suala hilo kwa ukamilifu.


Mtanzania huyu kumponza Mengi
  • Ni mropokaji, anayeandika bila kufanya utafiti
Na Mwandishi Wetu
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Aberdeen, Scotland, Evarist Chahali huenda akamponza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ambaye pia ni mmiliki wa gazeti la Kulikoni, kufuatia habari potofu aliyoiandika kwenye gazeti hilo dhidi ya gazeti la Risasi.

Kwa mujibu wa habari hiyo, mwandishi huyo ambaye ni Mtanzania anayedai kuchukua kozi ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika chuo hicho, aliandika makala ya kuyashutumu magazeti ya Udaku kuwa yanaandika habari feki na kutolea mfano gazeti la Risasi.

Katika makala yake ya Jumatano Agosti 8, mwaka huu, Chahali alidai kuwa habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Risasi ambalo ni dada la hili, zilizoambatana na picha hazikuwa na ukweli wowote.

Chahali alitolea mfano wa habari iliyochapwa kwenye gazeti hilo la Julai 18-20 iliyokuwa na kichwa cha habari 'Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu'.

Habari hizo ambazo chanzo chake ni mtandao, zilieleza kuwa wasichana hao ni Watanzania waliopiga picha wakiwa watupu kwa nia ya kutangaza biashara ya kuuza miili ambapo waliweka bayana mawasiliano yao.

Hata hivyo, Chahali alidai kuwa habari hiyo ni ya uongo (feki), kwani picha zilizotumika ni za nyota wa sinema za ngono (porn star) wa Marekani na si Watanzania.

Mwandishi huyo alieleza katika makala yake hiyo kuwa, aliamua kuandika hivyo baada ya kuambiwa na rafiki yake anayeishi Marekani.

Akiongea na gazeti hili, Meneja Mkuu wa Kampuni inayochapa gazeti hilo, Abdallah Mrisho, alisema kuwa amesikitishwa na makala ya gazeti la Kulikoni ambayo haikufanyiwa utafiti wa kutosha.

"Habari iliyoandikwa na gazeti la Risasi ni ya kweli, hatujawahi kuandika wala haturuhusu wahariri wetu kuandika habari za uongo ndani ya magazeti yetu, ila Chahali ameropoka.

"Kimsingi mwandishi wa makala hayo, (Chahali) ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kuandika habari bila kufanya utafiti na kufikia uamuzi wa kushambulia gazeti letu bila kuwa na uhakika na alichokiandika", alisema Mrisho.

Mrisho aliendelea kusema ana wasiwasi hata na shahada alizonazo Chahali, kwani mtu mwenye elimu kama yake hawezi kuandika habari za kuambiwa bila kufanyia utafiti, hivyo kuupotosha umma na anaweza kumponza mmiliki wa kampuni inayochapisha gazeti hilo, ambaye anaheshimika sana.

"Chahali hakupaswa kutoa shutuma nzito kama zile kwa maneno ambayo hakuyafanyia uchunguzi na kuchapa kwenye gazeti, kwani anaweza kumponza mmiliki wa kampuni hiyo tunayemuheshimu, anapaswa kuona aibu (shame on him)," alisema Mrisho.

Kuthibitisha kuwa habari iliyoandikwa ni ya kweli, wahariri wa gazeti la Risasi wamelazimika kutaja anuani ya tovuti ambako wasichana hao wanapatikana, ili umma kwa ujumla uelewe nani mkweli kati ya Chahali na gazeti la Risasi, ingawa haikuwa kusudio lao kufanya hivyo.

Anuani hiyo ni http://swallowmyjuice.hi5.com ambako picha zilizotumika, mahali wanakoishi na utambulisho wa wasichana hao vinapatikana.

Aidha, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika kilichoko ndani ya chuo cha Aberdeen, Chahali ni miongoni mwa wanafunzi wasiofanya vizuri sana katika masomo yao.

"Chahali sio miongoni mwa wanafunzi wanaofanya vizuri sana chuoni," kilisema chanzo hicho.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kozi moja na Chahali katika chuo hicho ni pamoja na Timofei Agarin, Gordon G. Davidson, Joyleve Elliat, Anna Gustavon, Jeremy Lamoreaux, Giseong lee, Yang Lia, Khristus Vassis, Lortraine Whitty na Anna Zawak.

Mrisho alimtahadharisha mhariri wa gazeti hilo kuwa asipokuwa makini na waandishi wanaoandika makala zao kwa chuki binafsi kama Chahali, wanaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa.

Akiongea na mwandishi wetu kwa simu juzi, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya This Day na Kulikoni, Evarist Mwitumba alisema kuwa hana habari kuhusu makala hayo.

"Nipigieni kesho asubuhi, kwa sasa niko barabarani naendesha gari na sijasoma gazeti lililoandika habari hiyo," alisema Mwitumba.

Wednesday, August 8, 2007

HODI ULIMWENGU WA MUZIKI TANZANIA!

Huyu ni mtoto mwenye umri wa miaka 8 tu, lakini tayari ameonesha kipaji cha kuimba na ana nyimbo lukuki za bongo flava, anaitwa Miriam Edward..mzazi wake mzee Mwakionde anaomba wafadhali wampe sapoti..!
Mzee Kamarade.. Ali Choki, mambo yake siku hizi supa, ...anakaa 'Kinondoni, mtaa wa tatu kutoka kwa Manyanya'...!
Diouf.....rapa wa Chipolopolo! yaonekana ameanza kupendeza, wadau wanadai siku hizi habwii tena

FUMANIZI NDANI YA GESTI!

Na Waandishi Wetu

Jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Saidi Abedi mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, hivi karibuni amemfumania mkewe wa ndoa akifanya mapenzi na rafiki yake wa karibu.
Tukio hilo la aina yake na la aibu lilitokea Agosti 5 mwaka huu katika nyumba ya wageni (jina limehifadhiwa), iliyopo maeneo hayo.

Akizungumzia fumanizi hilo, Bw. Saidi ambaye ni mlinzi wa kampuni moja binafsi jijini alisema kuwa, kwa muda mrefu amekuwa akipewa taarifa kwamba, rafiki yake huyo aliyemtaja kwa jina la Fredy amekuwa akimzunguka kwa kuwa na uhusiano usiofaa na mkewe.

“Majirani zangu walikuwa wakinieleza kila mara kuwa ninapokwenda kazini usiku mke wangu anatoka na huyu rafiki yangu, lakini niliona ni uzushi kwani nilikuwa nikimuamini sana mke wangu.

“Leo nikawawekea mtego kwa kumuweka jamaa yangu karibu na gesti ambayo walikuwa wakiingia, mke wangu aliniaga kuwa anaenda gengeni kumbe alikuwa amepanga na yule rafiki yangu wakutane wakafanye uchafu wao.

“Nikiwa nasubiri matokeo ya mtego huo, jamaa yangu alinipigia simu na kuniambia kamuona mke wangu akiingia kwenye gesti hiyo ndipo bila ya kuchelewa nilienda na kufanikiwa kuwabamba laivu,” alisema jamaa huyo.

Ilizidi kuelezwa kuwa, baada ya Bw.Said kufanya fumanizi hilo, varangati zito liliibuka gesti hapo ambapo alianza kushusha kipigo cha nguvu kwa mgoni wake huku mkewe akibaki ameinamisha kichwa kwa aibu.

Hata hivyo, mgoni huyo baada ya kuona mambo yamekuwa makubwa alimuomba rafiki yake huyo alizime ‘soo’ hilo na kuahidi ‘kumpoza’ kwa kumpa shilingi laki tano lakini aliyefumania alizikataa kwa madai kuwa fedha hizo ni za shetani.

Aidha taarifa tulizozipata wakati tunakwenda mtamboni zimetanabahisha kuwa, mwanaume huyo amempa mkewe talaka na mgoni amekimbilia kijijini kwao Mlandizi kukwepa aibu hiyo.


CHUO KIKUU CHA WAISLAMU KUFUTWA...

Na Richard Manyota
Chuo Kikuu cha waislamu nchini kilichopo mjini Morogogo huenda kikafutwa na majengo yake kurejeshwa serikalini Amani limebaini.

Habari za uchunguzi zilizofanywa hivi karibuni na gazeti hili na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP) Mchungaji Christopher Mtikila zimebaini kuwepo kwa uwezekano huo.

Kufutwa kwa chuo hicho kutafikiwa endapo kesi inayoandaliwa na baadhi ya viongozi wa dini ya kikristo akiwemo Mtikila watashinda shitaka la majengo ya Tanesco ambayo ni mali ya umma kugawiwa kwa waislamu.

Awali Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini Mkapa aliwamilikisha waislamu majengo hayo ambayo kwa sasa yanatumika kama Chuo Kikuu cha waislamu, jambo ambalo linapingwa na Mchungaji Mtikila na wenzake.

Akiongea na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake Mchikichini, Dar es Salaam, Mchungaji Mtikila alisema, “Tumeandaa mashitaka kupinga waislamu kupewa majengo ya umma.

“Nchi hii sio ya waislamu peke yao, ni ya dini zote, sasa kuchukua mali ya umma ambayo inajumuisha dini zote na kuwagawia watu wa dini moja ni kosa, ndiyo maana tumeamua kufungua kesi ili majengo hayo yarudishwe kwa wananchi,” alisema Mtikila.

Aliongeza kuwa, maandalizi ya kesi hiyo yamekamilika, ingawa alisita kuwataja viongozi wa dini atakaoshirikiana nao katika kesi hiyo, ambayo alisema itaungwa mkono kwa maandamano ya wakristo kufanyika nchi nzima.

Aidha Mtikila alielekeza lawama zake kwa viongozi wa Serikali ambao alidai kuwa wamekuwa wakitumia mgongo wa dini kutafuta maslahi yao bila kujali athari zake, ambapo alitolea mfano hili la ugawaji wa majengo ya TANESCO.

Gazeti hili lilijaribu bila mafanikio kumtafuta Sheikh Mkuu wa Tanzania na baadhi ya maaskofu wa makanisa ili kufahamu jambo hili kwa kina. Kazi ya kuwasaka viongozi hao na wale wa serikali inaendelea.


Tuesday, August 7, 2007

MISS MATATANI BAADA YA FUMANIZI!


Na Imelda Mtema
Siku chache baada ya kumfumania Miss mwenzake, Mrembo wa Utalii mkoa wa Tanga 2005, Ania Saidi amekumbwa na balaa kubwa baada ya kubondwa na kuumizwa vibaya na kundi la watu wasiojulikana.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea usiku wa Julai 31, mwaka huu Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Akiongea na mwandishi wetu, Ania ambaye ni Miss Ngorongoro Crater na aliyewahi kushika mataji ya Miss Ubungo namba 2 mwaka jana, alipatwa na kimbembe hicho alipokuwa ameenda eneo hilo kumpitia rafiki yake.

“Nilikuwa nimeenda kumpitia rafiki yangu ili tuweze kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa rafiki yetu anayeishi Mikocheni,” alisema Ania.

Alisema alikodi gari dogo (taxi) kutoka nyumbani kwake Sinza Palestina hadi Mwananyamala na alipofika maeneo anayoishi rafiki yake huyo dereva huyo aliegesha gari naye kuteremka.

“Dereva alinishusha eneo hilo kwa sababu gari lake halikuweza kufika katika eneo analoishi rafiki yangu huyo”, alisema mrembo huyo.

Mrembo huyo aliongeza kuwa baada ya kushuka na kupiga hatua tano alistukia amekabwa koo na kupigwa na kitu kizito kichwani kabla ya kuanguka chini.

Akiwa chini, miss huyo alisema kuwa, alifanikiwa kuwaona vijana watatu ambao walimpora pochi yake iliyokuwa na cheni pamoja na simu vyote vikiwa na thamani ya shilingi 750, 000.

Hata hivyo, alisema aligoma kutoa vitu hivyo lakini alizidiwa nguvu baada ya mmoja wao kuchomoa kisu na kumkata mkononi huku wakimchania nguo na kumfanya abaki nusu uchi.

Alisema kuwa, baada ya tukio hilo vijana hao walikimbia na kumwacha akiwa na maumivu makali mwilini.

“Nilinyanyuka na kujikongoja hadi kwa rafiki yangu na kupiga simu kuwapa taarifa ndugu zangu akiwemo mchumba wangu,” alisema mrembo huyo.

Alisema kuwa, mchumba wake alifika kwa rafiki yake ambapo alimchukuwa na kumpeleka katika Hospitali ya Mico, Sinza jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

Ania alisema kuwa, anahisi vijana hao walitumwa na wabaya wake kumfanyia kitu mbaya, kwani wakati wakimpiga aliwasikia wakitoa maneno ambayo aliamini kuwa walikuwa wametumwa na mtu fulani.

Hivi karibuni Ania aliripotiwa kumfumania miss mwezake aliyefahamika kwa jina la Nadia Mohamed, Msasani Club jijini Dar es Salaam.



WEMA, KANUMBA KUKOMBA TSH. 180,000,000

Na Mwandishi Wetu
Miss Tanzania 2006/07 Wema Sepetu na Msanii wa Maigizo nchini, Steven Kanumba huenda wakakomba kiasi cha shilingi za Kitanzania milioni 180 endapo watashinda kesi watakayoifungulia kampuni inayochapa gazeti hili Global Publishers & General Enterprises.

Uwezekano huo wa kuukwaa utajiri wa chapchap umekuja, kufuatia wawili hao wiki iliyopita kuiandikia barua kampuni hiyo na kudai pesa hizo wakidai kuwa wamechafuliwa majina lao.

Katika barua mbili tofauti kwa kampuni hiyo ambayo imetolewa na Rattansi & Company, Advocates na kusainiwa na wakili wake Nasir H.Rattansi, Wema na Kanumba wanadai kuwa habari mbili zilizochapishwa na gazeti hili kwa matoleo yake namba 400 la Julai 18 na namba 403 la Julai 28 mwaka huu zimewadhalilisha.

Barua ya kwanza iliyokuwa ikilalamikia gazeti hili, ilihusu habari iliyosema kuwa ‘Wema, Kanumba wabambwa laivu’. Kwa mujibu wa habari hizo, wawili hao walionekana usiku katika Ukumbi wa Mercy Club, walikokwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa kwa msanii wa Kaole Rachel Kongojole.

Ilidaiwa kuwa Wema na Kanumba walishindwa kuingia ukumbini humo na kutulia kwavile walistuka baada ya kudokezwa kuwa kulikuwa na waandishi wa habari.

Hata hivyo, barua ya wakili wao ilidaiwa kuwa Si Wema wala Kanumba aliyekuwepo ukumbini humo siku hiyo, hivyo kudai fidia ya shilingi milioni 90.

Katika habari ya pili ambayo pia fidia ya shilingi milioni 90 inadaiwa, iliyomhusu Wema pekee na kupewa kichwa cha habari, ‘Hata aoshwe vipi, Wema hatakati’, ilidaiwa kuwa mrembo huyo ni miss wa kwanza nchini kukumbwa na kashfa nyingi za ngono.

Barua ya wakili wa Wema ilidai kuwa mteja wake si mhuni ‘kihivyo’ hivyo kulitaka gazeti hili kukanusha na kulipa fidia ya kiwango hicho cha pesa.



Two moons on 27th August 2007

*27th August; the day the Whole World is waiting for ......

Planet Mars will be the brightest in the night sky starting August.

It will look as large as the full moon to the naked eye. This will cultivate on Aug. 27 when Mars comes within 34.65 Million miles of earth.
Be sure to watch the sky on Aug. 27 12:30 am. It will look like the earth has 2 moons.
The next time Mars may come this close is in 2287.

Share this with your friends as NO ONE ALIVE TODAY will ever see it again.

BIG BROTHER AFRICA KUMEKUCHA!!!

BBA Guy...Mrithi wa Mwisho Mwampamba .. Richard Bezuidenhout...ndiye mwakilishi wa Tanzania katika shindano la BBA2 liloanza rasmi Jumapili iliyopita Afrika Kusini ...ubini wake ndo kasheshe..!
Deal or No deal.... Lola Opanga (kulia), Matanzania aliyewahi kushiriki lile game la Deal or no Deal na kujinyakuliwa USD 16, 500 (shilingi za kibonngo 20,000,000) akifurahi na Miss Africa wakati wa utambulisho wa BBA juzi Sea Clif Hotel.... mambo tambarale kwake..! (Sorry niliandika kwa makosa dola 60,000, thx for your comments)
Project Fame girl.... Nakaaya (kati) mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka jana akipozi na wadau wa Showbiz, Henry Mdimu wa gazeti la Mwananchi (kushoto), nami mdau wa blog hii, juzi katika uzinduzi wa BBA Sea Cliff Hotel. Binti ni ndugu dam na Miss Africa 2005, Nancy Sumary..imetulia!

MWONGOZO SAHIHI WA ULAJI


YUO ARE WHAT YOU EAT

Asalaam aleikum jaman! Bwana Yesu asifiwe sana! Tunakutana tena katika kona hii kuelimishana kuhusu staili ya maisha tunayopaswa kuitumia ili tuishi maisha yaliyo huru na maradhi, magonjwa na mateso mengine ya kiafya.

Wiki hii nataka kuwafundisha mwongozo bora wa ulaji sahihi kwa kufuata vipengele 10 katika ulaji wako wa kila siku, vitu unavyopaswa kuvila ambavyo vitaimarisha afya ya mwili wako na kukupa kinga madhubuti dhidi ya maradhi mengine.

Kuwa na afya njema inaweza kuwa kitu rahisi sana iwapo utazingatia vipengele 10 vya msingi vifuatavyo, ambavyo vitakupa angalau mwanga wa kitu gani kinafaa kufuatwa katika staili yako ya kula kila siku .

Jaribu kadri uwezavyo kufuata vipengele hivi na kuvifanya kuwa sehemu ya maisha yako. Hata hivyo usijilazimishe sana kama hutawezi kuvifuata vyote. Ukishindwa kuvifuata vyote, basi angalau jaribu kufuata ile sheria ya asilimia 80 kwa 20.

Sheria hiyo inasema kwamba iwapo utakuwa ukila na kunywa vizuri kama inavyotakiwa kwa kiwango cha silimia 80, basi hata kama ikitokea ukala na kunywa vibaya kwa kiwango cha asilimia 20, bila shaka mwili wako utaweza kukabiliana na vitu hivyo vya asilimia 20 na vitadhibitiwa kirahisi.

1: KULA MLO WA ASUBUHI (breakfast)

Anza siku kwa kula mlo mzuri ili upate kiwango kizuri cha nishati mwilini na kuwa na uwezo wa kujidhibiti na utakacho kula baadae siku hiyo, ikiwa ni pamoja na kula kiwango kidogo cha sukari na kahawa. Upe mwili wako nishati ya kutosha kwa kunywa uji wa ulezi, mtama au mahindi ya lishe.

2. KUNYWA MAJI YA KUTOSHA (drink enough water)

Kunywa lita mbili za maja kila siku, maji ni muhimu sana kwa ufanisi wa mwili wako. Unaweza kukaa wiki kadhaa bila kula, lakini huwezi kukaa muda huo bila kunywa maji. Kama hujazoea kunywa maji kiasi hicho, basi anza kujizoesha taratibu kwa kunywa kiasi kidogo hadi mwili utakapoweza kufikisha lita 2.

Unaweza kunywa maji kiasi utakachoweza kisha kiasi kingine ukakifidia kwa kunywa sana juisi za matunda, matunda yenyewe, kama vile papai, machungwa, lakini epuka kunywa kahawa. Kama tulivyoona wiki iliyopita, ukiona mkojo wako ni wa njano au kahawia na una harufu kali, elewa mwili wako umepungukiwa maji.

Kipimo kizuri cha kutambua kama umekunywa maji ya kutosha kwa siku, ni kujiwekea mazoea ya kununua au kutumbea na chupa ya maji ya ujazo wa lita moja, ambayo utainywa mara mbili kwa vipindi tofauti vya siku ili kufikia kiwango cha lita 2.

3. TUMIA KAHAWA KIASI KIDOGO

Punguza unywaji wa kahawa, kwa sababu kahawa huwa ni chanzo cha upungufu wa maji mwilini na la msingi zaidi kahawa hukausha maji mwilini! Vile vile kahawa huharibu virutubisho na madini mengi yanayoingia mwilini na vile vile inaweza kukuchangamsha kupita kiasi na kusababisha matatizo ya kiakili.

Jiwekee ukomo wa kunywa kikombe kimoja cha chai au kahawa kwa siku, usizidishe. Pombe vile vile nayo ina kilevi cha kuchangamsha mwili, hivyo nayo inapaswa kunywewa kwa kiasi kidogo na kwa uangalifu.

4. NUNUA VITU ASILIA (buy fresh)

Penda kununua vitu asilia na hai, kwani kadri vyakula hivyo vitakavyokuwa katika hali yake ya asili ndivyo ambavyo vitakavyoweza kukupatia virutubisho vingi mwilini. Usipenda kununua vyakula vya kwenye makopo na kuacha kununua vitu asilia sokono. Jaribu kununua kila kitu kikiwa halisi, mfano; kama ni nyaya iwe halisi na siyo ya kwenye kopo. Kama maharage, pika mwenyewe, usile ya kwenye kopo.

5. ANDAA MLO WAKO MWENYEWE (prepare your meal)

Andaa chakula chako mwenyewe, vyakula vilivyokwisha pikwa na vile viliivyokwisha tayarisha kabisa, huwa siyo bora kiafya, kwani mara nyingi huwekewa dawa za kuhifadhi na kuongeza maisha ya kukaa dukani, dawa hizo zaweza kuwa na madhara kiafya zinapotumiwa kwa wingi. Aidha vyakula hivyo huwa na kiasi kikubwa cha sukari, chumvi na mafuta mabaya. Unapoandaa mwenyewe chakula, utajua kipi kizuri ukiweke na kipi kibaya ukiache.

Itaendelea wiki ijayo.....

Monday, August 6, 2007

DUNIA TAMBARA BOVU, IMANI IMEKWISHA, INASIKITISHA!


MAUAJI YA KUTISHA

Na Makongoro Oging’
Mauaji ya kutisha yametokea katika mkoa wa Pwani ambapo mkazi mmoja wa kitongoji cha Mihande, Mlandizi wilaya ya Kibaha, Bi. Rehema Maskati ameuawa kikatili kwa kuchinjwa shingo na mume wake aliyetambulika kwa jina la Stivin Mayala ambaye naye alijiyonga hadi kufa baada ya tukio hilo.

Taarifa zilizopatikana mwishoni mwa wiki iliyopita kutoka kwa watu walio kuwa katika eneo la tukio, zilidai kuwa Bi. Rehema ambaye alikuwa mhudumu wa nyumba ya kulala wageni ya Taluka, Mlandizi mwili wake uliokotwa ukiwa katika dimbwi la damu wiki iliyopita majira ya asubuhi.

Mashuhuda hao ambao waliomba majina yao kuhifadhiwa, walisema kuwa inaonekana mwanamke huyo aliuawa katika eneo hilo kwani hakukuwa na mburuzo na damu zilionekana sehemu hiyo ya tukio tu.

Aidha walidai kuwa inasemekana mume wa marehemu alijua muda ambao mkewe alipita katika eneo hilo kwenda kazini kwake ndipo alimvizia kisha kumuua.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Bi. Rehema alikuwa ametengana na mumewe kutokana na migogoro ndani ya nyumba na alikuwa akiishi kwa dada yake huko Mihande ambapo Bw. Mayala alikuwa akiishi Mlandizi B.

Habari zaidi zinasema siku hiyo ya tukio bwana huyo alikutana na mkewe karibu na Mto Mkalama sehemu ambayo alifanyia mauaji, naye kujiyonga hadi kufa katika mti wa mkorosho hatua kama 30 kutoka alipolala mwanamke huyo.

Ndugu wa karibu wa marehemu Rehema ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alisema mwanaume huyo inadaiwa kuwa alishauriwa na mkewe wakati bado wanaishi pamoja kuwa atahiriwe kitu ambacho kilikuwa kinaleta mgogoro ambapo hata hivyo alikubali kutahiriwa ili waishi kwa amani.

Taarifa zaidi zinadai kuwa pamoja na makubaliano hayo, lakini kulizuka tabia nyingine ya mwanaume huyo kunywa pombe kupita kiasi kisha kurejea nyumbani usiku na mara nyingi alikuwa akikojoa kitandani jambo lililokuwa likimuudhi sana Bi. Rehema.

Aidha madai hayo yameelezwa kuwa ndiyo yaliyosababisha mwanamke akimbie na kuishi na dada yake. Hata hivyo, inasemakana mwanaume huyo alikuwa akimbembeleza mkewe waendelee kuishi pamoja waache tofauti zao, jambo ambalo Bi, Rehema alikuwa hajaafiki ndipo mumewe akafikia hatua hiyo ya kumuua naye kujimaliza.

Imeelezwa kuwa baada ya miili hiyo kuonekana na wapiti njia, ilitolewa taarifa polisi ambapo walifika katika eneo la tukio na kuichukua kwenda kuihifadhi katika chumba cha maiti Hospitali Teule ya Tumbi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Pwani, ACP Andrew Salewi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


MAUAJI YA SINDANO

Dotto Mwaibale na Issa Mnally
Kumeibuka mauaji mapya ya kutumia sindano ya sumu ambapo mfanyabiashara mmoja, Bw. Miasi Nyamatimo (30), Mkazi wa Vingunguti Kiembembuzi jijini Dar es Salaam amenusurika kufa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake usiku na kudungwa sindano mgongoni.

Tukio hilo la aina yake na la kuogopesha, limetokea Agosti mosi mwaka huu ndani ya chumba alichopanga mfanyabiashara huyo muda mfupi aliporejea kutoka kwenye shughuli zake za biashara ya kuuza ng'ombe na mbuzi kwenye mnada wa Pugu.

Akiongea na waandishi wetu wiki iliyopita, Bw. Nyamatimo alisema kwamba siku hiyo alirudi nyumbani kwake saa 2.00 usiku ambapo aliwakuta wapangaji wenzake wakiwa wameingia katika vyumba vyao kujipumzisha.

Alisema baadaye alitoka kwenda kuoga huku mlango wa chumba chake akiwa ameufunga, lakini alisahau kutoa ufunguo.

Bw. Nyamatimo aliendelea kueleza kuwa baada ya kumaliza kuoga aliingia chumbani kwake, ghafla alivamiwa na mtu na kukabwa koo huku akimkandamiza kwenye madumu ya maji yaliokuwepo nyuma ya mlango wa chumba hicho.

Alisema alilazimika kupambana naye huku akishindwa kupiga mayowe ya kuomba msaada kutokana na mtu huyo kuendelea kumkaba kwa nguvu huku akiwa ameufunga mlango wa chumba hicho kwa ndani akitumia mguu wake.

Nyamatimo alisema kwamba alimuuliza kama alikuwa anataka pesa ampe, lakini hakumjibu chochote na katika hali ambayo hakuitegemea mvamizi huyo ambaye alikuwa amevaa soksi ya kuficha sura kama ‘Ninja’ huku mikononi akiwa amevaa soksi za mikononi (gloves), aliingiza mkono wake mmoja katika kaptula yake aliyovaa na kuchomoa sindano ambayo alimchoma nayo mgongoni.

Alisema akiwa amekata tamaa na kuishiwa nguvu, ghafla alisikia kishindo kikubwa cha mlango huo ukifunguka na mvamizi wake kudondoka chini kisha alimuona mama mmoja mpangaji mwenzake aitwaye Mama Jordan akiingia ndani na kuanza kupambana na aliyemchoma sindano huku akisaidiwa na watu wengine.

Bw. Nyamatimo aliendelea kusema kwamba watu hao walimtoa nje mvamizi huyo ambapo waliendelea kumpiga hadi akapoteza fahamu kisha walipiga simu polisi ambao walifika na kuwachukua wote wawili na kuwapeleka Kituo cha Polisi Buguruni.

Alisema baada ya kufika kituoni hapo alidondoka chini na kupoteza fahamu ambapo alikimbizwa Hospitali ya Amana na kupatiwa matibabu na siku iliyofuata aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Alifafanua kuwa alipokwenda kumtambua mtuhumiwa huyo kituo cha polisi alishangaa kuona ni binamu yake ambaye siku za nyuma alikuwa akiishi maeneo hayo ya Vingunguti kwa shangazi yake mdogo.

Bw.Nyamatimo aliendelea kusema kwamba ndugu yake huyo alipohojiwa kituoni hapo alidai kuna mtu mmoja alimtuma aende akamuue kwa makubaliano ya kulipwa shilingi 500,000.

Afisa mmoja wa polisi wa Kituo cha Buguruni ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa sio msemaji, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea na upelelezi.


Ubalozi kulipuliwa?

Luqman Maloto na Mashirika ya habari
Hofu imeibuka kwamba huenda Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ukalipuliwa, kufuatia kitisho kilichotolewa hivi karibuni na mmoja wa wanachama watiifu wa Mtandao wa Al - qaeda, Adam Yahiye Gadahn.

Hofu hiyo imeibuka, wakati leo ndiyo inatimia miaka tisa, tangu Balozi za Marekani za Dar es Salaam, Tanzania na Nairobi, Kenya zilipolipuliwa Agosti 7, 1998 na kuua mamia ya watu.

Kwa mujibu wa video ya Gadahn, iliyonaswa na Shirika la Habari la CNN, mtandao huo unaandaa shambulio katika balozi zote za Marekani ili kulishikisha adabu taifa hilo kubwa duniani.

Gadahn, raia wa Marekani, alisema, lengo la kulipua balozi hizo ni sehemu ya mkakati wa Al - qaeda kuiwinda Marekani ndani na nje, kama ambavyo nchi hiyo inavyousakama mtandao wao.

"Tunaendelea kuiwinda Marekani ndani na nje, kama ambavyo wao wanavyotuwinda ndani na nje," ilisikika Gadahn ambaye pia anajulikana kama Azzam katika video hiyo.

Akiongelea kitisho hicho, Msemaji wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Richard Kolko alisema, wataalamu wanaifanyia uchunguzi video ya Gadahn kujua mahali alipo.

"Kuongezeka kwa ujumbe wa vitisho kutoka Al- qaeda, kunaweza kuonesha vitu tofauti na watafiti wetu wanafanya kazi na wapelelezi kutathmini kila ujumbe kwa alama na mwongozo," alisema Kolko.

BBA LAUNCH AT SEA CLIF

Ni hivi..... BBA itakuwa ikipatikana Channel 37 saa 24 kila siku, na show ya nusu saa kila siku M-net... Meneja Uhusiano wa MultiChoice Tanzania, Lucy Kwhele.. akiteta nami uzinduzini jana sea cliff Hotel
Mmhh...., Nikiwa na mrembo, Miss TZ 2, Jokate Mwegelo tukiwakilisha uzinduzini BBA 2 jana Sea Clif hotel

UCHAFU, USAGAJI!

Na Waandishi Maalum
Pamoja na Serikali kuongeza mkazo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi, inaonekana baadhi ya Watanzania bado hawajali, kwani hivi karibuni kamera yetu iliwabamba warembo wawili wakifanya vitendo vya usagaji chooni.

Warembo hao waliofahamika kwa majina moja moja, Khanifa na Mwaija (pichani kushoto), walibambwa Agosti 2, mwaka huu ndani ya choo kilichopo kwenye Ukumbi wa Baa ya Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakifanya uchafu.

Kamera yetu iliyokuwepo ukumbini humo kushuhudia burudani kutoka kwa Kundi la Jahazi Modern Taarab, ilitonywa na chanzo chetu kimoja kuhusu uwepo wa ‘kamchazo kachafu ka' warembo hao chooni.

Chanzo hicho, jinsia ya kike ambacho kilionesha kukerwa na uchafu wa warembo hao, kilitupasha kuwa, Khanifa na Mwaija walikuwa kero kwa watu wengine kwa sababu waligeuza choo kuwa chumba cha kufanyia mapenzi.

Kiliendelea kutanabahisha kwamba, warembo hao walikuwa wameingia chooni muda mrefu, lakini cha ajabu badala ya kutimiza kilichowapeleka, waliamua kufanya vitendo vya kusagana.
“Wanatia kinyaa, tunaomba mtusaidie, yaani wamevuana nguo, mmoja matiti yako nje, sisi wengine tukienda chooni ni kero tupu,” kilisema chanzo hicho.

Baadaye, katika kupata ukweli wa mambo, ‘paparazi’ wetu wa kike aliingia kwenye choo hicho ambapo aliwakuta warembo hao na kufanikiwa kuwapiga picha wakiwa katika pozi la kimahaba huku wakitomasana.

Hata hivyo, kutokana na kile kilichotafsiriwa kama ni kutokujali, warembo hao waliendelea na mchezo wao bila wasiwasi licha ya kushuhudia wakipigwa picha huku baadhi wateja wakiwataka waondoke chooni.

Aidha, baada ya paparazi wetu kufanikiwa kuwapiga picha wasagaji hao, chanzo chetu kingine kilichodai kinawafahamu warembo hao, kiliwataja majina yao kuwa ni Mwaija na Khanifa ingawa hakikuwatofautisha.

Kilisema, warembo hao wameshakubuhu kwa vitendo vya usagaji na mara wanapozidiwa na kilevi, hushindwa kujizuia na kufanya mapenzi sehemu yoyote.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba kwa sasa wasagaji hao wanaishi kama mke na mume nyumbani kwao, ingawa hakikusema ni sehemu gani ya Jiji la Dar es Salaam.

Gazeti linalaani vikali vitendo vya aina hiyo, kwani siyo tu kwamba vinakwenda kinyume na maadili ya Mtanzania bali pia vinachochea kasi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Tunaiomba serikali idhamirie kukomesha hali hiyo. MHARIRI

The Big Brother Guy - Mwisho Mwampamba.

Mwisho Mwampamba kafika MWISHO!
Na mwandishi wetu Morogoro

Mshiriki wa Tanzania katika Shindano la Big Brother Africa (BBA) mwaka 2003, Mwisho Mwampamba a.k.a Mr. Morogoro, amedaiwa kuwa muuza chips baada ya kufilisika kimaisha.

Mwisho anadaiwa ‘kuchoka’, wakati shindano hilo lililompatia umaarufu na mafanikio kiasi baada ya kushika nafasi ya pili, likizinduliwa tena jana nchini Afrika Kusini, baada ya kusitishwa kwa muda ambapo mshindi wa mwaka huu anatarajia kujipatia Dola za Kimarekani laki moja (shilingi mil. 130).

Ndugu wa karibu na Mwisho, alilipasha gazeti hili kuwa 'staa' huyo ambaye alishika nafasi ya pili BBA, anafanyia biashara hiyo ya kuuza chips katika eneo la Forest, mjini Morogoro.

Mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake gazetini aliongeza kuwa Mr. Morogoro anafanya biashara hiyo katika banda ambalo anachangia na kaka yake aitwaye Isambe Mwampamba.

“Mambo yamebadilika, kila kitu kimemuendea mrama, hivi sasa maisha yake ni ya kubahatisha kwa sababu hata hilo banda la chips halimuingizii pesa kama alizokuwa akizipata na kutumia hovyo kipindi alichotoka BBA," alisema ndugu huyo.

Mtoa habari huyo aliongeza: "Wakati mwingine anategemea michango ya ndugu, hivi karibuni ndugu yetu mmoja baada ya kuona kero zimezidi za kila mara Mwisho kumuomba hela, aliamua kumpa daladala ili awe anaendesha usiku.

"Kwahiyo kuna wakati usiku huwa anaendesha daladala ili kuganga njaa, lakini hapendi kuonekana, si unajua ni 'supastaa', kwa kweli tunamhurumia, Mwisho hakuwa mtu wa kupigika kiasi hicho, kwa sababu alikuwa ameshatoka kimaisha".

Jitihada za gazeti hili kumpata Mwisho azungumzie madai hayo ziligonga ukuta, kwakuwa lilielezwa kwamba yupo safarini Dar es Salaam, pia lilipojaribu kumsaka kwa njia ya simu ya mkononi halikufanikiwa kwani namba yake ilikuwa haipatikani.

Alipopatikana kaka yake Mwisho, Isambe Mwampamba alisema kuwa banda la chips ni mali yake, lakini watu wanavumisha ni la Mwisho kwa sababu huwa wanashirikiana, pia huwa anakwenda bandani hapo mara kwa mara.

"Banda ni langu na kwa kuwa Mwisho ni ndugu yangu kuna wakati tulikuwa tunashinda naye pale bandani, sasa watu wanadhani ni lake, ukitaka kuamini hivi sasa nimelifunga kwa sababu nimepata kazi Kiwanda cha Tumbaku," alisema Isambe.

Baada ya tetesi kuzagaa kwamba Mwisho 'ameishiwa', watu mbalimbali wamekuwa wakitoa maoni tofauti, kuhusiana na mabadiliko ya kimaisha ya Mr. Morogoro huyo.

Wakiongea na gazeti hili mjini hapa, wananchi kadhaa walisema, Mwisho amekumbwa na balaa hilo kwa sababu alikuwa mfujaji wa pesa.

"Aliposhinda BBA alipata mikataba mingi, ikiwemo kurekodi filamu Nigeria, lakini jamaa alikuwa mtu wa matanuzi," alisema Kulwa Ibrahimu wakati Happy Kushamu alieleza: "Mwisho alitaka kuishi kizungu ndiyo maana amewahi kuishiwa.”

Hata hivyo, Chris Kabala alisema, anaamini matatizo ya Mwisho yametokana na laana aliyoachiwa na aliyekuwa mchumba wake, Elpy Zembatakis ambaye anadai alimtosa baada ya kupata mafanikio BBA.

"Laana siyo mpaka itoke kwa wazazi, kitendo cha Mwisho 'kumwaga' Elpy hakikuwa kizuri kabisa, fikiria alikuwa ndiye mchumba wake kabla hajaenda BBA, lakini aliporudi 'alimtosa', hiyo ilikuwa ni laana kwa sababu yule dada aliumia sana.

"Mwisho hakujali alitaka 'masupastaa' wenzake, kama Ray C (Rehema Chalamila) ambaye walitesa na tukasikia walifunga ndoa, lakini haikudumu, mara Rah P (Fredinah Payton), wakatangaza wanaona lakini ndoa yenyewe ikawa hewa tu," alisema Chris.